ads

Saturday 9 January 2016

KWA WATUMIAJI WA 'SMARTPHONES'

Wengi hua tunasikia 2G, 3G H, H+ au E nk je maana yake ni nini?
Kwa kifupi ni kasi zinazotumika kusafirisha data kwenye internet ambapo zinatofautiana uwezo kutokana na teknolojia:
1. Herufi G huwakilisha GPRS (General Packet Radio Service) na ndio ndiyo toleo la kwanza la teknolojia ya simu. 
Hua inamaanisha kasi  ya internet yako ni ndogo sana (86kbps)

2. Herufi E huwakilisha EDGE (Enhanced Data Rates for GSM evolution) hua inamaanisha kasi ya internet yako ni ndogo ila ina afadhali kidogo kuliko G👆🏼(236kbps)
3. 2G (Toleo la pili)
Ni generation ya pili ya mobile phone technology ambayo nayo inatumia GPRS system lakini speed yake ni kubwa kidogo G, (154kbps) ila ni ndogo kuliko E yaani ipo katikati ya G na E.

4. 3G (Third Generation of mobile technology)
Inatumia UMTS & imejikiita kwenye  mfumo wa GSM, na ina kasi kubwa kuliko hizo 👆🏼(kasi yake 386kbps)

5. Herufi H huwakilisha HSPA (High Speed Packet Access)
Ni muendelezo baada ya 3G ambayo ina kasi kubwa (kama 3.2 Mbps)

6.H+ stands for enhanced HSPA, Yaani hii ina speed kubwa zaidi ya H kama nilivyoielezea👆🏼inauwezo wa kasi ya 7.2 Mbps, ndio inayotumika kwenye simu nyingi siku hizi.
7. 4G (Fourth Generation of Mobile phone Technology) pia inajulikana kwa jina la LTE (Long Term Evolution).
Toleo hii ndio jipya kwa sasa ambayo inatumia H+👆🏼na inakuwa na speed kubwa zaidi (kama 14.4mbps to 21mbps)

8. WCDMA huwakilisha Wide-band Code-division Multiple Access.
Inatumia teknolojia ya 3G ila imeongezewa GSM ambayo inaiongezea kasi ya kusafirisha data na ndio maana simu nyingi zimeitumia kabla ya kuja kwa 4G.


JAMBO LA KUZINGATIA;
Mbps: maana yake ni Mega bits per second yani kiasi cha data kinachoweza kusafirishwa kwa sekunde kwenye internet.
Kbps: maana yake ni kilobits per second, hii ni ndogo kuliko mbps👆🏼

1 kbps = 0.001mbps

0 comments:

Post a Comment