Wednesday, 21 December 2016

TULIWATEGEMEA WAKAPUYANGA


Na.Mwanakalamu
Muziki ni kazi na biashana, kwenye kazi siku zote hazilingani na kwenye biashara pia kuna faida na hasara.Mwishoni mwa mwaka uliopita na mwanzo wa mwaka huu wengi tulitegemea wanamuziki wengi wangekuja kuwa moto wa kuotea mbali lakini mategemeo hayo yamebaki kuwa ndoto za mchana ambazo ama tunazipuuza ama twazisukumua mbele.Wanamuziki wafuatao ni kati ya wale waliotegemewa sana lakini matokeo yake yakawa si vile tulivyoamini;

KAYUMBA JUMA
Mshindi huyo wa BSS alitupa matumaini makubwa kuwa angekuja kukamata soko.Mwonekano wake sauti yake na aina ya muziki ambao alionekana kuupenda akiwa mashindanoni zilikuwa ni moya ya sababu zilizotufanya tutabiri hayo.
Tofauti na tulivyotegemea Kayumba alitoa nyimbo mbili kama sikosei ambzo licha ya kupata nafasi kwenye vituo vya redio na TV wakazi zainatoka lakini amsikio ya wengi yaliishia kutoamini kilichosikika kwenye spika za redio na TV.
Ni kawaida watu wengi wapatao umaarufu kabla ya kutoa nyimbo zao kupata shida ya kuteka hisia kwa muziki lakini naamini bado Kayumba ana nafasi ya kung'aa zaidi.
Nilitamani sana huyu kijana angeungana na Yamoto band kwa uimbaji wake kurandana sana lakini naamini ana nafasi ya kuwa nyota siku za mbele hata akiwa peke yake.

FRIDA AMAN
Huyu pia alitukamata kwenye mashindano ya BSS tukiamini angekuja kushindana kwenye muziki wa wanawake lakini sina hakika kama amefanikiwa kuachia hata wimbo mmoja.Inagawa nilisikia siku ya mwisho ya mashindano kuwa yeye na washiriki wenzake waliofanikiwa kuingia tano bora wangekua chini ya usiamamizi fulani kwa mwaka mzima lakini mwaka unaisha hali ipo tulii.
Bahati imekuwa njema kwake kwani amejikuta akiangukia kwenye utangazaji ambako naona anakumudu sana.

YAMOTO BENDI
Yamoto Band sijui nini kimewakuta , walianza mwaka vzuri sana huku wengi tukiwatabiria mengi mema.Hawa vija wanne wenye vipaji wamejikuta hawapo kwenye masikio ya watu robo tatu ya mwaka huu.
Sahizi tulikuwa tunategemea ratiba ya kutumbuiza huku na huko.Wimbo wao wa mama haukuwa na nguvu sana kama zilivyokuwa nyimbo zao za nyuma na hata walipotoa wimbo mwingine umeishia kutambulishwa na kusikilizwa wakati ukitambulishwa.
Bahati mbaya hata wakishirikishwa ama kila mtu akiimba kivyake wamekuwa si wale waliozoeleka tena.


RUBY
Huyu tulimwona kama Vannesa mwingine, alkini sijui nini kimemkuta.Licha ya nyimbo zake za mwanzo kuteka hisia za wengi lakini huyu binti inaonekana kismati kimeshuka aekuwa si yule aliyetegemewa.
Japo wengi wanaona kama kutoka THT lakini hata alipokuwa hapo chati yake ilikua ikishuka taratibu.
Tumpe nafasi mwakani.

MAYUNGA
Mkali huyu mwenye kipaji kikubwa kilichopelekea kufanikiwa kurekodi wimbo na nyota wa muziki duniani Akon amekuwa sivyo tulivyoamini angekuwa.Ametoa nyimbo mbili moja akifanya na Akon na nyingine ikimpa nafasi ya kushiriki EAT Awards.Zote zimekuwa nyimbo nzuri lakini bado hazijafanya kuwa vile tulivyotegemea.
Sijui ndiyo Kismati lakini nadhani hata uchache wa nyimbo zake na matarajio makubwa tuliyokuwa nayo kutoka kwake.

FONABO
Aisee huyu mtu anaimba, nilikuwa shabiki mkubwa wa Kayumba juma kutokana na kuimba nyimbo nilizokuwa nikizipenda pia historia ya maisha yake ilinifanya nimhurumie na nikatamani ashinde kitita cha pesa ili akaokoe familia yake.Ila kipaji cha Fonabo kilikuwa cha hali ya juu, ile imba yake nikawa naomba asije kuonana na 'demu' wangu maana asingehitaji kumwaka vocal lakini huyu mkali sijui kapotelea wapi maana tulitegemea angekuja kutushika haswaa.

Wapo wengi sana wameshindwa kutimiza vile tulivyotabiri juu yao lakini hawa ni miongoni mwao.Wanamuziki kama Mwasiti,Abdukiba,Nay Lee,Q Chillah na wengine wengi wanaingia kwenye kundi hili.

0 comments:

Post a Comment