ads

Sunday 17 May 2015

ENOCK BWIGANE ALIKUWA AKIMWITA PETIT





Masaa machache kabla ya mechi ya simba dhidi ya mtibwa nilijaribu kupanga kikosi ambacho nahisi kingecheza  nilianza na Ivo Mapunda golini pembeni Mohammed Hussein na Nassoro Said 'Chollo' kati nawaweka Isihakah na Mganda Juuko Musheed mbele yao yupo Jonas mkude.

Nilipofika hapa nikaanza kumkumbuka kijana mmoja ambaye kama angekuwa Tanzania katika soka basi wangemwita mzee ama babu kwa umri wake wa miaka thelathini na mbili.Leo ni Mara ya pili ndani ya wiki moja namkumbuka huyo kijana siku ya kwanza nilimkumbuka pale Okwi aliposifiwa kwa kufunga goli zuri dhidi ya Yanga.Huyu si mwingine bali ni marehemu Patrick Mutesa mafisango ambaye mei kumi na saba mwaka(leo) huku atakuwa ametimiza miaka mitatu tangu atangulie mbele ya haki.
Kijana huyu alikuwa akiwapa taabu kuanzia washambuliaji,viungo ,mabeki na hata makipa wa timu pinzani kwa uwezo wake wa kukaba,kumiliki mpira kutoa Pasi za magoli na hata kufunga magoli hadi anapoteza maisha nakumbuka alikuwa akiwaongoza viungo wenzake kwa ufungaji wa magoli kwani alikiwa ameshatikisa nyavu Mara kumi na mbili na kutoka pasi kadhaa za magoli.Alikuwa mchezaji kweli ambaye simba hawakujuta kumchukua kutoka Azam kwani alifanya zaidi ya kazi aliyokuwa amepangiwa.
Huyo ndiye alikuwa chachu ya mafanikio ya okwi katika ufungaji na ushindi wa simba kwa ujumla .
Unakumbuka ile mechi ya shandy hapa nyumbani? Unalikumbuka lile goli?
Nani kati ya viungo wa simba angefunga?
Mi sijui labda Mkude ambaye yupo vizuri sana katika kumiliki mpira lakini Mafisango alikuwa akizifanya kazi zote isipokuwa kudaka mpira kwa mikono na uamuzi.
Alikuwa akiifanya simba kucheza soka la kujiamini tofauti na leo watakavyoingia uwanjani kwani hawana mtu kama mafisango.Ningetamani itokee mafisango angekuja kucheza na mtu kama mkude ili awe huru kwenda mbele na kumpasia okwi ama maguli wafunge magoli mengi ambayo yangepunguzabkujiamini kwa viungo na mabeki wa timu pinzani lakini basi hayupo tena .Na hata angekuwepo pengine angekuwa kwa mkopo huko coast union ama polisi morogoro kwa madai ya uzee ama angekuwa ameachwa na simba katikati ya msimu kwa madai ya kushuka kiwango ili kujaza waganda ambao watu wachache wanaamini kuwa watamfanya okwi ajisikie yupo nyumbani.
Lakini pengine angechukuliwa na yanga baada ya kukosa ile penati kule Sudan na kubebeshwa lawama za kucheza chini ya kiwango lakini hayupo ametangulia tuendako.
ULALE PEMA PATRIC MUTESA PETIT MAFISANGO

1 comments: