Na.Steven Mwakyusa
Inawezekana Ray C ndiye msanii aliyetajwa mara nyingi zaidi katika nyimbo za Bongo Fleva!!
Mwanzoni mwa miaka ya 2000, Rehema Chalamila ama Ray C kama alivyokuwa akijiita alipata umaarufu mkubwa siyo tu katika uimbaji, bali uwezo wake wa kuzungusha kiuno!!
Vibao kama Mapenzi yangu, Wanifuatia nini, Na wewe milele, sikuhitaji pia mahaba ya dhati vilitosha kumuweka katika chatt ya juu katika huu muziki!!
Kinachoitwa kiuno cha Ray C kikawa gumzo na kupelekea wasanii wengi kuandika mashairi kukihusu,
Hizi ni baadhi ya nyimbo zilizomtaja Ray C kwa namna moja au nyingine!!
1. Mabinti-Mwanafa
MwanaFa ambaye alitamba na hiki kibao baada ya ingekuwa vipi! MwaFa anasema katika moja ya mistari yake
"Kuna kifua kama cha Zay B, kiuno kama cha RAY C, Na pozi kama za Jay dee sauti kama ya Fina""
2. Binti Malkia-Fid q
Hapa Fid Q alikuwa anajaribu kueleza jinsi alivyofika kwa binti malkia..Ra C hakuachwa katika mfananisho na Binti malkia..
Fid anadai...
"akizungusha rusha roho yani utadhani RAY C"
3. Kama unataka demu-Jmoe, Solo Thang & Chief
Hiki ni kibao kilichowakutanisha wakali watatu wa kipindi hicho...Solo Thang katika mistari yake anaimba...
"Yoh Nataka demu miguu mizuri kama RAY C, Macho kama Asia..."
4. Speed 120-Ngwea & Chidy Benz
Ray C aliendelea kutajwa na hapa Mangwea aliendeleza kile walichofanya wengine...
Ngwea anaimba "Mwishowe msije mkakata viuno stejini kama RAY C"
5. Family-Solo thang ft Jay moe...
Licha ya huyu mkali wa vina kutaja wasanii kibao katika hii ngoma Ray C hakuachwa nyuma! Moja ya mistari ni huu..
" Nataka kuwa na ww milele..ray c mbona mchokozi"
6. Nilikaona mwaka jana-Soggy Doggy
Nakaita hata hakasikii
Katoto kana mvuto utadhani ni RAY C
Pia ametajwa katika Sikiliza ya Mangwea, Ni mzuri ya Malick pia
NB: Nionavyo Ray C anabaki kusimama kama alama muhimu katika muziki wa bongo flava, ni msanii aliyekuwa na ushawishi wa aina yake miongoni mwa wasanii wa kike kupata kutokea! Baada ya dhoruba zilizomkuta, Ray to the C amejitahidi kurudi katika game bila mafaniko!
Mpaka sasa ana ngoma inaitwa "Mshum Mshum"..ni kazi nzuri ila sema wakati haupo kwake tena!!
Je ni kipi unakikumbuka toka kwa Ray C?
0 comments:
Post a Comment