Thursday, 5 June 2014

MUNGU GANI MTESAJIKila siku twasikia, kuna watu wameua,
Wengine wajisifia, shule wakizivamia,
Binafsi ninaumia, pia ninawachukia,
Mungu gani atesaye, mie hapo nina shaka.

Pande za Naijeria, boko wanajinafasi,
Mataifa kwingilia, washajiita mabosi,
Wale watu wanalia, na kujiona na mikosi,
Mungu gani atesaye, mie hapo nina shaka.

Walianza makanisa, sasa wameenda shule,
Watu kweli wametesa, mie ninawapa pole,
Nini sasa wamekosa, jamani mabinti wale,
Mungu gani atesaye, mie hapo nina shaka.

Wajiita waslamu, jamani hawaogopi,
Kweli umwagaji damu, wapi wao wamekopi,
Nipeni hiyo elimu, kaka kweli hawongopi,
Mungu gani atesaye, mimi hapo nina shaka.

Poleni ninyi mabinti, mungu awape imani,
Mlipo mlipige goti, mkaomba kwa imani,
Hao hawataki noti, bali kuvunja imani,
Mungu gani atesaye, mimi hapo nina shaka.

Dini zote zinapinga, mambo hayo kutokea,
Husein utaniunga, kama sitowakosea,
Pia nitoe ujinga, siyo kwa kunizomea,
Mungu gani atesaye, mimi hapo nina shaka.
Mshindwe boko haramu, mfanyayo tumechoka,
Nawapinga kwa kalamu,.......

0 comments:

Post a Comment