Na.Mwanakalamu
Miezi michache iliyopita,mwanamuziki Alikiba alitangaza rasmi kuwa ana ''Music Lebel'' ambayo itakuwa inasimamia wanamuziki kadhaa;Abdukiba, Jokate, AbbySkills ,Brown Mauzo na wengine wengi.Kwa mujibu wa maelezo yake alidai kuwa lebel hiyo ilikuwepo tangu muda kidogo hakuamua tuu kuitangaza,mwanzoni nilidhani ni ile tuliyokuwa tukiisikia kwenye nyimbo zake nyingi za albam yake ya pili ''After the middle finger Entertainment'' kumbe ni mpya yenye jina la 'Kings Music'.
Muziki na usimamizi wake ni biashara inayolipa sana kwa kipindi hiki lakini pia huhitaji gharama kubwa kuanzia fedha,muda,, ujuzi na mengine mengi.
Najua Alikiba ni mwanamuziki makini sana ambaye ameudhihirishia ulimwengu kwa kufanya mambo mengi sana kwa mwaka huu likiwa ni hilo la kuazisha lebel ya Muziki.Lakini pamoja na umakini wake kuna ushauri pia atahitaji kutoka kwa wadau wa muziki ili kufanikisha hili alilo lianzisha.Yafuatayo ni mambo makubwa matano ambayo Alikiba anaweza kuyafanya katika kuifanya Kings Music kufanikiwa zaidi.
1.FUNGUA STUDIO YA MUZIKI
Hili linaonekana kutokuwepo kwenye mipango yakO kwa mujibu ya maneno uliyoyatoa kwenye #Papokwapapo na Papi wakati ukijibu swali la mmoja wa watumiaji wa twiter.Japokuwa ulisema jambo hilo ni muhimu pia kwa wanamuziki hasa katika kuhifadhi nza kuendelea mawazo ya nyimbo yanapomjia kichwani.Lakini kwa 'lebel' kuwa na studio yake itasaidia mengi sana kufanyika kwa uhuru zaidi kwani kundi litakuwa na nafasi ya kufanya mambo yake kwa uhuru zaidi badala ya kusubiri zamu kwenye studio nyingine.
2.UWE NA BENDI YAKO
Alikiba ni mtu wa Live Band na hata wanamuziki wako wanaonekana kuwa ni wafuasi wa muziki wa aina hiyo hivyo litakuwa jambo la busara sana kuwa na kitu hiki.Pia itasaidia sana kupunguza gharama za kuzilipa bendi nyingine wakati mwingine kuepusha kutofautiana ratiba na bendi hizo za kukodi.Studio iwe imekamilisha na bendi ili pia kuweka uhuru wa wanamuziki wake kufanya mazoezi kwa uhuru na kujenga kile kiitwacho ''Chemistry'' inayoeleweka ya muziki.
Hili si tuu litawapa uhuru bali litaingizia lebel pesa za kutosha pale bendi yake itapotumiwa na wanamuziki wengine.
3.WASAJIRI ABBY DADY,MAN WATER NA GODLUCK GOZBET
Hawa wana studio zao ila unaweza kuwaleta studio kwako kwa makubaliano na pesa za kutosha.Wanaweza kuwa pia kama wamiliki wenza wa lebel yako.Unaweza kujiuliza kwa nini ufanye hivyo jibu rahisi tuu sana ukilinganisha biashara ya muziki na biashara nyingine katika zama hizi za kibepari kukusaya raw materials ni moja ya mbinu ya kibiashara.
Abby Dady ni mtu ambaye najua mmezoeana sana na anajua nini unakihitaji kwa wakati gani lakini pia ni mtengenezaji mzuri wa midundo hivyo ataweza kukupa nini wanamuziki wako wanataka.
Man Water huyo ni habari nyingine kwenye kuzalisha muziki unaokubali kupigwa na live band.Si unakumbuka Dushelele na Mwana?Huyo anaweza kuendelea kuwa studio kwake lakini akifanya kazi kwako kama part time lakini akiwa mwanaKings Music itakuwa poa sana.
Huyo Godluck kama jina lake ,kabarikiwa vipaji vingi anaweza kutunga,kuimba na kuproduce hivyo unaweza kumsajiri ukizingatia vipengele hivyo
yaani hapo ni kama unasajiri watu watatu na usiogope kutumia pesa maana itarudi zaidi.Huyo atasaidia katika kubalance muziki wa lebel yako badala ya kuegamia kwenye muziki wa kuchezeka zaidi.
Ukiwa na hao watatu muziki wenu hautochosha watu wala kufanana sana na utakuwa ni chakula bora kwenye bongo za wasikilizaji.
4.ABBY SKILS
Huyo ni mwanamuziki mkongwe uliyemkuta kwenye muziki, na anamchango mkubwa kwako.Unatamani awe juu kimuziki ukijaribu kurejesha fadhila.Ni mkali pia wa kutunga nyimbo hivyo ni vyema akatumika zaidi upande wa kutunga zaidi kuliko kuimba.Si kwamba hajui kuimba bali anajua zaidi kutunga na nyimbo zake nyingi anaonekana kuhitaji kushirikiana na wengine hivyo mwache atunge huku akija kuimba kwa mara moja moja sana pale anapojisikia.
Si kitu kibaya kwa muziki huu unavyoenda.
5.MR BLUE ,RAMA DEE,MAD ICE NA KALAJEREMIA
Najua ni wanamuziki ghali ila ukifanikiwa kuwasajiri na kuwaweka kwenye lebel hiyo mtakuwa mmeongeza madini ghali kwenye muziki wenu.
Hao ni kati ya wanamuziki wakali na wakubwa sana hivyo kwa lebel yenu kuwa nao ni faida kwao na kwa lebel.
Mwisho nikupongeze kwa mafanikio uliyoyapata kwa mwaka huu huku nikikuombea mafanikio makubwa sana mwakani na miaka minginge ijayo.Natumai chati yako itazidi kupanda kadri siku zinavyoenda. Pia kuwa na studio yako, maproducer na bendi yako siyo kufuli la kukufunga wewe na wanamuziki wa lebel yako kurekodi kwako pia muwe na vifungu vya kuwaruhusu kurekodi kwingine pia wao kurekodi nyimbo za wanamuziki wengine.Pia uwe na Dj na Cameraman pia wafanye ziara ya kwenye vyombo vya habari vya ndani na nje ya Afrika ili kuutangaza muziki wenu kimataifa zaidi.
Naomba kuwasilisha.
0 comments:
Post a Comment