ads

Monday 4 April 2016

LA MADANSA NA KISA CHA KIATU KIPYA


Na.Mwanakalamu
Natumai kila mtu aliwahi kuwa mtoto, na kwenye utoto kuna vituko vyake vya kuaibisha, kuchekesha , vya kujivunia na vya kujifunza pia.Kuna kisa niliwahi kusimuliwa na mama yangu kuwa kipindi hicho nikiwa mdogo siku moja nilinunuliwa viatu , ilikuwa usiku kama wa saa mbili nikapewa kuvijaribu vilinitosha vizuri sana miguuni na vikanipendeza.Sikutaka kuvivua vile viatu baada ya kuvijaribu , siku iliyofuata ilikuwa ya jumapili hivyo ningevivaa niendapo kanisani lakini kwangu ilikuwa ngumu kuvivua hadi walivyovivua kwa nguvu.
Kisa nilivipenda sana.
Asubuhi mama alivyokuja kuniamsha alikuta nimevivaa, yaani nilikuwa nimelala nikiwa nimevivaa, hakujua nilivivaa muda gani hata mwenye sikumbuki maana nilisimuliwa tuu.
Siku ya jumapili niliwahi kanisani kuliko mtu yeyote nikiwa na viatu vipya huku wakati 'Sunday School' inaendelea nilikuwa nikiweka viatu juu ya mabenchi ya kanisani ili wavione hayo mama alisimuliwa na mwalimu wetu wa Sunday school ambaye alikuwa jirani yetu lakini mbaya zaidi nilitamani niingie na viatu hadi bafuni.
Tuachane na kisa hicho hapo juu kuna kitu kimeibuka kwenye muziki wetu wa hapa nyumbani, bongofleva.Kila mwanamuziki ana wacheza shoo wake maarufu kama madansa, hawa kazi yao ni kutumbuiza mwanamuziki akiwa jukwaani huku wakiifanya hadhira iburudike mara dufu.
Akipanda Diamond, na madansa wake wakicheza ndogo mdogo utapenda, Vanessa naye akicheza Closer yake weh! hadi raha Alikiba naye akija na mwana basi wee watu oyeeee!
Kero pale Diamnd akiimba lala salama huku madansa wake wakinyonga nyonga na kucheza kwa staili walizobuni, hapo unaweza jutia hela yako ama Alikiba akiimba Mapenzi yana run dunia huku wale jamaa wakijikunja kunja unaweza tema mate kabisaaa.
Tusishangae Ditto na yeye akaja kuimba Wapo na madansa wakijipinda kufuata muziki wake Duh! kama enzi zangu nalala nimevaa kiatu.
Hili halihitaji kwenda Bagamoyo kuujua muziki ama kuwa na DSTV nyumbani kujua nini cha kufanya bali fikra nusu ya punje ya haradani huweza kutuonesha cha kufanya kuliko kufanya kama mie nilivyojitesa kwa kulala na viatu.
Nyimbo kama lala salama, mapenzi , kamwambie na hata wife wa dunia ambayo kidogo Ally amejitahidi huimba mwenyewe, hizo ni nyimbo za kuwaimbia wanawake hapo ndo utakuta mwanamke anazimia kwa hizia hapo ndipo fleva wa Nigeria huwafanya wadada watamani hata kumgusa na wakimgusa hutokwa na chozi la furaha lile chozi la kumfariji mwanamuziki kwa anagusa mioyo ya watu na si kuturusha watu jukwaani huku ukiimba Cinderela, Sophia ama Mbagala .
Eboh! hilo nalo Jeep.

0 comments:

Post a Comment