Sunday, 5 February 2017

ANAANDIKA MELISSANilimfahamu kupitia rafiki yangu, hakuonekana kujali wala kuwa na muda na wanawake kwani hata huyo rafiki yangu alikuwa akiniambia hivyo.lionekana mwenye haraka sana na kila anachokifanya na hupenda sana kujali muda, si kwa kuiangalia saa kila dakika bali nadhani alikuwa na saa yake kichwani iliyowekwa 'alam' kwani hata kama mtakuwa katikati yaa kushughulikia suala fulani na juda mliojipangia ukapita ule mliojipangia atasema muda umefika tupange siku nyingine.
Tabia hiyo iliwakera wengi sana hasa wanawake ambao ni mabingwa sana katika kupoteza muda kwa kujivuta, ingawa si wote ila wengi.Tofauti na wengi walivyokuwa wakiichukia tabia yake mie ilinivutia na taratibu nikajikuta nikivipenda vingi alivyokuwa akivipenda huku nikitamani kuwa kama yeye katika kujali muda.
Nilipenda muziki aliokuwa akipenda kuusikiliza , nilipenda kwenye kuangalia mpira wa wavu kwenye viwanja vya chuo jirani kwani chuoni kwetu hapakuwa na wapenzi na wachezaji wengi wa mchezo huo na walipokuwa wakicheza hawakuwavutia wengi hivyo ilikuwa ni bora kutembea mita miatano hadi chuo cha jirani pia nilipenda tabia yake ya kupenda kusoma vitabu.
Kupenda vingi alivyovipenda kulitufanya tuwe karibu na baadaye tukawa marafiki kabla ya kuja kuridhiana na kuwa wapenzi.
Mwanzo wa penzi letu lilikuwa ni penzi matata na lililompendeza kila mmoja wetu huku tukijaribu kunakili na kuendana na tabia za mwenzake.
Baadaye penzi likiwa katika kilele chake ambapo mengi ambayo kila mmoja wetu alikuwa akiyatamani katika mapenzi alikuwa ameyapata katika kiwango cha juu kabisa nikajikuta simtamani tena, sikuwa na sababau ila nikajikuta simpendi , si kwamba nilimchukia ila kama nilimchoka hivi yaani nilitamani tena tuwe tuu marafiki wa kawaida na si wapenzi tena.
Nikatamani kumuwambia tuachane, nikajikuta sina sababu ya kumwambia tuachane hakunikosea , sikumkosea labda niseme ndo nilikuwa naanza kumkosea kwa maksudi kwa kumwacha.
Nilitafuta kila sababu walau akosee kidogo tuu ili nimwambiae tuachane lakini ni kama alijua kwani alikuwa hakosei na hata nilipokuwa namkosea alikuwa akiomba msamaha na kuonesha waziwazi ile hofu ya kuogopa kunipoteza.
Hapo akaanza kutojali muda kwenye mambo yake na kuanza kunijali sana, kuna muda alikuwa tayari kunihangaikia kuliko kuwaza mambo yake na yakifamilia, nilijua si kwamba alipenda iwe hivyo bali ilimtokea tuu kama vile ilivyonitokea kuanza kutompenda.Kadri alivyokuwa akihangaika kunipenda na kunifanyia mambo mazuri ndivyo nilivyozidi kumchukia na kila alilolifanya kwangu nilikuwa nikilichukia,nilichukia nilichukia baadaye nikamchukia na huruma kwake ikapotea, nikaamua kufanya kitu ambacho kitamfanya aamini kuwa simpendi.
Ilikuwa ni wiki ya mwisho ya maandalizi ya mitihani ya mwisho ya mwaka wa masomo chuoni.
Siku mbili kabla ya kufanya mitihani, ilikuwa ni siku ya jumamosi, palikuwa na mwanamuziki ambaye alikuwa akimpenda sana akitumbuiza kwenye tamasha moja lilifanyika kwenye klabu moja maarufu ya usiku.Aliniomba twende pamoja lakini nilikataa na kumsimanga kwa maneno machafu 'eti anamshobokea mwanaume mwenzake lazima atakuwa matataizo''Alijua kama ulivyojua ni matatizo yepi niliyokuwa nayamaanisha kwa kumshobokea mwanamuziki huyo ambaye alisema alikuwa akizikubali sana kazi zake na kuhudhulia tamasha lake angekuwa ametimiza moja ya lundo ya ndoto zake.
Alionekana kuumia lakini aliomba msamaha na ruhusa kuwa angeomba aende peke yake , nilimruhusu nikiwa nimeshapata mbinu ya kumfanya niachane naye.
Nilimwacha aende peke yake, na kipindi hicho alikuwa amepunguza ukaribu na marafiki zake wa karibu katika harakati za kutaka kulijenga penzi letu ambalo nilikuwa nalibomoa kwa nguvu zote.Alipoondoka ikamfuata rafiki yake ambaye alikuwa si mpenzi wa muziki nikijifanya nataka tusome naye kwani tulikuwa kozi moja.
Rafiki yake bila kujua hila zangu alikubali tusomee kwake usiku ule na bila kujua alijikuta akifanya mapenzi na mie usiku kucha hadi panakucha.
Nilitaka atufumanie usiku ule kani nilia mini lazima angempitia rafiki yake usiku ama kwenda kulala pale kwania likuwa akikaa hostel zilizokuwa ndani ya chuo na asineweza kukuta pamefunguliwa kwa muda ambao angerudi.Tofauti na nilivyodhani hakutumania tukajua bali alirejea mapema sana kwani huko alijikuta anahisi kanikosea kwa kwenda klabu akiniacha mwenyewe hivyo alipanga aniombe msamaha kisha aende kwa rafiki yake kulala kwani nilikuwa nikikaa na rafiki yangu asingeweza kulala pale.
Alipofika kwangu alibisha hodi hadi alipochoka huku akipiga simu yangu bila kupokelewa, akaondoka na kwenda kwa rafiki yake ambaye nilikuwa nimelala naye , aliingia hadi pale chumbani na kutuona tukila raha, alituchungulia kwani maksudi niliacha malango wazi bila kuufunga hivyo aliingia moja kwa moja.Kwa kuwa tulikuwa katikati ya raha hakuna aiyemuona , aliondoka na kwenda kwa rafiki yake mwingine alipolala hadi asubuhi.
Mchana wa siku ile aliniuliza kwa mitego juu ya kilichotokea jana yake nilimjibu kwa jeuri sana kumuumiza ili aniache ila hakufanya hivyo ingawa aliumia.
Tukafanya mitihani na matokeo yake yalikuwa mabaya sana, kwa kifupi Ali 'disco'.Lakini leo hii ni Injinia aliye na mafanikio makubwa sana ana familia yake yenye furaha sana.
Mimi ni mke na mama wa watoto watatu familia yetu ipo vyema pia lakini tukio lile linaniumiza kila siku na kunipa amani.

Nimekuandikia Moringe najua utaandika kisa kimoja kizuri sana na kuwa funzo kwa wengine....
NIMESHINDWA KUANDIKA KISA KIZURI KWANI MANENO YAKE TUU NI KISA CHENYE MAFUNZO...
Niambie ulichojifunza kwenye kisa cha Melisssa.
NB;Melisa si jina lake halisi.

0 comments:

Post a Comment