ads

Thursday 11 February 2016

LUPELA YA ALIKIBA INAPOLINGANISHWA NA TANGAZO LA VODA

Na.Mwanakalamu
Kuna matangazo mengi yanayotangaza bidhaa ambayo huwavutia watu wengi, kuna yanayokuwa na nyimbo ziizotamba, kuna yanayotungiwa tune na melody mpya, kuna yale yanayoinga lafudhi za makabila tofauti ya ndani na nje ya nchi na mengine kibao.Yote ni kuvutia hadhira ili ipate ujumbe uliokusudiwa.Naam pia katika matangazo hayo kuna yale yanayokuwa bora zaidi ya mengine na huvutia wengi sana wakati mwingine huwa kama kauli mbiu, unakumbuka ''we ndoroooobo''? naam hilo likageuka kauli mbiu.
Wiki iliyopita mwanabongofleva Ally kiba alitoa wimbo na video mpya ''Lupela'' video ambavyo vyote kwa pamoja vimetayarishwa chini ya usimamizi wa WildAid , inayoshughulika na kuzuia ujangili nchini na duniani kwa ujumla huku Ally akiwa miongoni mwa mabalozi wa kujitolea.Mengi yakaibuka, tene mengi yaliyotarajiwa, kuna sifa na ukosoaji wenye mantiki na ule usio na mantiki.
Ulipotoka wimbo rasmi nikautuma ule wimbo kwa watu kumi walio katika makundi ya watu matano ya watu wawili wawili, kulikuwa na kundi la waliojua mie ni shabiki wa Ally ambapo lakini hawakuwa wapenzi sana wa muziki, kundi lingine ni lile la wale ambao walijua mie nampinga sana Ally na kumbeza hao nao hawakuwa wapenzi sana wa muziki, kulikuwa na lile la wale waliojua kuwa sipendi sana kufuatilia muziki bali nasikiliza unaposikika, wawili wengine walijua kuwa naukubali muziki wa Ally na ni timu Kiba huku wao wakiwa ni wapinzani wake na kundi la mwisho lilikuwa likijua kuwa mie ni timu Diamond wao wakiwa ni timu Kiba.
Baada ya dakika tano nikaanza kupokea maoni mbalimbali kuhusu wimbo huo , sikuhangaika nayo kwani nilijua katika maoni hayo nitakutana na sifa na ukoisoaji usio na maana nilishawazoea nikaamua kuwasubiri wale wasio na upande huku nikisoma mawazo ya watu mbalimbali mitandaoni juu ya wimbo huo, hapo ndipo nikakutana na huu utani eti ''Tangazo la Voda ni bora kuliko wimbo wa Lupela'' Nilicheka sana ni utani mzuri ambao upande wa pili ulikuwa umewapatia mashabiki wa Ally.

Jana jioni ndipo nilipofanikiwa kupata maoni kutoka kwa watu wangu niliokuwa nimewatumia wimbo ule na kuomba tathmini yao , kwani wamekuwa wakinisaidia sana kwenye kupima nyimbo ambazo nashindwa kuziweka kwenye mizani kutokana na kutawaliwa na ushabiki katika kuzihukumu kuliko uhalisia.Yafuatayo ni mambo niliyoyangundua kwenye wimbo na video ya Lupela.

1.AUDIO HAIJAMALIZIKA 
 Ukiusikiliza wimbo uliowekwa kwenye mtandao wa Mkito.com utajikuta ukikunja sura kutokanna na wimbo huo kukata kienyeji sana.Kana kwamba wimbo unaendelea lakini utashangaa wimbo unaisha biti ikiwa juu , yaani msikilizaji anakuwa hajatayarishwa kuwa wimbo umefika mwisho.Hii inanipa shaka kwa mwanamuziki wa kiwango cha Alikiba kulifanya hilo ama uongozi wake kufanya hilo na kulipotezea huku watu wakitoa pesa kununua wimbo huo.

2.VIDEO KUWA NA SAUTI YA CHINI
Kwa wale waliobahatika kuingia youtube na kuitazama video ya wimbo huo watakubaliana nami kuwa video ina sauti ya chini ikilinganisha na audio yake.Sina uhakika kama video hiyo hiyo ya ubora huo huo imetumwa kwenye vituo vya tv na ikipokelewa.Kosa lingine dogo lenye athari kubwa kwa mwanamuziki mkubwa kwani aliowawekea wimbo huo huko ni wapenzi wa muziki amabo ndio walengwa wake na wateja wakubwa wa muziki huo.

3.ALIKIBA KAWAKARIRISHA
Licha ya kasoro zisizohitaji ufundi kuzitambua, bado kuna kundi kubwa la watu limejua kuwa Ally kiba huwa hakosei na yupo sahihi nyakati zote wakati kundi linginbe kubwa linaamini Ally hukosea nyakati zote.Kundi la kwanza hufikia hatua ya kuamini kuwa kundi lingine hulipwa hata pesa kuaminisha umma kuwa Ally kiba hukosea nyakati zote, wakati kundi linaloshutumiwa likiamini Ally hushuka kiwango kwenye kila wimbo si ajabu kusikia kundi hili likikosoa mavazi, rangi , wakati mwingine huweza kusifia audio na kuikandia video ama kusifia video ya nyuma ambayo wakati ikitoka waliikandia kupia maelezo.Madai haya ya kundi la pili yasiyo na mashiko wala utaalamu bila  hoja za kitaalamu huwafanya wa kundi la kwanza waamini kuwa kuna pesa iwatoayo watu ufahamu na kujenga chuki.
Kundi la kwanza nalo hukosea na kujikuta liiamini Ally ni mtaalamu asiyekosea na hata anapokosea hudai alikusudia kukosea na kuweka utofauti jambo amabalo si sahihi, kwani utaalamu usiojali mahitaji ya jamii si kitu kwani muziki ni kwa ajili ya wasikilizaji na watazamaji kama mwanamuziki atalilia kusimamia misingi na utaalamu wa muziki bila kujali mahitaji huweza kujikuta hafikii lengo alilokusudia.

4.TAALUMA NA VIPAJI VYA WATU HAVIHESHIMIWI
Katiko moja ya mahiojiano yake na vyombo vya habvari Professa Kitila Mkumbo aliwahi kuwatuhumu watanzania kuwa ni kati ya watu wanaoamini zaidi ushirikina kuliko sayansi.Hawataki kuamini tafiti wala taaluma ndiyo maana kila mtu anafikiri kuwa anaweza kufanya kila kitu.Ndiyo hata Tanzania ni hivi hivi chukulia mfano siku ile Rubi alipotukanwa kisa Ally kiba kuna waliodai kuwa hata kuimba hajui, hivi ni kweli Ruby hajui kuimba? ama wale waiowahi kudai kuwa Barnaba hajui kuimba , si matusi haya. Kuna wale wanaodai kuwa Ally kiba kazeka na hafai kuwa staa hivyo kila akiimbacho hakiweezi.
Pia kuan watu wanaokosoa hata utaalamu uliotumika katika kuiandaa video Lupela ,kuna vitu vinakera na huwafanya hata wanamuziki wetu wakitudharau hata tunapowashauri mema , ''Eti video ina kiwango kidogo'' labda hatujui taaluma za waandaaji wa mitindo wa kucheza hadi rangi za picha ama labda kwa sababu ni Ally au hatujazoea vitu vya mtindo huo, hilo silijui labda ni ule ushirikina aliousema Profesa Kitila.

5.ALIKIBA MKALI WA AKAPELA
Wakati inatoka Nagharamia kuna shabiki mmoja wa muziki alikereka na kuuchukia ule wimbo akisema jamaa wameharibu na hawajui chochote , balaa lilikuja alipomsikia Ally akiimba akapela hapo akajikuta akimwomba msamaha kimya kimya kwani hakuujua ukali wake kabla. Ndivyo ilivyokuwa kwa nyimbo nyingine kama Chekecha , wimbo huo ulinogeshwa kwa akapela zake huku mwana ikibebwa na gitaa kuingia kwenye mioyo ya wale wabishi.
Lakini pia mazoea yake ya kuchelewesha video hufanya nyimbo zake zibebwe na akapela apoimba kwenye vituo vya redi ama matamasha tofauti na wanamuziki wengine ambao video hubeba wimbo.Ni Dushelele na Lupela pekee ni nyimbo za karibuni ambazo zilitoka audio na video kwa pamoja.
HITIMISHO
Wimbo huo licha ya kuwa na mapungufu mengi una video iliyobeba ujumbe mkubwa kwa jamii yetu amabayo suala la ujangili ni suala gumu linalohitaji ushiriki wa kila mmoja kwenye jamii.Ally anabeba kilio cha tembo wengine na wazalendo wachache ambao wanauchungu na vitendo vinavyoendela mbugani.Wimbo huu hauhitaji tunzo za waandaiaji wanaojulikana bali unahitaji tuzo zetu wazalendo tukifichua kila hila za majangili ambao kuwashinda tunahitaji kumshiriisha Mungu kuwashinda kwani ni watu ambao kuuwa si kitu cha kutisha.
Mwisho utani wa kuwa wimbo huo si bora kuliko tangazo la voda ni kati ya utani bora amabo nimewahi kuusikia baada ya uchaguzi ukiwa sambamba na ule utani wa majina ya wanyama na balozi wa wanyama wote.Nilitamani hata mkito waweke lile tangazo la voda kabla ya Lupela kuanza ili tupate kulinganisha vyema.


0 comments:

Post a Comment