ads

Tuesday 2 June 2015

UNATAKA KUANZISHA MIRADI HII? SOMA HAPA

Na.Steven Mwakyusa
Watu wengi wamekuwa wakitamani kufanya biashara pasipo kujua wapi wanataka kufika! Matokeo ya hili ni biashara kutokua (kudumaa) na baadaye kufa. Watu wa aina hii ndiyo mara nyingi hukumbwa na imani za kwamba ili ufanikiwe basi ni lazima uroge!!
Mtu wa aina hiyo utasikia leo anafuga kuku. kesho kaishaacha kuku ana miliki Tax, kesho kutwa kaachana na Tax anamiliki kibanda cha M- pesa, mara kaacha kibanda cha M-PESA sas ananunua viazi kutoka Iringa na kupeleka Dar. Sasa hapa ndipo tatizo huwa linaanzia, kabla ya kulalamika kuwa biashara ni ngumu kuna maswali ya kujiuliza,
Je umejipa muda gani katika biashara husika? Je unalenga kufika wapi?
Mfano
1. Kuuza Mitumba- Hapa hakikisha unataka kuwa wapi
siku moja? Je kuuza mitumba Dunia nzima?
2. Ukianza Biashara ya Mgahawa jiulize unataka
kuwa wapi siku moja? Je unataka kuwa na migahwa
East and Central Africa?
3. Samaki- Je unataka kufika wapi na hao samaki?
4. Salon- Je unata kufika wapi na saluni?
5. Tax- Je lengo lako ni nini? Je ni siku moja kuwa na
kampuni kubwa ya Tax Africa?
6. Kufuga kuku- Je unataka kuwa na nini katika hii
biashara ya kuku?
7. Kufuga ngo'ombe- Je unataka kuwa wapi siku moja
na ufugaji ngo'ombe?
Katika jambo lolote ni vyema kujipa muda (watafiti wanasema angalau miaka 10) ili mafanikio yaonekane! Kuendelea kufanya biashara kimazoea na baada ya kusikia tu biashara fulani inalipa hakuwezi kutufikisha kokote!!

1 comments:

  1. asante nimejifunza kitu kufanya utafiti ni bora, ili kutimiza malengo

    ReplyDelete