ads

Wednesday 10 February 2016

MIEZI SITA BILA YA JUA

Na.Steven Mwakyusa(Mtu makini)
Wakati ambao jua halizami kwa miezi 6, pia halichomozi kwa miezi 6 pia!!

Hili linaweza kuwa jambo geni na la kushangaza kwa walio wengi, ila ni jambo ambalo limekuweko toka kuwapo kwa hii dunia!!


Ifahamike kwamba chanzo kikuu cha nuru ipatikanayo duniani ni jua!! Na pia mchana na usiku ni matokeo ya dunia kujizungusha katika muhimili wake kwa saa takribani 24 ambayo inaitwa siku!! Imezoeleka kupata masaa 12 ya giza (usiku) pia masaa 12 na mwanga(mchana), lakini hali hii ni tofauti katika kizio cha kaskazini(north pole) pia kizio cha kusini (south pole)!!

Jambo hili hutokea dunia inapozunguka jua kila mwaka na mhimili wa dunia huwa umeinama kwa digrii 23.5 kutoka kwenye jua. Hivyo, wakati wa kiangazi katika Kizio cha Kaskazini, Ncha ya Kaskazini huinama kuelekea jua na wakati wa majira ya baridi kali ncha hiyo huinama mbali na jua. Kwa kuwa dunia huzunguka juu ya mhimili wake mara moja kwa siku, kwenye Mzingo wa Aktiki usikummoja kwa mwaka, yaani, karibu Juni 21, jua halitui. Vivyo hivyo, siku moja kwa mwaka, yaani, karibu Desemba 21, jua halichomozi, ingawa mchana huenda kukawa na nuru hafifu kama wakati wa mapambazuko.

Kadiri unavyoelekea upande wa kaskazini juu ya Mzingo wa Aktiki, ndivyo jua linavyokosa kuzama usiku wakati wa kiangazi na ndivyo jua hukosa kuchomoza siku nyingi wakati wa majira ya baridi kali. Kwenye ncha za Kaskazini na Kusini za dunia, kuna miezi sita ya mchana na miezi sita ya usiku.

Zamani, katika jamii fulani, watu walilala saa maradufu katika miezi ambayo jua halikuchomoza kuliko walivyolala katikamiezi ambayo jua halikuzama. Kuishi maisha ya kisasa kumewawezesha wengi kulala kwa muda uleule kila usiku. Lakini wakati wa kiangazi ambapo jua halizami, bado wakazi wa Kaskazini huwa na nguvu za ziada za kufanya kazi.

“Inapokuwa mchana kabisa saa 5:00 usiku, sijisikii kwenda kulala,” asema Patrick, anayeishi Alaska. “Nyakati nyingine mimi hutoka na kwenda kukata nyasi au kufanya kazi nyingine.”

Kwa upande mwingine, miezi ambayo jua halizami au kuchomoza inaweza kuchosha kimwili nakisaikolojia. Hivyo, watu fulani hujaribu kuzuia nuru isipenye kwenye chumba chao cha kulala katika miezi ambayo jua halizami na kutumia taa wakati jua halichomozi, ili kusawazisha wakati wao wa kulala na kuzuia uchovu na kushuka moyo.

Hata hivyo, licha ya magumu hayo, wakazi na wageni wanakubali kwamba kushuhudia jua likiangaza katikati ya usiku ni jambo lisiloweza kusahaulika.

Hali hii unaweza kuishuhudia katika maeneo ya kaskazini mwa Alaska, Kaskazini ya Russia, Norway, Sweeden, Finland pia maeneo mengi ya Iceland japo inaweza isifikie miezi 6!!

0 comments:

Post a Comment