Na.Moringe Jonasy
Kuna mwandishi mmoja wa gazeti la Raia Mwema aliandika kuwa Marehemu Mchungaji Mtikila aliuzidi wakati, akiwa na maana ya kuwa mengi aliyoyafanya wakati uliopita yalitakiwa yafanyike zama hizi.Mwandishi yule aliyaandika mendi sana yaliyofanywa na marehemu Mtikila enzi za uhai wake likiwemo suala ya kupanda mbegu za siasa za hoja na mantiki na kushikilia misimamo kwa hoja jambo ambalo mwandishi aliamini yalitakiwa kufanyika zama hizi.
Maneno yale yaliniiingia sana akilini na kunifanya nianze kufikiria watu na mambo ambayo yalifanyika mapema zana kiasi cha kuuzidi wakati na kujikuta nikiangukia kwenye sanaa.Nikakutana na kichwa kimoja chenye vipaji vingi kilichowahi kutikisa mwishoni mwa muongo uliopita.
Hiki kichwa si kingine bali ni kichwa cha mwanamuziki wa bongo -fleva ambaye wakati anatoka na wimbo wake wa Promice aliyekuwa mtangazaji wa Redio Free Afrika alikuwa akimwita Mb dog wa Bukoba akifananisha namna yake ya uimbaji na ile ya aliyekuwa amelikamata soko la muziki wakati huo Mb Dog.
Miezi michache iliyopita mwanamuziki huyu alizushiwa kifo kabla ya ukanusha na kudai alikuwa na ndoto za kuwa mwanasoka na kucheza ligi kuu nchini ama nje ya nchi jambo ambalo wengi waliliona ni kama kutafuta kile kinachoitwa kick kwani katika hali ya kawaida inawezekana mwanasoka kustaafu kisha kufanya muziki lakini kwa mwanamuziki kucheza soka baada tena katika umri ambao kwenye soka huitwa ni uzeeni ni maajabu kweli.Lakini huenda ni katika kuendelee kuuzidi wakati lakini safari hii nadhani ameuzidi kwa kubaki nyuma yake.
Licha ya haya yanayoendelea kufanyika sahizi ikiwa ni pamoja na kutoa nyimbo nyingi nzuri mfululizo ambazo hazina nguvu tena kama zilivyokuwa nyimbo zake za huko nyuma ila mwanamuziki huyu naona aliuzidi sana wakati kwa kutoa nyimbo ambazo naamini hata kama zingetoka leo hii zingeteka soko la muziki wa bongo na hata Afrika nzima kwani zilikuwa za kiwango cha juu sana ikijumlishwa na kukua kwa teknolojia katika utengenezwaji wa video.
Nyimbo kama kwa ajili yako,Kafia getho, Full shangwe, Utaipenda na nyingine nyingi ambazo zilikuwa kwenye albam zakembili za kwanza zingeweza kumpa tunzo nyingi za ndani na nje ya nchi lakini basi ndo hivyo aliutangulia wakati huyu mkali.
Nyimbo kama kwa ajili yako,Kafia getho, Full shangwe, Utaipenda na nyingine nyingi ambazo zilikuwa kwenye albam zakembili za kwanza zingeweza kumpa tunzo nyingi za ndani na nje ya nchi lakini basi ndo hivyo aliutangulia wakati huyu mkali.
Wapo wanaodai kitendo cha kwenda Kenya na kuanza kuimba nyimbo za kuwafurahisha wa Kenya pekee (Nitaandika kuhusu hilo) bila kuangalia Afrika mashariki ama Afrika kwa ujumla ni moja ya sababu zilizomrudisha nyuma lakini kuna mengi sana nyuma ya muziki wa Hussein ambayo hakuna mwingine zaidi yake ambayo yamemfanya ashindwe kuendelea kuutangulia wakati.
Labda nyimbo zake anazozitoa nazo zimeuzidi wakati tusubiri wakati wake ukifika tutazikumbuka na kutamani atuimbie lakini atakuwa ametangulia zaidi kwa kuimba nyimbo za miongo mingine ijayo.
#Niambiechochote mwanakalamu.
0 comments:
Post a Comment