ads

Wednesday 9 March 2016

YAJUE HAYA KUHUSU PESA !!

Na.Steven Mwakyusa(Mtu Makini)
Ugunduzi wa pesa karne nyingi zilizopita umeleta mapinduzi makubwa sana kiuchumi na ustawi wa maisha ya mwanadamu kiujumla!! Mengi yamekuwa yakisemwa kuhusu pesa, wengine wakidai pesa ni shetani huku wengine wakienda mbali na kudai pesa ni makaratasi yaani si chochote na si kila kitu!!
Je ni kweli pesa si chochote? Maisha yanawezekana bila pesa? Kama pesa ni makaratasi kwanini zisichapishwe za kutosha kila mtu awe nazo? Kujibu haya yote ebu tuanze kuangazia historia ya pesa/hela/fedha!!
Ki historia tumepita hatua tofauti ya kiuchumi
Barter trade: Hapa watu walikuwa wanabadilishana mali. Mwenye mbuzi akitaka mchele atamtafuta mwenye mchele. Ila tatizo lilionekana pale ambapo yule mwenye mchele kama hataki mbuzi inakuwa ngumu kwa mwenye mbuzi kupata mchele. Ndio hatua ya pili ikafuata ambayo ni:
Commodity money: Hii ilikuwa ni kutumia vitu vya thamani kama mchele, shells (za baharini). Ila baada ya kugundua fedha na dhahabu na kuonekana kuwa ni adimu na haziharibiki haraka ndio zikawa zinatumika sana na kuanza kutengenezewa sarafu (coins). Sifa za pesa za namna hii ni kuwa ile pesa yenyewe inaweza kutumika. Mchele utapike ule, dhahabu unaweza kutengeneza vitu vya urembo n.k. Ile pesa yenyewe ina thamani. Ila baada ya coins kuwa nyingi hususan za fedha zenye thamani ndogo, na Benki za mwanzo kuanzishwa (na wachimba dhahabu kuhifadhi dhahabu za watu) kulikuwa na haja kuboresha exchange of currency baina ya watu bila ya kubeba ma kilo ya ma coins.
Representative money: Wakati huo ndio ma Benki ya mwanzo (ilikuwa zaidi ni store za kuhifadhia dhahabu. Sio kama mabenki ya kisasa) walikuwa wanatoa bank notes zinazoonyesha una kiasi gani katika dhahabu hiyo. Kwa hivyo kama umehifadhi kilo kumi ya dhahabu utapewa bank note yenye kuonyesha una kilo kumi ya dhahabu. Ukitoa kilo tano utapewa bank note kuonesha una balance ya kilo tano n.k. Hili jambo liliwafanya watu waanze kutumia bank note mitaani badala ya kutumia zile dhahabu. Kwa mfano mnunuzi anampa muuzaji bank note ya kilo ya dhahabu na badala ya yule mnunuzi kuenda banki kutoa zile dhahabu, anatumia bank note ile kununua vitu anavyohitaji.
Baada ya wamiliki wachache wa mabenki yale wameona kuwa watu hawatumii dhahabu tena bali bank notes, wizi ukaanza. Na huu wizi ndio umesababisha kuanzisha na hatua ya nne ya pesa ambayo ni
Fiat Currency: Wizi ninaouongelea hapo ni wamiliki wa benki hizo wakaanza kujichapisha bank notes pasi kuwa na mali ya dhahabu. kwa vile alikuwa anajua kuwa watu wanahifadhi tu dhahabu lakini hawatumii, alikuwa akijiandikia bank note na kununua mali za watu atakavyo.
Watu kipindi hicho walishtuka sana baada ya kuona wamiliki wa mabenki (nikisema benki hapa namaanisha store za kuhifadhi dhahabu) yale kutajirika kupita kiasi kila mmoja akaanza kudai dhahabu zake. Kwa vile bank notes zilikuwa nyingi kuliko idadi ya dhahabu, wamiliki wa benki ile walishindwa kulipa kitu kilichowafanya wanyongwe. Ila serikali iliona faida fulani ya kuchapisha hizo bank notes katika kukuza uchumi kwa haraka lakini inatakiwa kuwa under supervision kwani ikifikia wakati kila mmoja ana $1 Million, $1 Million moja haitokuwa na thamani. Na hiyo ndio sababu kubwa mabenki hawachapishi pesa (currency) ovyo kwani pesa itashuka thamani.
Tukirudi kwenye hoja ya msingi, what is money? And what is currency?
Money: Is anything of value which can be provided in the market place. Kwa hiyo idea yako, knowledge, workforce, your labour, Asset. All of that is money.
Na kwa nchi ili itajirike LAZIMA vitu vyenye kuleta thamani katika nchi ndizo zitasababisha uchumi kukuwa sio currency.
Currency: This is a medium of exchange to get something of value. Hiki ni kitu kitumikacho kwa ajili ya kupata kitu chenye thamani. Lakini kitu chenyewe hakina thamani. Ukiwa na billioni moja sasa hivi. Hizo pesa (currency) hazina thamani lakini kinaweza kukusaidia kupata vitu vyenye thamani.
Take home message ni nini: Ukitaka kukuza uchumi wako binafsi au hata nchi, inabidi kutafuta Pesa zenye thamani (Money) na sio Pesa zisizo na thamani (currency)
Kupewa Ma billioni ya pesa na pesa (currency) hizo kusambazwa, kama pesa (currency) ni kidogo kuliko pesa za kweli (money) zilizokuwemo nchini, basi pesa hizo (currency) hushuka thamani.
Na tunadanganyika kuwa vitu vinapanda bei. Hapana, kilo ya nyama itabakia kuwa kilo ya nyama na kilo tano za dhahabu zitabaki kuwa kilo tano za dhahabu. Pesa ya uongo (currency) ndio inashuka thamani sio pesa ya kweli (money).

0 comments:

Post a Comment