ads

Wednesday 9 March 2016

HONGERA ALIKIBA, KWA HILI UTAKUWA UMEJIFUNZA KITU

Na.Mwanakalamu
Wiki hii ilianza kwa taarifa nzuri kwa upande wa filamu nchini ''Bongo Movie'' ambapo wasanii wawili wa upande huo Richie na Elizabeth Michael ''Lulu'' walifanikiwa kurudi na Tunzo ambazo zimewashtua watu wengi ambao tumekuwa tukizipuuza filamu zetu za ndani kwa kuzikosoa na kuziona si kitu.Lakini katika tunzo hizo zilizokuwa zikifanyika Nchini Nigeria kulikuwa na mtanzania mwingine ambaye alipata nafasi ya kutumbuiza , huyo si mwingine ni Alikiba.
Alikiba mshindi watunzo za tunzo za Kili mwaka uliopita katika vipengele vingi kikiwemo kile cha utumbuizaji bora ambacho kiliibua hisia za ''kubebwa'' hasa pale alikiwa mshindani wake mkubwa katika kipengele hicho Diamond Plutnumzkutwaa tunzo hiyo kwa Afrika katika tunzo za MTV ingawa jambo hilo si geni kutokea kwani iliwahi kutokea hata kwenye soka kimataifa pale Mchezaji mahili duniani Christiano Ronaldo alikosa tunzo ya ndani ya taifa lake mbele ya Pepe halafu akatwaa ya Dunia.
Tuyaache hayo ya tunzo , tuje kwenye hili lililonifanya niandike juu ya alichojifunza Alikiba na ambacho wanamuziki wengine wanatakiwa kujifunza baada ya Ally kutumbuiza huko Nigeria.Nimeitazama ile ''show'' kupitia tovuti ya African magic ambapo alitumbuiza wimbo wa Mwana akiwa na bendi na ''madancer'' waliojitahidi kucheza kwa ustadi wa hali ya juu.Lakini nilipata shaka juu ya ukubwa wa mwanamuziki huyu ambaye hapa ndaniwengi tunaamini ni mwanamuziki mkubwa ambaye mara nyingi jina lake huwa linalinganishwa na Diamond mshindi wa MTV EMA kwenye utumbuizaji bora.
Ndiyo kwa hapa ndani jina la Ally limekuwa na pacha kwa jina la Diamond ni kama ilivyo kwa Simba na Yanga hata kama kutatokea Azam mia lakini Simba na Yanga zitabaki kuwa timu zinazojaza uwanja wa Taifa, lakini kwa Afrika bado sana majina ya wanamuziki hawa kuwa katika mzani mmoja , Mweke Diamond hapa pale mweke Davido ama KCEE na si Alikiba.
Kwa nini hili limetokea kwa mwanamuziki mkubwa na mkongwe kama Alikiba?
Ukweli ambao Alikiba alikuwa anaukataa daima na kuwaaminisha washabiki na wafuasi wake kuwa yeye alishajulikana Afrika na hata duniani akitumia ile ''Project'' ya One 8 lakini katika uhalisia Alikiba hakufika kuwa mwanamuziki wa Afrika kwa kuimba katika project hiyo kama haamini amwangalie Aman ama yule wale wenzake ukiachana na 2 face na Fally ambao walikuwa tayari ni wanamuziki wa Afrika kabla ya kwenda huko.
Hivyo kwa kuimba na one 8 kisha kurudi pale walipoishia si tiketi ya wao kuwa wanamuiki wa Afrika bali ilihitajika nguvu kubwa kuwekeza katika muziki ili ''kuikamata'' Afrka na Dunia kwa ujumla badala ya kurejea ''bongo'' kisha kuendelea na muziki wa kufanyia show Dar Live ama Escape one ama kwenye jukwaa la Fiesta na si kwenye tunzo za Mtv ama AFRIMA kule Darbun ama Lagos.
Maendeleo ya sayansi na teknolojia inayounganisha watu kutoka pande zote ya duni a yameongeza maingiliano ya tamaduni na mitindo ya maisha kubadilika na kuufanya muziki moja kati ya vitu vingi vinavyoingiliana na kuunganisha tanaduni tofauti.Hilo likawafanya wanamuziki kuanza kufanya nyimbo za pamoja ili kuongeza wafuasi wa ndani na nje ya Afrika jambo ambalo Alikiba amekuwa akilipinga na kuamini muziki wake pekee utafika kule walikofika wengie wakati mwingine amekuwa akijidanya na kuudanganya umma kuwa ameshafika huko, ila kwa hili la juzi , 'atakuwa kajifunza kitu'.
Raha ya mwanamuziki anapotumbuiza ni kuwasikia anaowatumbuizia wakifuatisha walau maneno machache ya wimbo na kama lugha ngeni sana basi wataiga uchezaji wako ama midundo ya ngoma , hilo juzi halikufanyika zaidi ya wale watanzania wachache (wasiozidi watano) walioamua kutia shangwe huku wengine wakimwona ni kama mtu mgeni kabisa kwenye muziki wa Afrika.
Kwa nini iwe hivi?
Jibu hapa ni ule ukweli mchungu kwa Alikiba na wafausu wake kuwa hana wimbo ulioikamata Afrika si kwama nyimbo zake si nzuri. Hapana nyimbo zake zinafaa hata Ameika na Asia tatizo ni kuwafanya hao waamerika na waasia kuzisikiliza hizo nyimbo.Nyimbo anazifanya kuwa za taifa ndiyo kila taifa lina wimbo wake na mtu wa taifa lingine ajifunze wimbo wa taifa lingine bila sababu haiwezekani hivyo yahitajika nguvu kubwa kumshawishi hapo mbinu mbalimbgali huhitajika ikiwa ni  pamoja na kuimba na mwanamuziki wa kwao wanayemkubali, kuimba vizuri, kwenda kutambulisha nyimbo kwao na zaidi kwenda kufanya matamasha kwao hata kama ni bure ama kwa bei ndogo ili baadaaye uje kupata maradufu.Ingawa kuna wanamuziki wanaoamini kuwa soko la ndani ya nchi hii linatosha lakini ipo haja kubwa ya kutanua soko la nje na kuleta ule ''Ukimataifa'' wa Mwanamuziki huyo.Kwa hali ya juzi najua amejifunza.
Jambo la pili ni kutumia vyema mitandaoya kijamii, Muziki ni moja kati ya sekta chache zinazokimbizana sana na teknolojia mitandao ya kijamii inaweza kuwa nyenzo kubwa ya kuufanya muziki wa mwanamuziki fulani kufika mbali.Alikiba ana mashabiki wengi ndani ya Tanzania na wachache Kenya na wachache sana nje ya Afrika mashariki ili akamate nje ya hapo anatakiwa pia kutumia mitandao ya kijamii vyema wakati mwingine inashangaza hata kwenye chaneli yake ya youtube haina nyimbo zake zote ana nyimbo chache ya kwanza ikiwa ni mwana na matamasha machache nani ataamini kuwa ndiye aliyeimba Cinderela kama amemfahamu Alikiba kwenye Mwana.Mnigeria gani ama Mghana gani ambaye atajua kuwa alikiba alifanya show ya Maana kwenye Sauti za Busara kam hata haioni hiyo show youtube? Huu ni utani ila kwa hili la juzi ATAKUWA KAJIFUNZA KITU.
Jambo lingine ni kuwaambia mashabiki na wafuasi wake wanaoamini kila kitu na kumwona Ally hakosei na hahitaji mawazo ya kumjenga ma walimzunguka pekee wanamtosha  ukweli.Atawaambiaje/
Weka Behind Scene ya video zako .Hii itasaidia hata wale wagumu kuelewa dhana za video kuzielewa.Najua show ya Nigeria imemmfunza.
Nimalize kwa kushauri Alikiba na wasimamizi wake kuangalia uwezekano wa kufanya matamasha ndani na nje ya Afrika mashariki kwa manufaa yake na wafuasi wake ambao daima wanahisi huwa anaonewa ama kufanyiwa mchezo mchafu pale anapokosa tunzo kubwa ama anapokosa kushiriki kwenye matukio kama hili la juzi kwani.Ukweli kuwa hata Kiss Daniel anawezaa kuwaimbisha na kuwarusha wanyarwanda ambako wako jirani kabisa na kule kijijini kwa bibi ''Kigoma'' kuliko Alikiba kutokana na hili la kujitangaza.Wanaijeria wametengeneza soko la ndani ambalo ni kubwa na la nje kwa kuwatumia wale wachache wenye nguvu na kuifanya kazi ya chipukizi kuwa rahisi na ile tuu kusema mwnamuziki katoka Nigeria huwapa nafasi ya moja kwa moja ''Kutusua''Kwenye nchi zetu.
Najua ukweli unaujua na ulikuwa ukiujua siku zote ufanyie kazi Ally, usiwadanganye watu kwa kuimba na Sauti Soul unaweza kuwateka wa Mali, waghana ama Wasauzi bali unahitaji nguvu nyingi katika kuwekeza kwenye muziki wako ili tuu jina lako ulilolitengeneza ndani ya nchi liwe kubwa pia nje ya nchi wakati mkihangaika kuwa na uhakika wa kufanya show zenye hamasa na wingi wa watu huko ng'ambo.
Hongera Alikiba hongera watanzania Ukweli huishi milele, ila unafiki hutuporomosha na si kutujenga.
Naomba kuwasilisha.


0 comments:

Post a Comment