ads

Saturday 9 April 2016

YAJUE HAYA KUHUSU UCHAFUZI WA MAZINGIRA

Na.Steven Mwakyusa
Uchafuzi wa mazingira umekuwa ukikua siku hadi siku kutokana na ongezeko la watu duniani likienda sambamba na kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu! Kuongezeka kwa uhitaji wa makazi, kukua kwa technolojia hasa uzalishaji katika viwanda, usafirishaji na kilimo vinatajwa kuwa sababu za kuongezeka kwa huu uchafuzi!
Uchafuzi wa mazingira umegawanywa kulingana na kitu kinachoathiriwa moja kwa moja, hapa tuna ardhi(land pollution), hewa(air pollution), maji (water pollution ) na kwengineko zinatajwa kelele(noise pollution)
Athari za uchafuzi wa mazingira zimekuwa kubwa, hasa kwa kusababisha magonjwa na kuua mimea pamoja na viumbe wa majini samaki wakiwemo. Joto limekuwa likiongezeka duniani (global warming ) na kusababisha mabadiliko makubwa ya hali ya hewa!!
‪#‎1 Mto‬ Ganges uliopo India unatajwa kuwa ndiyo mto uliothiriwa kwa kiasi kikubwa na "water pollution"
#2 Inakadiriwa kuwa watoto 1000 wanakufa kila siku nchini India kutokana na magonjwa yanatokana na uchafuzi wa maji.
#3 Kutokana na takwimu la Shirika la Afya Duniani (WHO), katika mji wa Mexico City watu 6400 wanakufa kila mwaka huku wengine zaidi ya 100,000 wakipata matatizo katika mfumo wa upumuaji kutokana na uchafuzi wa hewa(Air pollution)
#4 Kati ya mwaka 1956 na 1968 viwanda nchini Japani vilitupa madini ya Mercury moja kwa baharini, Mercury iliathiri samaki na baadaye mpaka walaji wa samaki na kupelekea watu wengi kuugua na wengine kufa!
#5 BMWs yanatajwa kuwa magari rafiki kwa mazingira huku Mitsubishi na Chyrister yakitajwa kuwa na uchafuzi zaidi wa mazingira. Ila kadri siku zinavyoenda ndivyo magari yanavyozidi kuboreshwa na kutoa moshi kidogo!!
#6 Inakadiriwa zaidi ya computer 130,000 zinatupwa kila siku wakati simu 100 million zinatupwa kila mwaka na kusababisha uchafuzi mkubwa.
#7 Viwanda nchini Marekani vinazalisha kemikali za sumu zinazofikia tani million 3 kila mwaka!

NB; Ukiliangalia suala la uchafuzi wa mazingira "locally" unaweza usione athari zake kwa haraka, ila kama utalitazama "globally", hatari iliyo mbeleni ni kubwa kuliko wengi tunavyifikiri. Japo kufuta kabisa huu uchafuzi ni jambo lisilowezekana, ni wajibu wa kila mmoja kujitahidi kulipunguza hili tatizo. Matumizi ya nishati mbadala kama gesi na solar badala ya mkaa na kuni yanasaidia kupunguza kiwango cha CO2 hewani, pia matumizi ya mboji badala ya mbolea za viwandani inasaidia hata pia kufanya "recycling" ya taka ngumu hasa za plastic!!

0 comments:

Post a Comment