ads

Sunday 15 May 2016

KUVUNJIKA KWA NDOA HIZI ZA WASANII MWANZO WA MAFANIKIO YAO


Na.Mwanakalamu
Wiki chache zilizopita taarifa ya Mo Music kuachana na menejimenti yake iliyomtoa baada ya kutomfanyia kile awalichokuwa wamekubaliana zilitoka na kuzua mijadalaa kadhaa miongoni mwa wadau wa muziki.Kuna wale waliokuwa wakikubaliana na uamuzi wake lakini kulikuwa na wale waliokuwa wakipingana na uamuzi wake huku hoja na tabiri mbalimbali juu yake na muziki wake zikitolewa.Mo Music si mtu wa kwanza kuachana na menejimenti iliyomtoa kuna wengi waliwahi kauchana na wale waliokuwa chachu ya kujulikana kwa kwenye muziki japokuwa kila mmoja alitoka kwa njia yake na maneno aliyoyajua.
Zifuatazo ni ndoa za wanamuziki zilizovunjika na kuleta neema kwa wanamuziki;-
Diamond Vs Sharobaro Records
Hii ilikuwa baada ya tukio la kulipuka kwa mabomu ya Gongo la Mboto, ambapo kwa mujibu ya maelezo yao kwenye vyombo vya habari kuwa Diamond alitaka kurekodi wimbo kwa ajili ya kuwapa pole waathirika lakini Bob Junior aligoma kwa sababu ambazo hadi leo zinachanganya kumbukumbu zetu.Kwani Diamond alidai Bob Junior alikataa kumrekoria wimbo huo huo bure akidai hadi alipwe pesa lakini Bob Junior naye akadai kuwa wakati anaombwa kurekodi wimbo huo alikuwa amepata matatizo yamasikio kuuma hivyo alimwomba Diamond awe na subira  akikanusha habari za kudai pesa kabla ya kazi kwani alikuwa ametayarisha albam ya kwanza ya Diamond bila malipo.
Huo ukawa mwanzo wa kutengana kwa Diamond na studio hiyo ambayo alikuwa ameizoa na akaenda kwa Maneck kurekodi wimbo wa Gongo la Mboto alioimba na Mrisho Mpoto.Baadaye akaenda kwa Lamar  akatengeneza moyo wangu ambapo waandishi na wadau wengi walizidi kumkosoa na kudai kuwa alikuwa amepotoka kwa uamzi huo na alikuwa akijizika mwenyewe.
Lakini tofauti na tabiri za wakosoaji wengi Diamond alianza kupanda ngazi hadi leo hii ukiwataja wanamuziki watano wa Afrika huwezi kumwacha Diamond na anastudio yake na Music lebel ya WCB.Lakini kitu cha kushukuru kwa sasa ni kwamba watu hawa wamemaliza tofauti zao na tunategemea kolabo kati ya Bob Junior na Diamond.

Tundaman Vs Spark
Hawa walikuwa maswaiba kweli na uimbaji wao ulikuwa umezoea masikio ya wadau wengi wa muziki.Walifanikiwa kutoa albamu ya pamoja iliyokuwa na ngoma nyingi kali ambapo wlaipata kuwashirikisha wakali kadhaa wa bongo fleva kama Madee na Chid Benz.Mafanikio ndiyo ynasemwa kuwa ilikuwa ni chanzo cha ugomvi wao huku kila mmoja akidai ndiye mtunzi wa wimbo uliobeba ushirikiano wao ‘’Nipe Ripoti’’ walimshirikiasha pia Madee.
Kutengeana kwao kukampoteza Spark ambapo wadau wengi wa muziki hatujui alinachokifanya mara baada ya kutoa wimbo wake wa ‘’Tangu nitoke jela’’ lakini Tundaman ni kama alikuwa amepata  Baraka baada ya kuvunjika kwa ushirikiano wao ambapo ameweza kudumu kwenye ‘game’ akitoa ‘hits’ kadhaa ambapo kwa sasa Mama kijacho bado inasumbua masikio ya wadau wengi wa muziki.

AY&FA Vs East Coast Team
East Coast team ni kati ya makundi makongwe ya muziki ambayo yaliwahi kuuteka muziki wa Tanzania yakiwajumuisha wakali kadhaa kama GK, AY , FA na wengine lakini ghafla AY NA FA wakajitoa kundini huku wadau wengi wa muziki tukiachwa vinywa wazi baada ya kutojua sababu ya watu hao kujitoa.
Wengi hawakuamini kama AY na FA wangeweza kusurvive wakiwa peke yao lakini tofauti na tabiri za wengi wakali hao wakajiundia umoja wao ambapo walifanikiwa kutoa nyimbo kadhaa ambazo zililikamata soko la muziki wa bongo.Walitoa pia Albam ya pamoja iliyokuwa ni moja ya albam bora za muziki wa Hip hop nchini.Miaka kadhaa baadaya ya kundi hilo kuachwa na wawili hao ni kama limekufa kwani  halisikiki tena kwa ngoma kali huku wakionekana kutoendana na mabadiliko katika muziki wa bongo.
Kwa hiyo tunaweza kusema kujitenga kwao na kundi hilo AY na Fa kulikuwa ni njia ya mafanikio yao.
Kasim Mganga Vs Tip Top
Kasim Mganga, tajiri wa Mahaba kutoka Manzabay kule kule kwa Mb Dog alifanikiwa kutoa hits kadhaa  akiwa chini ya Tip top.Alipojitoa Tip top wengi walitabiri kuwa ulikuwa ni mwanzo wa kupotea kwenye muziki ikizingatiwa kuwa Tip Top walikuwa kama wameukamata muziki wa bongo na wengi walikuwa wakitamani kuwa chini ya uongozi huo.
Lakini Kasim akaziba masikio na kuchukua njia yake na baada ya muda mfupi kasim aliendela kupanda ngazi huku ujuzi wake wa kulichezea koo likatoa sauti mwanana na akili yake ikitoa mashairi murua kuhusu mahaba  vikimfanya azidi kuwa kwenye ramani ya muziki Bongo.
Dogo Janja Vs Ustadh Juma
Wengi tulimfahamu Dogo janja baada ya kufika Tip top huku Madee akiwa moja ya sababu ya kufika hapo ambapo kupitia kipaji chake akajikuta akisomeshwa na Madee.Baada ya miezi kadhaa ya umaarufu Dogo Janja akaonesha ujanja wake na kudai alikuwa akinyonywa na Madee na uongozi wa Tip Top ukila zaidi jasho lake zaidi ya alivyokuwa alilila mwenyewe , aaacha shule na kufanya mahojiano na vyombo vingi vya habari akitoa shutuma nyingi kwa Madee na uongozi mzima wa Tip top.Miezi michache baadaye Dogo Janja alizidi kuonesha ujannja wake kwani alipokelewa kwa mbwembwe uwanja wa Ndege akiingia kwenye menejimenti mpya alikwa Ustadh Juma almabye aliamua kumchukua.Chini ya menejimenti hiyo Dogo Janja akatoa jiwe kali la ‘’Ya moyoni’’ ambamo alimshirikisha PNC.KATIKA ‘Ya MOYONI’ Dogo janja aliyatoa kweli ya moyoni huku zile shutuma ambazo wengi tuliamini  penmgine zilitoka kwa bahati mbaya  zikisikika kwenye wimbo na kumfanya wengi kumhurumia  kwa mteso aliyokuwa akiyapata chini ya Tip Top.Akaja na nyimbo nyingine kadhaa ambazo hazikueleweka miongi mwa wadau wa muziki hadi pale tuliposikia karudi tena Tip top akiomba msamaha na kuachia wimbo wa my life ambao bado unafanya vizuri na umemrudisha kwenye chati ya wanamuziki wenye matamasha.
Kurudi Tip Top na kuachana na Ustadh Juma ni kama kumemfungulia njia kwani leo hii unapomzungumzia Dogo Janja unamzungumzia mmoja wa wanamuziki wenye magari yao.

Naomba kuwasilisha; Niambie ni ndoa gani nyingine kwenye muziki ilivunjika na kuleta neema kwa mwanamuziki, niandikie hapa chini.

0 comments:

Post a Comment