Na.Steven Mwakyusa
Kuna kipindi ngoma kali huwa zinatoka kwa pamoja, sijui kama ni coincidence tu au huwa inapangwa kabla!! Kama ni mfuatiliaji wa muziki wa hapa kwetu utagundua kwamba kuna msimu ambao nyimbo kali huwa zinaachiwa, mara nyingi ni mwishoni mwa mwaka..na mwanzoni mwa mwaka yaani January na February!!
Mpaka sasa kuna new release kadhaa ambazo kwa namna moja au nyingine zitaenda kusumbua kwa mwaka unaoisha na unaoenda kuanza!!
1. Ruby-Sijutii
Ruby ambaye ni hitmaker wa "Na yule" pia baada ya kufanya vizuri katika "Nivumilie" ya Barakah Da prince pia "Ayaya" ya Abdu kiba amekuja tena katika "Sijutii"..Ruby ni mmoja wa wasanii wa kike wanaozitendea haki sauti zao, kiufupi ni msanii ambaye anaweza kufanya maajabu hapa nyumbani na hata nje ya nchi! Pata wasaa kusikiliza sijutii hakika hutajutia muda wako!!
2. Rich Mavoko-Naimani
Huyu naye ni mmoja ya wasanii wanaovitendea ipasavyo vipaji vyao! Silali ndiyo ngoma iliyompa jina katika muziki, na baada ya hapo hakika hajawahi haribu..ni kuanzia "Marry me", "Follow me", "Roho yangu" pia "Pacha wangu". Humo ndani ni kuanzia uandishi mpaka beat vimesimama...kama hujaipata jipe muda kuisikiliza!!
3. Mo music-Skendo
Huyu baada ya "Basi nenda" nilianza kutia shaka kuhusu uwezo wake, hasa uwezekano wa kutoa kazi yenye ukubwa kuizidi "Basi Nenda". Angalau "Nitazoea" ilianza kunirudisha kwenye mstari, katika "Skendo" kazidi kuonesha uwezo wake..kifupi jamaa anaweza! Jipe muda pia kumsikiliza!
NB; Kuna ya Alikiba "Lupela" pia kazi ya Diamond zinakuja, hawa ni kama wanategeana hivi, ngoja tuzidi kuwangoja tu!!
0 comments:
Post a Comment