Thursday, 7 April 2016

HUYU NDIYE 'KID BOY' NINAYEMTAKA

Na;Mwanakalamu
Kwa wadau wa Bongo fleva miaka ya 2000 hakuna ambaye hakumfahamu kijana huyu aliyewavutia wengi kuwa watangazaji wa redio.Anaitwa Sandu George Mpanda maarufu kwa jina la Kid Boy , ni mtangazaji hodari akiwa mmoja wa ule 'utatu mtakatifu' wa Kipindi cha Show Time akiungana na Dj John na Mtoto wa mama Sabuni Glorie Robinson Sabuni, kilikuwa ni bonge la kipindi.Hawakuwa moja wa wale watangazaji wa ''Kitu flani ameizing' hawa walikuwa wakitangaza kwa kiswahili safi siwezi kusema sanifu kutokana na utata wa neno lenyewe usanifu lakini kilikuwa ni kiswahili rasmi.
Kid pia alikuwa mtayarishaji wa muziki pia msimamizi wa wanamuziki , Husein Machozi, Sagna, Baraka Da Prince ,C sir Madini na wengine wengi wamepitia kwenye mikono yake ama akiwa mtayarishaji wa nyimbo zao au hata kuwasimamia lakini kama sikosei alikuwa akihusika kwa kiwango kikubwa katika kuandaa matamasha makubwa ya muziki yaliyokuwa yakifanyika Jijini Mwanza.
Unaikumbuka ''Maneno'' ya Mheshimiwa Temba? Kidboy alihusika katika kuitia kachumbali.
Septemba 2010 nadhani ni mwaka mbaya kwake kama ilivyokuwa kwa mashabiki wake pale alipokutana na janga lililomsababishaia maumivu na hofu kwetu ambao hatukuwa tukibanduka redioni kujua hali yake.Nakumbuka kipindi hicho nikuwa shuleni licha ya kuwa tulikuwa tukizuiwa kuwa na redio kwangu niliona ni makosa kukaa bila kujua hali yake si kwa kuwa alikuwa akinifahamu bali kwa sababu ya uhodari wake katika kutangaza na kuuchambua muziki wa bongo fleva.
Miaka kadhaa baadaye nikashangaa kutomsikia tena redioni hadi pale nipohangaika kutafuta taarifa mtandaoni , nilipokutana na kile kilichoitwa 'tone redio' redio iliyopatikana online na kuambiwa kuwa alikuwa mmoja wa waanzilishi na watangazaji wa redio hiyo ambayo sikupata kuisikia kutokana na kuwa mbali na intanet hadi pale nilipomsikia kwenye Milazo 101 ya Radio one kisha kumwona Bongo 5 hapo nilifarijika kuwa huenda ningemsikia kwa utamu zaidi ama kusoma ule uchambuzi wake ambao daima nilikuwa nikiusikia wakati akitangaza lakini kwa bahati mbaya nilimsikia na kumwona mara mbili siku ya Zari white part pale Mlimani City akimhoji Mwana Fa na Millard Ayo ambaye kwa maneno yake niliona kabisa kumkubali Kidboy na huenda alikuwa mmoja wa watu walimvutia kwenye utangazaji.
Pia nilimsikia kwenye tunzo za watu , tangu hapo nimeishia kulisoma jina lake Bongo 5 akiweka taarifa huku kazi ya kuandika makala za kitafiti na kiuchambuzi zikibaki kuwa kazi ya Fredrick Bundala gwiji mwingine katika utangazaji na uandishi wa kazi za kiuchambuzi na kiutafiti ambaye walau nimekuwa nikimsikia kwenye Chill na Sky.
Leo wakati napitia kwenye ukurasa wa Fredrick Bundala nikakutana na taarifa iliyonivutia na kunifanya nifarijike haswaa!
Kidboy kuwa mkuu wa vipindi kwenye redio mpya LakefmMwanza nikajua zile zama za utangazaji safi zinarudi akiwa kama mwandishi na mtangazaji ule ubora katika tasnia hiyo unategemewa kurudi.
Si tuu katika utangazaji pia kwa upande wa muziki nayaona mabadiliko na maendeleo kwani sina shaka katika kuusema ukweli kuhusu muziki haijalishi mwanamuziki anapendwa ama ni mkubwa lakini anapokosea wimbo fulani ama kitu fulani kwenye wimbo lazima arekebishe mradi apewe nafasi ama aipate nafasi na isipopatikana alikuwa akiitafuta.
Kumbuka kipindi alipokataa kupiga copy za nyimbo za wanamuziki kama vile Kafara ya Tanzanite akiyekopi mbagala ya Diamond Platnumz.
Huyu ndiye Kidboy ninayemtaka najua ataleta mabadiliko na maendeleo katika tasnia ya burudani na habari kwa ujumla.

Naomba kuwasilisha....

0 comments:

Post a Comment