Nafsi ya mtu ni jumba,jumba la giza totoro,
Tena lenye vingi vyumba,usiyojua zoke kasoro,Waweza kuhisi cha simba, kumbe chumba cha kongoro,
Nafsi inabeba mengi, ni siri ya mwenye nayo.
Machoni naona pendo,pendo lile nitakalo,
Wala silioni pindo,pindo linichukizalo,
Na sivihisi vishindo,wala baya uwazalo,
Nafsi inabeba mengi, ni siri ya mwenye nayo.
Imani ninajivika,imani ile imara,
Na pendo nimejitwika,pendo si biashara,
Ufamle nimejivika,na malkia hongera,
Nafsi imebeba mengi, ni siri ya mwenye nayo.
Nikuonapo wacheka,cheko linakuja kwangu,
Pindi unasikitika,waliteka cheko langu,
Ubaba nimejivika,nakuona mke wangu,
Nafsi imebeba mengi,ni siri ya mwenye nayo.
Na leo sina jeuri,nawaza nikwite nani,
Nilijitia kiburi,kama nimekweka ndani,
Nawaza wako uzuri,sijui atapewa nani,
Nafsi imebeba mengi,ni siri ya mwenye nayo.
Kweli nafsi kichaka,ama paka gizani,
Nimekosa pa kushika,na nitampenda nani,
Sasa ninaweweseka,kwama vile punguani,
Nafsi imebeba mengi,ni siri ya mwenye nayo.
Upendo ni jadi yako,hilo kumbe sikujua,
Nikahisi mie wako,kudeka nikazoea,
Siku inakwenda huko,nitajizuiq kulia,
Nafsi imebeba mengi,ni siri ya mwenye nayo.
Kaditama ninatua, huku nahisi ndoto,
Nimechelewa kujua,kweli penzi utoto,
Wengi nimewasumbua,kuhisi nakwepa moto,
Nafsi imebeba mengi,ni siri ya mwenye nayo.
Merkur 37C Safety Razor Review – Merkur 37C
ReplyDeleteThe Merkur 37c is an kadangpintar excellent short handled DE 출장안마 safety razor. It is more suitable for both heavy and non-slip hands and is therefore https://deccasino.com/review/merit-casino/ a great option for experienced febcasino.com