Na.Moringe Jonasy
Kwa mara ya kwanza niliposikia wimbo wao nilihisi ni wimbo ulioimbwa na vijana kutoka jumba la vipaji THT baada ya kuhisi kulikuwa na sauti ya Barnaba, lakini baada ya kuusikiliza zaidi na kuwafuatilia waimbaji nikakutana na majina tofauti kabisa.Baadaye nikawatumia rafiki zangu wengi ule wimbo kupitia whatsap nikiwauliza kama walikuwa wakiujua ule wimbo mkali na wanipe maoni yao , matokeo yake katika watu kumi na tano niliokuwa nimewatumia ule wimbo ni mmoja tuu ambaye alikuwa akiwajua waimbaji wa ule wimbo tena si kwa majina na mmoja mmoja bali jina la Bendi yao Jembe ni Jenmbe band ama JJ band.
Sikushangaa sana kukutana na hali hiyo kutokana na namna vijana hao walivyojitangaza kwa wimbo mzuri badala ya kujitangaza kwa skendo na maneno mengi badala ya vitendo.Lakini kwa muziki wa kileo baada ya wimbo mkali kama Nishike wapenzi wa muziki mzurikuna kitu wanakisubiri nacho si kitu kingine bali ni Video nzuri si kwa kutaka kuwaona sura zao na kuogopa matapeli wanaojiita majina ya wanamuziki na kuwaibia watu bali ni kujitangaza zaidi ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu ikizingatiwa kukua kwa teknolojia ambapo siku hizi si lazima uwe na televisheni ndipo uione video bali hata kupitia simu za mikononi na kompyuta.
Lakini tangu mwezi mei hadi leo hii sijaona video ya wimbo huo wala kusikia lolote kuhusu video ya wimbo huo mzuri ambao mmoja wa wadau ninaojadiliana naye kuhusu muziki aliniambia ni Sauti Soul wa Miaka ijayo kama wataufanya muziki kama kitu cha thamani. Laki mdau mwingine akaniambia JJ band ni kama Jokate aliyeimba wimbo mkubwa Afrika Leo leo kisha akaanza bilinga bayoyo za kutoa video na kuwavunja moyo wapenzi wa muziki wake na kuhisi hakuupa muziki thamani kama anavyovipa vitu vingine avifanyavyo wisho wa siku inaonekana kama alijaribu kufanya muziki.
Hapo nikakubaliana na mdau huyo na kuwaona JJ band na Jokate wa Leo leo wakipita njia moja ambayo si nzuri hasa kwa wengi tulioukubali uwezo wao wa kisanaa japokuwa naweza kuhisi huenda mambo ya kiuchumi na usimamizi huweza kuwa sababu ya wao kufikia huko.
Naamini siku moja wakirekebisha tatizo hilo wanaweza kufika hata kule ambako hawakuwahi kuota kufika.
#niambiechochoteMwanakalamu
0 comments:
Post a Comment