ads

Friday 8 April 2016

ROMA USIHANGAIKIE 'TRACE' BADO TUNAKUHITAJI


Na.Moringe Jonasy
Nimekaa sebuleni nikipumzika baada ya shughuli za asubuhi ambazo zinanifanya nihitaji pumziko la nafsi na akili kwani tangu asubuhi nimeichosha sana akili kutokana na kazi ngumu ya kuandaa miswada mitatu ya mashairi,riwaya na tamthiliya ambazo ipo kwenye hatua za mwisho kabla ya kuchapwa.
Siku nyingine muda kama huu ningekuwa juu ya baiskeli nikizunguka huku na huko kukuza ujuzi wa mazingira na tamaduni kwa lengo la kukuza upeo wangu na kujaza maktaba ya kichwa.Leo nimeshindwa kwenda nilikopanga kwenda (KIA) Kutokana na mvua iliyonyesha hivyo nimeamua kukaa na kuanza kusikikiza muziki.
Naam Belle nine alishautaja umuhimu wa muziki akiuweka kama moja ya vitamin ambazo tunazihitaji nami sipuuzi ushauri wake naanza kusikiliza wimbo wake,unafuata wa Samir Nakuombea hapo najikuta nashindwa kusahau mikasa ya mapenzi niliyoshuhudia maishani mwangu baadaye nashindwa kusikiliza wimbo wa Christian Bella 'Nashindwa' kwani naye ananifanya niumie baada ya wimbo huo kugusia maisha yangu ya mahusiano na kuniumiza.
Nakutana na wimbo wa mwana ulioimbwa na Ally Kiba hapo nakumbuka mengi yanayoendela nchini unapoisha wimbo wa nusu nusu unasikika kwenye spika za redio yangu na kuniburudisha haswaa kisha sauti ya bonta inafuata akiimba wimbo wa kura yangu najikuta naurudishia zaidi ya mara tano kabla ya kuendelea ninapokutana wimbo wa ROMA mkatoliki Tanzania.
Hapo nasita kuendelea kusikiliza nyimbo nyingine naufanya huo wimbo uendelee kujirudia kusikika.
Napelekwa mbali kifikra baada ya kusikiliza nyimbo za mwanamuziki huyu ambaye si tuu anajua kuimba bali anajua nini cha kuimba, wakati gani na kwa watu gani.
Je, kuna siku wimbo wa ROMA utapigwa kwenye vituo vikubwa vya redio duniani ama hata Afrika?
Video zake zinaweza kushindania tunzo kubwa za kimataifa?
Nani anamsikiliza ROMA nje ya Tanzania ama Afrika mashariki?
Ni baadhi ya maswali machache yaliyonifanya niyatafutie majibu.
Kwenye suala ya kusikika kimataifa ni jambo gumu labda akianza kuongelea matatizo si tuu ya ndani ya nchi bali ajaribu kuyaongelea ya duniani kwote ama haya Afrika tuu kwani yanafanana kwa kiasi kikubwa, kama rushwa popote ipo, kama ukimwi na imani potofu zipo sehemu nyingi sana ,umasikini usiseme ,uvivu na ukoloni wa weusi wenzetu barani Afrika bado janga kubwa.
Je, kwa kufanya hivyo atasikilizwa Nigeria ama Ghana ambako tangu kizazi cha wapigania uhuru kipite hawajakisikia kiswahili hadi juzijuzi walipoanza kumsikiliza Diamond?
Diamond aliwezaje? Kuwashirikisha na kutoa video zenye ubora.
Je akifanya hayo atasikilizwa ama kutambulika kimataifa?
Hilo bado gumu sana kwani hata sisi hatuwasikilizi wanamuziki wa aina hiyo wanaoimba huko kwao zaidi ya kusikiliza muziki wa aina nyingine na si auimbao ROMA.
Baada ya kujiuliza mwaswali mengi najikuta nikihitimisha kuwa licha ya ROMA kuimba nyimbo zinazohitajika sana kwenye nchi za bara hili lakini bado ana kazi kubwa ya kufika huko akina shetta na Ommy Dimpoz wamefika hivyo namwomba asihangaikie kupigwa trace ama MTV bali aendelee kuhudumia jamii ya kitanzania ambayo naamini bado inahitaji sana elimu aitoayo.
''ROMA tafadhari usihadaike na mafanikio ya wengine binafsi bali endelea kuusaidia unma ufanikiwe"
Naomba kuwaasilisha
Niambie mtazamo wako#mwanakalamumwenzangu

0 comments:

Post a Comment