Monday, 18 May 2015

UNAFIKI WA WAANDISHI KATIKA HIKI MNACHOKIITA BIFU


Na.Moringe Jonasy
Habari zenu ndugu wana Afrika ya mashariki, natumaini mu wazima wa afya poleni kwa wagonjwa na ndugu waliopoteza maisha kwenye matukio ya ajali zinazoendelea kutumaliza kila uchwao.Pia niwape pole ndugu zetu ambao usalama wao upo katika mashaka huko Afrika ya kusini kutokana na vurugu zinazoendelea.
Leo naomba nikiandike kwa mara nyingine hiki kinachoitwa bifu kati ya wasanii mbali mbali hapa nchini.
Na bifu ambayo wanapenda kuizungumzia ni kati ya Ally Saleh Kiba na Naseeb Abdul ambayo licha kwa nyakati tofauti kukiri na kukanusha kuwa ipo bado waandishi wa habari wenye taaluma ya habari ama wenye nafasi ama uwezo wa kuandika na walichokiandika kikasomwa na watu waliowatarajia.
Kwa upande wa Ally kupitia mahojiano mbalimbali kam mkasi na spora show aliwahi kukiri bila kupepesa macho kuwa hana maelewano na Naseeb na sababu kubwa ikiwa ni kufutwa kwenye wimbo alishirikishwa na kisha kutuhumiwa kumfuta Naseeb kwenye wimbo wake na mashahidi ni maproducier wa hizo nyimbo.
Lakini kwa upande wa Naseeb kupitia spora show alileta habari nyingine kabisa kama kumwomba Ally waimbe wimbo wa Single boy na Ally alikataa kwa kudai kuwa Naseeb alitaka mtelemko( jina kupitia Ally) kitu ambacho alikipinga kwa kuwa alikuwa ashafahamika na alikuwa ni msanii mkubwa.
Lakini licha ya tuhuma na mambo hayo yakiwemo habari za Naseeb kudai Ally ''amefulia kimuziki na kimaisha'' na Amekopa hela ili amalizie nyumba yake zilipambwa na hao tunaowaita waandishi hadi baadhi ya wasanii wakimshutumu Naseeb bila kujua nini athari zake kwa wasanio hawa wawili wenye vipaji vya hali ya juu.
Mwisho wa siku wasanii hao wameonekana kutopikika chungu kimoja na kusababisha mashabiki kuwa na upinzani mkubwa kwa sababu ya wasanii hawa.Wapo wanaojiita team kiba huku kazi yao kubwa ni kumsapoti Ally na kumponda Naseeb na team Diamond ambao lao ni kinyume na team nyingine.
Siwalaumu hata kidogo hao wana team zaidi ya kuwalaumu wanahabari ambao wanaona pa kumalizia tatizo hili na kuujuza umma ili ujue wapi tatizo na uamue nini cha kufanya badala ya sahizi watu wamejikuta mashabiki wa Naseeb kutokana na kitu fulani ambacho wanahisi Ally kamkosea mwenzake na kinyume chake.
Suluhisho ni hao waandishi kuwafuata KGT na Maneck waliotengeneza lala salama na single boy na kujua kama habari zinazozungumzwa kama zina ukweli badala ya kuendelea kuwafanya watanzania MAMBULULA kwa kuzungua chanzo kama vile wanakuna jipu lililoiva kwa kukwepa kulipasua ambayo ndiyo tiba yenyewe.
Na wasanii hao bila hiyana sijui kwa kuwaogopa waandishi kuwaandika vibaya waishia kuwalaumu watanzania eti WANAWAGOMBANISHA bila kujua hao waandishi ndio wagombanishi wakubwa.
Mwisho niseme tuu kwa nini nimeamua kutumia ALLY na NASEEB badala ya Alikiba na Diamond kwa sababu moja kubwa ; Nawaomba wasanii hao wajaribu kujiona kama watu wengine wa kawaida yaani ALLY na NASEEB kisha waone kama wapo sahihi kufanya wakifanyacho badala ya kujiona Alikiba na Diamond majina ambayo nahisi yanawapa upofu na kujiona hawaishi kwenye hii dunia tunayoishi wengine.
NIWATAKIE KAZI NJEMA WASANII WOTE MUZIKI WENU TUNAUPENDA KULIKO POROJO ZENU...
Naomba kuwasilisha.
Moringe Jonasy
17/04/2015

0 comments:

Post a Comment