Monday, 18 May 2015

MUNGU IBARIKI AFRIKA

Na.Moringe Jonasy.
Vuta picha mmekaa mahali mkicheka na kufanya mambo mengine mkiwa na uhakika wa siku inayofuata bila shaka yoyote kwani hakuna aumwaye kiasi cha kuyafikiria mauti ,hakuna anayesafiri kusema kuna ajari wala nchi haina vita kusema kuna watu watkuja kuwaangamiza kwa risasi na mabomu.
Kila mmoja anapanga namna atavyotumia siku chache za mapumziko ya pasaka wengine wanapanga kufanya sherehe ya kuzaliwa siku inayofuata na mengibe mengi ya neema.
Lakini dakika chache zifuatazo hali inabadilika kabisa unajikuta upo chini ya uangalizi mkali wa watu wenye silaha wakiwa hawana kitu wanachokihitaji zaidi ya uhai wako.Wenzako wanauawa kwa kupigwa risasi huku damu zikimwagika ovyo ovyo kana kwamba maji yanamwagwa kwa ajili y kufanya usafi ndani ya mahali ulipokaa.
Zamu yako ya kutobolewa fuvu la kichwa kwa risasi inafika mwili unakufa ganzi haraka haraka unajaribu kumwomba Mungu akusamehe dhambi zako kwa maana hakuna nafasi ya kutokea miujiza ya kuokolewa sara nazo haziishi unawakumbuka wadeni wako unawakumbuka wazazi zako jinsi walivyokuwa na mategemeo makubwa juu yako.
Unamkumbuka mpenzi wako ,unawakumbuka wanao lakini ghafla maumivu yanakatisha mawazo yako yaliyodumu kichwani mwako kwa sekunde zisizozidi mbili na kuupelekea mwili wako kuachana na roho yako kwa maumivu makali.... Aghhhh sitaki kufikiri.
Waafrika wenzetu wa Kenya jana wamekutana na hali hiyo ambayo ni kama hekaya za kuwa juu ya mti ulioko pembezoni mwa mto huko juu kuna joka kubwa nchi kavu kuna simba na mtoni mamba katega domo lake akudake na tawi ulolishikilia limeoza na linasekunde kadhaa kujiachia kutoka kwenye mti.
Haikuwa hekaya wala filamu moja ya kutisha bali tukio fulani la kutisha kuona ,kusikia ma kukutoke ambalo lilichukua maisha ya mamia ya tumaini la jamii mbali mbali za Kenya na nchi jirani wataalamu na wanaoelekea kuwa wataalamu zaidi ya miamoja waja wanaenda kufukiwa mara moja inauma.
Lakini mbaya zaidi wataalamu hao wanauawa na binadamu wenzao waliozaliwa na wanawake kama tulivyozaliwa wengine ,sijui wananini maana hata simba anaweza akawa na huruma watu mia?
Nakumbuka wakati nasikia kuwa kuna shambulio nilikuwa nikiandika hadithi fulani hivi nikiwa katika kutafuta taarifa mbambali juu ya geografia ya Afrika nikakutana na habari hiyo kama Breaking news kabla ya kuanza kupokea taarifa za ukweli na zilizotiwa chumvi kupitia whatsap ,facebook na instagram na kupoteza kabisa hamu ya kuandika huku nikiwachukia wauaji hao.Lakini kitu kingine kilichonichefua ni pale niliposikia kuna watu waliachiwa huru wengine wakiuawa kwa misingi ya dini, niliona wauaji wale waliamua kupoteza kizazi kile kwa kuwaharibu kiakili/kisaikolojia waliobaki hai kwani waliwaachia majeraha makubwa akilini kwa kuuliwa jamaa zao ambao waliishi nao kwa amani kwa kipindi chote kabla ya tukio hilo baya.
Lakini si hivyo tuu ndugu na jamaa wa waliouliwa wataanza kuwahusisha walioachiwa na mipango ya kufanyika suala hilo lakini masikini wa Mungu huenda wamepoteza hata ndugu zao wa damu na marafiki hata wafadhili wao kwani siku hizi familia kuwa na watu wa imanintofauti ni suala la kawaida kwani kama ilovyo kwa viumbe wengine binadamu ni "Social being" hivyo maingiliano ya dini, kabila ,taifa na tamaduni ni suala lisilozuilika.
Kuna walioanza kuilamu serikali ya Kenya kwa kutouimarisha ulinzi huenda wanastahili ila mie lawama zangu ni kwa wale wauaji ambao wanafurahia kuwaua wenzao wakihusisha matendo yao na dini safi ambayo siamini na sitaamini kama inawatuma wao kufanya unyama kama huo.
Wengine wakaanza kuzitahadharisha nchi jirani ikiwemo Tanzani na kukumbusha juu ya matishio ya kuvamiwa Dar es saalam na Mwanza lakini wengine wakaanza kujisifu kwa uimara wa majeshi yetu kwa kuamininkuwa tupo kwenye mikono salama bila kujiuliza ni kwa namna gani wanashiriki kulinda usalama wa nchi yetu.Haonhao wanafurahia askari kupigwa ama kudhalilishwa kwa namna yoyote ile kisa tuu wanaamini wapo kwa ajili ya chama tawala,hao hao wanawasaidia wahaniaji haramu kuingia na kuishi nchini na kuwaficha ili wasijulikana na vyombo vya usalama bila kujua wanatengeneza mazingira ya kushambuliwa na kwa bahati mbaya wale wauaji wakija kushambulia hawatokuhurumia kusema eti uliwahifadhi , ni hatari sana.
Mwisho niwape pole woye walioguswa na tukio la Garisa na mengineyo kama la westgate,kampala na mengine kwani naamini tukio hili limekumbusha machungu ya mashambulio yaliyopita na kutonesha vidonda vilivyokuwa vikielekea kupoa.
Mungu Ibariki Afrika

0 comments:

Post a Comment