Saturday, 9 April 2016

YAJUE HAYA KUHUSU KILIMO CHA GREENHOUSE

Na.Steven Mwakyusa
Hiki ni kilimo ambacho kinamuwezesha mkulima kudhibiti mazingira yake kwa maana ya nishati ya jua, unyevu na upepo.
Wazo la kuzalisha mazao katika controlled environment lilikuwepo toka enzi za utawala wa Rumi na baadaye Green zilianza kuundwa na kufanya kazi karne ya 13 huko nchini Italia. Greenhouse imekuwa technolojia inayotumika katika nchi nyingi kuanzia Ulaya mpaka Asia, kumekuwa na project nyingi sana za Greenhouse na zimeonesha kuleta tija kubwa kwa wakulima.
Greenhouse inamuwezesha mkulima kulima mazao hasa ya matunda na mboga. Greenhouse inamuwezesha mkulima kulima katika kipindi chote cha mwaka pasipo kujali misimu.
Ikumbukwe kuwa unaweza kuzuia magonjwa pia wadudu ambao ni hatari kwa mazao. Hili limeonekana kuwa na tija jwa magonjwa na wadudu ni changamoto kubwa katika kilimo ukiachilia mbali mabadiliko yasiyotabirika ya hali ya hewa.
Kabla ya kuamua kujenga Greenhouse unatakiwa kufanya utafiti katika udongo(soil pH, structure, texture &profile) ili ujue kipi cha kuongeza ama kupunguza. Pia unatakiwa kuchunguza aina ya maji na chemikali zilizomo ndani yake.
Kwa Tanzania bado inaonekana ni technologia mpya ila imekuwepo kwa muda sasa. Ukubwa wa Greenhouse unategemea na mahitaji yako pia mtaji ulionao. Kwa mfano material ya kujenga greenhouse y enye ukubwa wa 8m*15m hayazidi 3million, kwa ukubwa huu unaweza kuzalisha mpaka tan 30 za nyanya kwa mwaka na pia Greenhouse ina Guarantee ya kukaa miaka 10.

1 comments: