"Elastic Heart" ni moja ya nyimbo zilizofanya vizuri sana katika chart za muziki za Uingereza na Marekani, Elastic heart ni wimbo wa mwanamuziki ajilikanae kama "Sia"..katika Elastic Heart Sia haonekani mahali popote zaidi ya kusikika sauti yake ilipangika vilivyo!! Sauti inasikika ni ya mtu mzima ila anayeonekana katika video ni binti mdogo wa miaka 14 ajulikanaye kama "Maddie Ziegler"!!
Maddie Ziegler pia ameonekana katika wimbo wa "Chandelier", "Cheap Thrill" pia wimbo unaotamba kwa sasa katika chart mbali mbali za muziki uiitwao "The greatest"
Kwanini Sia haonekani katika video zake licha ya uwezo wake mkubwa wa kuimba, ili ni swali ambalo lilinifanya nizidi kupekua huyu Sia ni nani hasa?
Sia Furler alizaliwa December 18 mwaka 1975 huko nchini Australia, alianza shughuli zake za muziki mwaka 1993 na akaja kutoa album yake ya kwanza mwaka 1997 iliyokwenda kwa jina la "only see", mwaka 2000 alisainiwa na label ya Sonny Music na akafanikiwa kutoa album yake ya pili "Healing is difficult", pia aliweza kutoa album kama "some people are real problems" (2008) na "we are born" ya mwaka 2010!!
Baada ya album ya mwaka 2010 Sia alianza kupata athari za pombe pia madawa ambayo alikuwa akitumia kwa muda mrefu, muziki ukawa mgumu sana kwake hali iliyopelekea mpaka kupelekwa Sober, na baadaye alirudi katika hali ya kawaida!!
Sia aliamua kurudi kwenye muziki, ila akilini alijua umaarufu wa muziki ndiyo ulimpeleka katika matumizi ya kupindukia ya pombe na madawa! Kuanzia hapo Sia aliamua kurudi katika muziki, ila hakutaka kuonesha tena sura yake hadharani!!
Mwaka 2014, Sia alitoa album aliyoiita "100 forms of fear" ikiwa na vibao kama "Chanderlier pia Elastic Heart"!! Licha ya nyimbo hizi kuvunja rekodi mbali mbali, ikiwa pamoja na kuangaliwa youtube zaidi ya mara 2.7billion, bado Sia hakutaka kutoka hadharani pasipo kuficha sura yake, iwe katika show hata katika interview za tv na radio Sia ameendelea kuficha sura yake!!
Mwaka 2016 pia umekuwa wa mafanikio kwake, album ya "This is acting" imeendelea kufanya vizuri huku vibao kama "Cheap Thrill" na "The greatest" vikizidi kushika chart za muziki!
Kiufupi Sia ameleta kitu kipya katika muziki wa Pop, identity yake imeendelea kuwa mjadala katika mitandao ya kijamii, pengine ndilo lilikuwa lengo lake toka awali, kwa hapa kwetu wanaita kick, lakini je kwa hapa kwetu msanii gani anaweza kuhimili kuficha sura yake siku zote?
NB; Sia pia amewahi kuandika nyimbo kama Diamond ya Rihanna, Pretty hearts ya Beyonce, Perfume ya Britney Spears pia kashirikishwa katika "Titanium" pia Bang my head" Zote za David Guetta
0 comments:
Post a Comment