Sunday, 5 February 2017

BARAKA DA PRINCE NI NINI TUJIFUNZE KWAKO?
Na.Mwanakalamu.
Kumbuka kipindi kile unahangaika kuimba upo peke yako huku ukiwa na ndoto nyingi.Kumbuka kipindi upo na rafiki yako unayemwamini ukimwimbia na baada ya kuimba anaigiza kama mtangazaji akikfanyia 'interview' kana kwamba unautambulisha wimbo huo kwenye moja ya redio kubwa ambayo kwa wimbo wako kusikika basi utakuwa umefika kwa watanzania wengi wapenzi na wasio wapenzi wa muziki.
Vuta picha tuu anapooigiza kukupongeza kwa ksuhinda tunzo ya muziki ya mwanamuziki bora.
Halafu yote umeyapata, kuanzia mahojiano ya kutambulisha nyimbo, kushinda tunzo na kuimba nyimbo ama kukutana na wanamuziki na watu wengine maarufu ambao huwahi kuwaza kuwa uanweza hata kuwashika mkono.
Inakuwa ni kumbukumbu inayosisismua na kukufanya umshukuru Mungu kwa ulikotoka.
Kumbukumbu ambazo huja wakati fulani pekee unapokuwa peke yako ukikumbuka ukuu wa muumba juu ya maisha yako.Unatafakari kama si muziki ungekuwa nani unabaki kubashiri namna ambavyo ungekuwa.
Lengo la kukuandikia leo si kukukumbusha tuu ulipotoka na hisia hizo za kusisimua ambazo naamini kila mmoja humjia kwa namna yake kwani kila mtu amepitia njia yake kufika hapo alipo bali ni kutaka kukuuliza juu ya unachotufunza mbali na uimbaji wako mzuri.
Hakuna shaka juu ya uimbaji wako , sauti ivutiayo huku ukiwa umejichagulia aina ya muziki ambayo ni ngumu kukubalika (kwa kuwa si nyimbo za kuchezeka sana) lakini nyimbo zake hudumu kwa kipindi kirefu.
Nilikuwa shabiki wa muziki wako tangu umeimba wimbo ambao si wewe ama uongozi wako wa mwanzo hupenda kuutambulisha kama ulikuwa wako.Ilikuwa Sio fine ile ya kwanza si ile uliyoirudia.Ukaja wimbo ulioimba na Bob Juniour kama sijakosea ikafuata Sio fine ambayo wengi waliisikia na baadaye jichunge.
Kijana ulivuka vikwazo na kupanda ngazi ukiwa na usiamamizi wa mtu mmoja makini Sandu George ambaye alipekea kufikia mafanikio makubwa ya kuchukua tunzo ya mwanamuziki bora chupukizi huku wimbo wa Siachani na wewe ukiweka rekdi kadhaa kwenye muziki wako.
Baadaye ukaja kutoa moja kati ya nyimbo bora zilizovuma bila video, 'Nnivumilie' ukimshirikisha mkali mwingine wa muda huo Rubby.
Mara ukabadilisha wasimamizi wa kazi zako, kitu hicho kikakufanya usitoe kabisa video ya wimbo ule ambayo kwa ukubwa wake wengi tuliamini ingekuwa ni moja ya ngazi yako kufika juu zaidi.
Ulikoenda ukatoa 'Siwezi' , wimbo uliozidi kukuweka juu na kukupa michongo ya maana kufikia ROCKSTAR 4000 kukuona na kukusaini.
Hapo pia ukatoa wimbo usiochosha ukumshirikisha mwanamuziki ambaye ulikuwa na ndoto za kuja kuimba naye.Lakini licha ya kufanya nyimbo hizo chache na kufahamika ndani na nje ya Afrika Mashariki pia uimbaji wako uliwavuta wengi na kukufanya ushirikishwe na wanamuziki wengi sana.
Kushirikishwa kwenye nyimbo kulizidi kukuweka kwenye masikio ya wapenzi wengi wa muziki lakini baada ya uhamia ROCKSTAR 4000 kukatokea suala la kutofanya video ya wimbo, safari hii ni wimbo ulioshirikishwa.
Wimvo ambao uiuimba vyema kabisa, ukishirikishwa na Suma Manazareti baadaye ukaja kudai ni mambo ya mkataba.Najiuliza ni mikataba gani hiyo ambayo huzuia kufanya kazi ambazo ulizianza kwenye mikataba ya nyuma.Huonimkama unakosea yaani kila ukihama unaacha viporo?
Huoni kama unaziba njia za baraka zinazofunguka baada ya kuwaumiza hao ambao ulianza nao hizo 'project'?
Unawafunza nini wanamuziki wachanga ?
Kwamaba wasiingie mikataba?
Ama wagande walipo kwa kuhofia kuja kugombana na wenzao kwa kuwavunja moyo kisa mikataba mipya?
Kwa bahati mbaya licha ya kipaji kikubwa cha uimbaji na kutunga ulichojaliwa una mkosi ama niseme bahati mbaya kama waswahili tusemavyo wa kushindwa kuwasiliana vyema pale unapoona jambo lipo tofauti.
Nakumbuka ulivyomjibu Stan Bakora, nakumbuka ulivyomwakia Eric Omond hii yote itajenga picha kuwa huna busara na unadharau tafuta namna bora ya kutuliza hasira kwani bado una safari ndefu ya maisha na ya muziki.
Nisiseme mengi leo ila naamini utaangalia na kuyafanyia kazi niliyokueleza, usipoyafanyia kazi nayo si vibaya ni namna uliyoamua kuishi.
Mie siyo bora sana , lakini nakuuuliza Baraka.....
Tujifunze nini kutoka kwako?

0 comments:

Post a Comment