ads

Wednesday, 22 July 2015

ROSE MUHANDO NI UTELEZI TUU HUO INUKA UENDELEE NA SAFARI


Na. Moringe Jonasy Mhagama
 
Haleluya naitazamia mbingu mpya na nchi mpya
Huko nitapumzika milele
Taabu zangu zikiisha, nitamwona Bwana wangu
Akinikaribisha kule, karibu upumzike

Hapa ndipo nyumbani kwako, hapa ndipo mahali pako

Hapa ndipo makao yako, karibu upumzike

Haleluya nitaketi kwa furaha, nitapumzika kwa mungu, nitapumzika
Nitavikwa mavazi meupe, nitavikwa taji ya ushindi
 Taabu zote na mateso yote, hakika vitakoma
Nitaungana na malaika, maserafi na makerubi

Tukiimba nyimbo za ushindi, haleluya usifiwe

Naona mbingu zimefunguka, na Yesu yu mkono wa kuume
Akinitazama kwa upole, kwa macho yenye huruma
Tatazama vidonda vyangu, tatazama makovu yangu
Niloumizwa duniani, na watu wa ulimwengu
Tachukua kitambaa, atanifuta machozi
Akisema pole mwanangu, Yesu tanikumbatia
Bado kitambo kidogo, nitapumzika
Yesu atanipeleka, kwenye kijito cha uhai
Huko taniosha mwili wangu, nitapewa mwili mpya

Nami nitaimba hosana, hosana ndiye mbarikiwa

Nitaruka kama ndama, milele hata milele
Tavumilia, kwa ajili yako Baba
Yatosha walivyokuonea, Yatosha walivyokudhulumu
Yatosha walivyokupiga, karibu upumzike
Yatosha walivyokuudhi, Yatosha walivyokutukana
Yatosha walivyokuzomea, karibu upumzike
Haleluya, mateso yangu yakiisha nitauona uso wa Mungu
Nitamwona Yesu niliyepigwa kwa ajili yake

Yatosha walivyokuonea, Yatosha walivyokudhulumu
Yatosha walivyokupiga, karibu upumzike
Yatosha walivyokuudhi, Yatosha walivyokutukana
Yatosha walivyokuzomea, karibu upumzike

Yesu atanipeleka, kwenye kijito cha uhai
Huko taniosha mwili wangu, nitapewa mwili mpya

Baada ya taabu, ni furaha........
Sauti ya mwadada Rose Muhando kwenye wimbo wa Tabu zangu alioshirikiana na Anastazia Mukabwa  iliniamsha kutoka usingizini na kunifanya nigande kimawazo.Japokuwa ilikuwa ni sauti ambayo niliyokuwa nikiisikia kila saa kumi na mbili na nusu ili niamke na kumshukuru na kumwomba Mungu kabla ya kuamka na kuendelea na ratiba nyingine leo hii nilikuwa nimeenda mbali sana kimawazo.
Niliguswa sana na huu wimbo na kujikuta nikishindwa kufikiri kitu kingine zaidi ya maneno niliyokuwa nikiyasikia kutoka kwenye spika za simu yangu yalikuwa ni maneno yaliyonigusa sana.
Taratibu nikaamka na kuanza kumjadili kichwani mwanamama Rose Muhando nikakumbuka niliyokuwa nikiyasoma mitandaoni na kwenye magazeti wanayoyaita ya udaku mie nimezoea kuyaita ya Rangirangi kuwa 'ROSE MUHANDO AFIKIRIA KURUDI KWENYE UISLAMU' hapo nikapata mashaka na hofu kubwa iliyoniletea maswali mengi kichwani.
Ina maana sitosikia wimbo mwingine wa Rose Muhando​?
Kwa hiyo kilichomleta kanisani kilikuwa si cha kweli?
Nani kamfanya Arudi huko?
Nini kosa lake?
Hapo sikupata majibu zaidi ya kuzidi kujiuliza maswali mengi sana juu ya matokeo ya Rose kurudi kwenye imani yake ambayo ndiyo iliyomkuza na mapito tuu ya dunia yalimfanya aende kanisani.
Ni kweli amekuwa akishutumiwa kwa mambo mengi ambayo  huenda mengi hayakuwa hata na chembe ya ukweli kama vile Kutoa mimba,Kutumia madawa ya Kulevya , kuwatapeli mapromota na wakati mwinginehata namna ya uchezaji wake kwenye nyimbo zake ulikosolewa si tuu na wapenzi wa muziki wake bali hata wachungaji ambao kwa mujibu wa madai ya waandishi waliotoa taarifa za Rose kutaka kurejea Dini yake ya zamani wamedai kuwa ndicho haswa kilinachomwondoa kanisani.
Lakini, pia kitendo cha kuusifia utumbuizaji wa mwanamuziki H baba kuwa kama dhambi kwake kwa mujibu wa maneno ya watu.
Ni kweli huenda sababu hizo na nyingine zisizoandikwa ndizo zimtoazo kanisani lakini naomba nikuambie dada Rose kuwa haya yote yanayokuandama ni kama utelezi tuu unaotaka kukuangusha  Inuka simama na usonge Mbele hata kama utarejea kwenye Imani yako ya awali zingatia na ummtegemee muumba mweza wa yote kama ulivyokuwa ukituimbia na atakusimamia.
Kuhama hakutakupunguzia kusemwa zaidi ya uhuru wa nafsi ambao unaamini utaupata huko hivyo ukifika huko usije kukwaza na mambo yatakayozungumzwa juu yako na kufikiria kurejea kanisani kisha tena kutoka na mwisho wa kutangatanga kwako kutakutoa kwenye imani zote na kubaki njia panda kama kifaranga kilichompoteza mama yake.
Nakumbuka ulipoingia mkataba na SONY ulituambia utaimba zaidi hivyo kama utahamia msikitini IMBA ZAIDI kwani umepewa kipaji cha kumsifu na kumwomba Mungu kwa njia ya nyimbo.
Sina Mengi zaidi ya niliyokuambia hapo juu Huo ni utelezi endelea na Safari.
Niambie Chochote #mwanakalamumwenzangu

0 comments:

Post a Comment