ads

Friday 8 April 2016

IKO WAPI ZOUK YA BONGOFLEVA?

Na.Steven Mwakyusa
Kuna kipindi katika Bongo flava, ilitokea muziki aina ya Zouk ulipata maarufu na kupendwa na tulio wengi!!
Kwa kifupi Zouk ni mziki mtamu, unasikilizika, unaeleweka na unabeba hisia za kutosha!
Wasanii wakubwa na wachanga walijitahidi kuimba aina hii ya muziki kadri walivyoweza!! Ukitaja manguri basi utaacha kumtaja Mr Paul na vibao vyake kama Zuwena na Harusi, Stara Thomas naye alisikika na vibao kama Mimi na wewe pia Wasiwasi wa mapenzi!!
K bazil pia alifanya vizuri na kibao chake cha Riziki alichoimba na Stara Thomas pia Bizman!! Pia Bizman ambaye alikuwa na mtayarishaji wa muziki katika studio za Soundcrafts hakubaki nyuma, vibao kama Ametoroshwa, nilishe nikulishe, pia Nipe muda vilikonga nyoyo za wengi, Banana Zorro ni mmoja pia ya wasanii waliyoiimba Zouk, huku vibao kama Wasiwasi, mapenzi gani vikimpa chart ya juu!!
Wanaoitwa underground pia walifurukuta kutaka kutoka na aina hii ya muziki, hapa tulimsikia Voice Wonder na Nimpende nani, Hama Q alisikika na Lady, Presssure ya Hafsa Kazinja pia ilimfanya ajulikane, Deo Mwanambilimbi pia hakubaki nyuma, yeye alisikika akiwa na Banana Zorro katika wimbo ulioitwa kwanini!!
Muda ulienda huu muziki ukapotea, na imebaki historia....kipi kiliupoteza hata mimi sijui!!

0 comments:

Post a Comment