Na.Steven Mwakyusa(Mtu Makini)
Ushindani katika burudani ya muziki si kitu kipya, ushindani uekuwepo miaka na miaka!! Kimsingi hii ni asili ya binadamu, japo wanasema asiyekubali kushindwa si mshindani..ila mimi naamini mshindani wa kweli ni yule asiyekubali kushindwa! Kushindana kunaenda mbali zaidi hasa pale ambapo maslahi binafsi hasa ya kiuchumi yanapoanza kuguswa!
Ni wazi muziki umetawaliwa na tambo za kila aina, na hili tulilizoea hasa kwa wale wasanii waliokuwa wakiimba hip hop..ushindani unapokolezwa na mengineyo ndipo huibuka kitu kinachoitwa beef!
Huu ushindani unaopelekea beef kimsingi ndiyo uliovunja makundi kama 2berry, HBC, TnG squad, Gheto Boys, Watu Pori na Wateule kwa kutaja kwa uchache..
Hivyo basi beef inaweza kuwa baina ya wasanii ndani ya kundi moja, au wasanii wasiohusiana kwa lolote!
Kihistoria imeshuhudiwa beef zifuatazo hata kama wao hawakuweka wazi, au pengine hazikupata attention ya watu
1. Afande Sele Vs O ten
2. East Coast team Vs TMK family
3. ECT vs Tmk wanaume Halisi
4. Juma Nature Vs Inspector Haroun
5. Fid Q Vs Rado
6. Afande Sele Vs Ditto & Koba
7. Afande Sele Vs Madee
8. Afande Sele Vs Soggy Doggy
9. Afande Sele Vs Solo Thang
10. Zay B vs Siste P
11. TID vs Dully Sykes
12. TID vs Q Chief
Kwahiyo ukiangalia wasanii wengi katika kutofautiana kwao, Afande Sele ndiye ameongoza kutofautina na wasanii wengi!
Na hii ilichagizwa sana na ushindi wake katika Shindano la Ufalme wa Rhymes la mwaka 2004 kwahiyo ukichunguza Afande alikuja kuwa na beef na wengi waliokuwa hawakubaliani na ushindi wake.
Sasa mwaka 2014, aliibuka mfalme mwingine na kuleta sintofahamu katika game ya muziki wa hapa nyumbani, Alikiba alirudi baada ya anachokiita likizo na kuanza kujiita King..akimaanis ha Yeye ni King of Bongo fleva. Huu ufalme haukupokelewa kwa hisia sawa na wapo wengi wanaohoji mpaka leo ni wapi Alikiba Alipewa huo ufalme na nani alimpa, hata ukiniuliza mimi hilo silijui..
Huu ufalme ndiyo ulioenda kuchagiza kile kinachoiywa beef baina yake na nguli mwingine katika bongo flava "Diamond"...kau li za kiba kwamba kaja kufuta vumbi kiti chake pia akidai kizuri kikikosekana hata kibaya huonekana hazikuacha mtazamo chanya hata kidogo...
Huu ndiyo ukawa mwanzo wa kinachoitwa timu baina ya hawa wawili, team zikachagizwa na uwepo wa mitandao huku tambo na kejeli zikizidi kuibuka na kuhusisha walioko na wasiokuwamo!
Hivyo basi hizi tambo hazijawahi fikia tamati, kila upande umekuwa ukivutia kwake! Na hili limeweza kuathiri wasanii wengineo kwa namna moja au nyingine!!
Hivyo nani ni namba moja hiyo siyo hoja yangu kwa leo, hoja yangu ni kutaka kujua je ni msanii/wasanii gani wanaofatia baada ya hawa wawili, llabda niseme ni nani msanii namba 3 baada ya Kiba Diamond?
Je ni Baraka, Benpol, Jux ama Barnaba? Je hawa wasanii wanaweza simama peke yao na wakafanya show iwe ndani au nje ya nchi?
Ni nani msanii namba 3? Je ni Ruby, Vannesa Mdee, Maua au Mwasiti?
Ni nani anaweza kufikia ukubwa wa hawa wawili? Ni RayVan, Harmonizeau Rich mavoko ?
Nakaribisha michango yenu!!
0 comments:
Post a Comment