Masaa machache kabla ya mechi ya simba dhidi ya mtibwa nilijaribu kupanga
kikosi ambacho nahisi kingecheza nilianza na Ivo Mapunda golini
pembeni Mohammed Hussein na Nassoro Said 'Chollo' kati nawaweka Isihakah na Mganda Juuko Musheed mbele yao yupo Jonas mkude.
Nilipofika hapa nikaanza
kumkumbuka kijana mmoja ambaye kama angekuwa Tanzania katika soka basi
wangemwita mzee ama babu kwa umri wake
wa miaka thelathini na mbili.Leo ni Mara ya pili ndani ya wiki moja
namkumbuka huyo kijana siku ya kwanza nilimkumbuka pale Okwi aliposifiwa
kwa kufunga goli zuri dhidi ya Yanga.Huyu si mwingine bali ni marehemu
Patrick Mutesa mafisango ambaye mei kumi na saba mwaka(leo) huku atakuwa
ametimiza miaka mitatu tangu atangulie mbele ya haki.
Kijana huyu
alikuwa akiwapa taabu kuanzia washambuliaji,viungo ,mabeki na hata
makipa wa timu pinzani kwa uwezo wake wa kukaba,kumiliki mpira kutoa
Pasi za magoli na hata kufunga magoli hadi anapoteza maisha nakumbuka
alikuwa akiwaongoza viungo wenzake kwa ufungaji wa magoli kwani alikiwa
ameshatikisa nyavu Mara kumi na mbili na kutoka pasi kadhaa za
magoli.Alikuwa mchezaji kweli ambaye simba hawakujuta kumchukua kutoka
Azam kwani alifanya zaidi ya kazi aliyokuwa amepangiwa.
Huyo ndiye alikuwa chachu ya mafanikio ya okwi katika ufungaji na ushindi wa simba kwa ujumla .
Unakumbuka ile mechi ya shandy hapa nyumbani? Unalikumbuka lile goli?
Nani kati ya viungo wa simba angefunga?
Mi sijui labda Mkude ambaye yupo vizuri sana katika kumiliki mpira lakini Mafisango alikuwa akizifanya kazi zote isipokuwa kudaka mpira kwa mikono
na uamuzi.
Alikuwa akiifanya simba kucheza soka la kujiamini
tofauti na leo watakavyoingia uwanjani kwani hawana mtu kama
mafisango.Ningetamani itokee mafisango angekuja kucheza na mtu kama
mkude ili awe huru kwenda mbele na kumpasia okwi ama maguli wafunge
magoli mengi ambayo yangepunguzabkujiamini kwa viungo na mabeki wa timu
pinzani lakini basi hayupo tena .Na hata angekuwepo pengine angekuwa kwa
mkopo huko coast union ama polisi morogoro kwa madai ya uzee ama
angekuwa ameachwa na simba katikati ya msimu kwa madai ya kushuka
kiwango ili kujaza waganda ambao watu wachache wanaamini kuwa watamfanya
okwi ajisikie yupo nyumbani.
Lakini pengine angechukuliwa na yanga
baada ya kukosa ile penati kule Sudan na kubebeshwa lawama za kucheza
chini ya kiwango lakini hayupo ametangulia tuendako.
ULALE PEMA PATRIC MUTESA PETIT MAFISANGO
RIP our legend
ReplyDelete