Na.Moringe Jonasy
Kila mwanamziki kutoka nje ya Tanzania iwe nchi ya Afrika ama nje ya Afrika ukimuuliza kuwa angependa kuimba ama anamfuatilia mwanamuziki yupi wa kike basi atakuambia Vanessa Mdee na kwa wanaume atakuambia Diamond Platnumz.Si P square,Waje,Ne-yo, Kimani(Victoria) ,Yemi Alade , 2 face na wengine wengi wimbo ni huo huo Vanessa na Diamond japokuwa wengine pia hutajwa ila hawa ni kama vilele vya mlima wa Tanzania.
Hawa wote wamepita njia tofauti za muziki wakati Diamond akitumia muda mrefu ''Kutoboa'' tena kwa kutumia njia ya kushirikiana na mwanamuziki mkubwa kwa upande wake Vanessa alianza kuuwa mkubwa Afrika kabla hata hajafanya wimbo na mwanamuziki mkubwa wa nje na hata alipokuja kufanya alichokifanya ni kuongeza tuu ukubwa wa jina lake.
Vanessa Mdee ambaye amekuwa mfano wa kuingwa na wanamuziki wengi chipukizi anastahili pongezi kwa mafanikio yake yeye pamoja na walio nyuma ya juhudi zake kwani kwa binti kama yeye kufika alipo kuna vikwazo vingi njiani.
Hapa napenda nitumie neno ''Bravo'' kukupongeza.
Lakini licha ya pongezi nilizotoa ambazo najua wengi ama wamezitoa kabla yangu ama watakuja kuzitoa baadaye nitakuambia ulipozingua kama pale kilele kingine cha muziki hapa nchini ambaye naweza kusema ni pacha wako Diamond Platnumz alikosea.Najua alijua kuwa alikosea ndiyo maana sioni tena akikosea kama alivyokosea kwenye video ya wimbo wa Nasema nawe ambao ni aibu kuitazama ukiwa na watu unaowaheshimu.
Licha ya wengi kuutetea kuwa ni utamaduni wa watu wa Mwambao wa nchi ( Siyo utamaduni wa nchi nzima) bado video ile ambayo ilipata umaarufu mkubwa si Afrika tuu hata nje ya Afrika inabaki kuwa video Mbaya isiyo namaadili kati ya video zake zote.
Kwako video ya wimbo mzuri wa 'Never Ever' watu wa mtaani wanaweza kusema ''Umezingua'' kwani umeonekana si tuu kushindwa kufuata maadili yetu bali hata ya wenzetu umepitiliza.
Kugauni kilicholowa ukichezesha mwili , Loh! utamaduni wa wapi huo, ama ndo kimataifa?
Kwa nini usifanye kama ''No body but me''?
Kweli ''umezingua'' ila bado una nafasi ya kubadilika katika video nyingine huku lawama hizi za ''kuzingua'' kwako ziwafikia na walio nyuma ya ''kuzingua'' kwako kama walivyoipokea ''Bravo'' yangu na ya wapenda muziki mzuri wenzangu.
Naomba kuwasilisha.
#niambiemtazamowako.
0 comments:
Post a Comment