Na Moringe Jonasy
Hii ni mara ya tatu naandika juu Alikiba , hii inatokana na hali
iliyopo hapa nchini kwa wapenzi wa bongofleva hadi wasiokuwa wapenzi
kwani limekuwa jambo lililozungumziwa sana nchini kuliko hata suala la
kuuawa kwa mlipuaji mabomu huko Arusha.
Japokuwa sikuwa Leaders ile jumamosi ,nilibahatika kuiona ile show online na kung'amua vitu vichache ambavyo vilimfanya alikiba ashangiliwe sana.Mambo matano yafuatayo yanaweza kuwa sababu ya Alikiba kushangiliwa...
1.SAUTI YAKE
Kwa bahati nilikuwa miongoni mwa watu tuliofanmikiwa kumsikia Alikiba
kabla ya Njiwa na Cindelela ambazo zilimweka kwenye ramani ya bongofleva
kwenye wimbo mmoja ambao alikuwa ameimba na wasanii wenzake lakini
sauti yake ilinifanya niupende ule wimbo waliouita Leila.
Kuna mtu
mmoja aliniambia alikiba anabana pua nami nilimpa jibu rahisi tuu kuwa
KAMA ANABANA PUA BASI ANABANA VIZURI. Lakini alikiba alithibitisha kuwa
alikuwa akibana pua kabla hajaenda kuimba na R Kell ambapo alifunzwa
jinsi ya kuimba vizuri huku matumizi makubwa ya koo , pua na ala
nyingine za sauti na matokeo yake tuliyaona kwenye nyimbo zake kama
Mapenzi,feal free ,Dushelee,my Everything na Mwana dsm ambazo zinazidi
kutuonesha tofauti kati ya wasanii wa Marekeni na wa Bongo.
Hii
haikumpa shida kuimba kwa sauti yake yenye ubora pale jukwaani na
kuendelea kuibua shangwe kutoka kwa mashabiki wake wengine waliopo
kwenye hili kundi la kutumia vyema sauti zao ni pamoja naMarlow ,Rama D
na Diamond.
2.MWANA NI HABARI YA MJINI
Hili halina ubishi
kuwa mwana ni miongoni mwa hit song kwa kipindi hiki , wimbo una sifa
zote ujumbe, sauti na pia unachezeka.Ningeshangaa kama Alikiba
angeshangiliwa kama angekuwa na my everthing kama silaha yake wakati
alishatutibua wafuasi wake kwa kutotoa video. Kama ilivyo Mdogo mdogo
,Pacha wangu,Najiona Mimi na nyingine nyingi zinazotikisa jiji.
3.ALIVYOTINGA STEJINI
Alingia kwa mbwembe huku akiwaambia wafuasi wakiwa na hamu ya kuona
kitu ambacho angekifanya baada ya kukaa kimya kwa muda wa takribani
mwaka mmoja.Kama angekuwa hajarudi kweli nilitegemea kuwa angezomewa
lakini kwa kuwa alikuwa amerudi kweli Shangwe ilikuwa haki yake.
4.HURUMA YA MASHABIKI
Mashabiki wamemhurumia Alikiba baada ya muda wa malezi na kumpa nafasi
mdogo wake huku akijifanyia kautafiti juu ya mziki wetu akiwa nje ya hii
tasinia.
Vimaneno vilivyozungumzwa wee na watu juu yake viliwafanya
wafuasi wake wampe moyo na kumwambia kuwa anaweza na wapo pamoja naye.
5.KUMPA DENI
Kilichofanywa na mashabiki pale Leaders alikiba asikione kama ni
ushujaa ama ushindi wa vita ambayo alikuwa ameshinda bila kuwepo kwa
hiyo vita bali atambue mashabiki wamempa deni ambalo aanze kulilipa kwa
kutoa video ya mwana Dsm yenye ubora,collabo la maana na wakali wa
muziki Duniani lakini mwisho waje kumpigia kura si kwenye Kill bali
kwenye kora,MTV,Chanel O , BET na nyingine nyingi.
NAOMBA KUWASILISHA NI MTAZAMO WANGU HUU
0 comments:
Post a Comment