ads

Monday 4 April 2016

WANAMUZIKI WALIOFANYA KOLLABO ZIKA 'HIT' WAKAPOTEA

Na;Steven Mwakyusa (Mtu Makini)
Katika muziki wa bongofleva kumewahi tokea wasanii ambao walihit katika nyimbo walizoshirikishwa na baadaye watu wakawa na hamu ya kuwasikia katika nyimbo zao wenyewe, ila matokeo yake yalikuwa tofauti!
Ebu tujikumbushe wasanii waliong'ara katika nyimbo walizoshirikishwa na baadaye wakashindwa kusimama wenyewe!!
1. Mishi- Huyu kwa mara ya kwanza alisikika katika wimbo wa Selina wa Alicom, baadaye akasikika katika Chonde chonde ya Nuruel, Pole kwa safari ya Juma kakere pia Nimeridhika naye ya Qchief, baada ya hapo sina kumbukumbu kama aliwahi imba wimbo wake mwenyewe achilia mbali kusikika katika collabo nyinginezo!!
2. Zahran-Huyu ni msanii aliyesikika na kufahamika katika wimbo wa Abby Skills(Nilikupenda), baadaye alikika katika Sikuoni ya Alikiba, baada ya hapo ni kimya mpaka leo!!
3. Lil Gheto-Huyu kwa mara ya kwanza alisikika katika wimbo wa Ji(Kidato kimoja), baadaye alisikika katika nyimbo za Berry Black na AT, na mpaka leo hajawahi tengeneza hit yeyote kama Solo artist!
4. Scount Jentaz-Hawa kwa mara ya kwanza walisikika katika nyimbo za DNF, huku Jirushe(Original version) ikiwapa jina mjini kwa kipindi hicho, mwisho wa DNF ukawa mwisho wa SJ pia huku wakiwa hawajatengeneza hit yeyote!!
5. Miss Sarah- Huyu naye alisikika katika wimbo wa Caz T, Nakuhitaji (Angwisa), baada ya haoo hakuweza tena kusimama mwenyewe!!
6. Simple X- Huyu alisikika katika hakuna noma ya Prof J pia katika Nawakilisha, baadaya ya hapo haijulikani aliimba nini tena!!
Wengine ni pamoja na
-Josephine-Kibanda cha simu(Soggy)
-Aliyeimba chorus ya Tumbo Joto(Kali P)

 

0 comments:

Post a Comment