Sunday, 17 May 2015

NINAPOJIVUNIA KUISHI ZAMA HIZI TANZANIA.


Nisiwe mnafiki najivunia kuishi katika zama hizi.Zama ambazo licha ya taifa stars kufanya vibaya katika karibu kila mashindano nimefanikiwa kuwaona Mbwana samata ,Tom Ulimwengu, Juma Kaseja, Nadir Haroub,Juma Nyoso,Mrisho Ngasa,Jerry Tegete,Kigi Makasi na wengine wengi ambao kila nikiwatazama najikuta najivunia kuwa mtanzania wa zama hizi.
huku nikikinzana na mitazamo ya kuwa soka letu linashuka.


Najivunia kuishi zama za akina Mwigulu nchemba,Zitto Kabwe,Kafulila, John Myika ,Anna Makinda na wengine wengi kama Lissu.Zama za siasa za wazi huku unafiki wa zama zote ukiumbuliwa na uwazi wa vyombo vya habari ama wa kwa masudi au kwa kutokujua laini nimefanikiwa kuishi zama hizi za UKAWA , KUVUANA MAGAMBA na parakatumba zote kwenye siasa.Zama za kuwa na wanasiasa machachari bila kujali umri wala jinsi zao kama akina Halima Mdee, Esta bulaya,Anne Kilango Malechela,na Marehemu Amina Chifupa nisijivunie tuu kuishi katika zama zao jamani? Hapana lazima nijivunie na nitajivunia daima.
Nani hajawahi kufurahia zama za shule za kata na chuo Kikuu karibu kila mkoa?, kama haufurahiii basi hunitakii mema motto wa mkulima wa mtama ambaye kwa malezi niliyopitia kufanikiwa kwenda Mzumbe,Tosamaganga,Zanaki na kwingineko ni ndoto ya mchana weupe huu nikitembea juani nikisaka maji ya kupikia kwa takribani saa la tatu nzima lakini kila bonde linaonekana kukosa uhahi wa miaka yote.
Zama za bima ya afya,zama za barabara za rami hadi nyumbani kwangu Ludewa nikimweleza mdogo wangu lami iivyo sipati tabu kumweeza tofauti na alivyopata taabu baba yangu mdogo aliyekuwa akinisimulia juu filamu za ng’ambo atajapo barabara nzuri akilini nikifikiria njia yetu ilitengenezwayo kwa muda ama kwa kuandaa kumpokea Mwanasiasa mmoja akiwa na huyu wamwitaye mwekezaji wakija kuangalia maeneo ambayo wanapanga kuweka mgodi mkubwa wa makaa ya mawe , na madini mengine yanayobebwa kwa tani eti kwenda kufanyia utafiti Ulaya.
Kwa nini nisijivunie kuwa na Mbunge ambaye hata unaibu waziri kivuli hajapta lakini kila sehemu Tanzania hii wanjivuni kuwa na mtu kama yeye?.Au niendelee kumuuliza Mrema kilichompata Kolimba?.Najivunia kwani leo hii hata naweza kutumwa na baba yangu benki nikalipie pembejeo zakilimo ama kutumwa na mama yangu mwalimu wa mwandiko darasa la kwanza na la pili tangu nikiwa na miaka miwili kwenda kumchukulia kalaki kake akamlipe Muuza TV aliyemkopesha ili nasi tuendane na wakat,i nani anataka kuikosa The Komedi?.
Najivunia kuwa na uchaguzi wa kuchagua redio ipi ya kuisikiliza badala ya kusubiri usiku nisikilize RTD ama nimalize Betri zangu kwa kusikiliza Redio za Malawi ambazo hauna ninachokielewa zaidi ya MLIBWANJI ? Leo hii hata wilayani wangu kuna redio inayoweza kutangaza bei mpya ya panadol , ama bei ya maparachichi ya mzee Magoha tofauti na zama za kusubiri saa saba ama kumi kusikiliza kama kweli mtoto wa Mzee Kasuku alikuwa amefariki kweli kwenye matangazo ya vifo.
Kweli najivunia hizi zama ambazo kupitia mimi mama yangu anaweza kufungua laptop na kuweka CD ya Rose Mhando kusikiliza Yesu Nibebe.Ama kwenda kwa ndugu yake Kajole kutoa hela aliyotumiwa na mwanaye aliyeolewa huko Mbinga lazima nijivunie bwana hizi zama nzuri.
Lakini lazima nijivunie kuzaliwa zama za akina Diamond Platnumz ambao leo hii hamwombi mtu kufanya Kollabo bali yeye huombwa kufanya hivyo, mwangalie kwenye picha hapo chini hivi uliwahi kufikiria jambo hili miaka kumi iliyopita? Kama ulifikiria we sasa utakuwa Pweza ama Shekh Yahaya tena ulifikiria ndani ya ndoto ya kutisha ambayo daima hukupenda kuikumbuka.
Ulifikiria kuwa utafika muda Kuna mtanzania atachukua mamilion kwenye BBA? Ama kuna mwanadada atakuja kuchukua tunzo kubwa za muziki hapa Afrika am duniani kwa ujumla? Mie nimewaona hawa watu Vannesa na Jide. Hadi hapo nisijivunie? Kwa nini au huoni raha kusikia kuna watu wa kutoka Tanzania hii hii wanaimba nyimbo na wamarekani ambao watu kutoka nchini humo wanawaona kama Miungu watu unabisha?au humjui R Kelly ama Kingstone?
Nisijivunie zama za yamoto bendi ama THT nikijiaminisha kuwa muziki huo wanauweza wakongomani pekee ama nitafute tape ya Msondo Ngoma niliyoiharibu nikitaka nyuzi za kufukuzia ndege wala mpunga shambani.
Zama za kusoma hadithi kwenye simu yako huku waandishi mahiri wa zama hizi kama

0 comments:

Post a Comment