ads

Thursday 25 February 2016

YA ALFRED WEGENER NA ''CONTINENTAL DRIFT THEORY''

Na.Steven Mwakyusa (Mtu Makini)
Ni miaka mingi imepita huku wanadamu wakijaribu kuja na nadharia mbalimbali kuhusu kuundwa kwa dunia na ulimwengu kiujumla!!
Moja ya nadharia iliyowahi kupata umaarufu mkubwa kuanzia miaka ya 1912 ni "continental drift"...Wegener ambaye ndiye muasisi wa hii nadharia, aliamini takribani miaka 300m iliyopita dunia yote ilikuwa na bara moja "Pangaea", na baadaye Pangaea ilianza kugawanyika na kupata mabara tunayoyaona sasa yaani Ulaya, Afrika, Amerika ya kusini na Kaskazini, Asia, Australia na pia Antarctica!!
Wegener aliweza kutoa mifano hai katika kuthibitisha kile alichokuwa akisema, kubwa likiwa ni muonekano wa pwani za mabara mbali mbali hasa Afrika ya Magharibi na Amerika kusini!! Vipande hivi vikiunganishwa hakika vinafiti kwa kila kimojawapo!! Lakini hoja hii ya Wegener ilishindwa kusema kwanini baadhi ya vipande vikiunganishwa havileti picha ya kuwa kitu kimoja!!
Wegener pia alijenga hoja kuhusu mfanano wa miamba katika milima kati ya Amerika ya kusini na Afrika, mfano miamba ya Santa Catarina ya Brazil ina ufanano ule ule na miamba ya Karroo ya Afrika ya kusini!! Vile vile miamba inayotengeneza milima ya Appalachian ya Marekani ina ufanano na milima ya Caledonian kule Scottland!!
Mfanano wa wanyama wa majini pia wale wa mwitu kati ya Afrika na Amerika ya kusini ilitumi kama hoja ya kusema haya mabara yalikuwa pamoja kabla!!

Pia kupatikana kwa makaa ya mawe katik kizio cha kusini cha dunia yaani Antarctica kulitumiwa kama uthibitisho kwamba bara lilihama toka maeneo ya Ikweta na tropical ambayo yanaruhusu miti na uoto (ambayo ndiyo chanzo cha makaa ya mawe), hivyo basi bara la Antarctica lilihama baada ya kutokea deposition ya "fossils" ambayo ndiyo iliyotengeneza hayo makaa..Wegener aliamini hivyo maana hakuna uoto wowote unaopatikana huko katika kizio cha kusini mwa dunia!!
Mpaka Wegener anafariki mwaka 1930 ikiwa katikati ya utafiti wake kuelekea Greenland, hakuweza kusema ni kipi kilisababisha hayo mabara kumove!! Baadaye baadhi ya watafiti miaka ya 1950 na 1960 waliweza kugundua kile kinachoitwa "Plate tectonics theory"
Je inawezeka Plate tectonic theory ilitoa majibu juu ya nguvu iliyokuwepo nyuma ya continental drift?? Je continental drift theory bado ina mashiko katika dunia ya leo??

0 comments:

Post a Comment