ads

Sunday, 5 February 2017

JESHI LIMESHATEKWA,VITA HAKUNA TENA

Na.Mwanakalamu.
Wiki chache zilizopita ilisambaa video mitandaoni ikionesha tendo la aibu ikimwonesha mtoto mmoja ambaye alikuwa akifanyiwa ama tusema akifanya ngono.Ilikuwa ni video ambayo kama tusingekuwa na unafiki ingepotea na kufutika kabla haijafika mbali.Ingekuwa kipindi cha mtoto wa mwenzio ni wako video ile isingepata nguvu hata leo mie kuiongelea.Sikujisumbua kuisaka ile video ya aibu kwani najihisi bado nipo katika zama za mtoto wa mwenzio ni wako, zama ambazo wengi wetu tulizitupa mara tuu tulipopata simu za kupangusa, simu janja zitufanyazo tuwe karibu zaidi na dunia ya kwanza.
Ilisemwa na kujadiliwa kwenye mitandao ya kijamii wengi wakimhusisha binti aliyekuwa akioneakana kwenye video ile na binti wa mwigizaji mmoja maarufu nchini hivyo kuzua mabishano ya kinafiki wengi wakibisha kutaka kuthibitisha na si kule kubisha kuwa 'siye' wakimaanisha.
Nikiwa mmoja wa wafuatiliaji wa 'forum' maarufu nchini niliufuatilia mjadala ule ambao ulikuwa wa ''Mwenye hiyo video anitumie'' na si kutatua shida ile iliyoikumba familia ile , sijui kwa kusingiziwa ama ukweli.Kuna wachangiaji walioenda mbali wakidai malezi ya yule mtoto anayefananishwa naye yamesababisha ahusishwe kwenye kashfa hiyo nzito, hao waliwalaumu wazazi wake kuwa chanzo cha yote.
Wengine walidai ilikuwa ni video ya muda zaidi na ilishasambaa kabla ya hapo , lakini kuna wengine huko instagram waliwataka watu kuwatumia shilingi 1500/= ili watumiwe hiyo video.
Nilijikuta nazidi kuelewa tulipofika,nikaelewa tulivyo tu wema na wastaarabu mbele ya watujuao lakini kinyume cha hapo tunaonesha maana halisi ya tabia zetu.
Mtu anafurahia kuisambaza hata kwa kuiuza video chafu ya binti wa watu ambaye hata iwe kwa hiari yake ama kwa lazima hakuna uhalali wa kusabazwa bicha hiyo kwa maadili natamaduni zetu zitakavyo.Lakini kuna mtu kwa kutumia utambulisho feki kwamba hatofahamika pia yupo radhi kutoa pesa kupata video chafu.
Je, angekutana na picha ya dada yake, mama yake ujanani,bintiye ama hata mke wake utotoni atafanya nini?
Lakini kwa kuwa na hakika huyo ni mama wa mwingine baadaye, mke wa mwingine baadaye ama dada na binti wa mwingine, atatigwa kuipakua na kuisambaza kwa nguvu zote.
Ile vita inayotangazwa juu ya mazoea mabovu kama hayo ya kusambaza picha chafu ni ya kwenye vitabu na nakala za serikali tuu na si serikali.Serikali iundwayo na watu , watu wenye mawazo machafu kama hayo yasiyo na soni nyuma ya kamera ama macho ya wengine haipo tena, atapigana nani wakati wanajeshi wake ambao ni watu hawapambani nayo bali wameshakuwa mateka na watumwa wakubwa wafurahiao utumwa wao?
Leo kila mmoja anaamua namna ya kumlea mwanaye akiaswa anadai ni wake msimwingilie, leo kuna majasiri wa kumbaka kwa lazima ama ushawishi na kumrekodi ama kumpiga picha na kuzisambaza mitandaoni na kupata umaarufu kwa kuisambaza picha hizo zikafika mbali na kuharibu ule ubinadamu tuliokuwa nao mwanzo.
Leo vyombo vya habari vimekuwa chanzo cha kuyapeleka mbali mambo hayo na leo nimeshtuka kituo kile kile kimelizua lingine kumuhusu mwigizaji.Watashangiliwa kwa sababu hakuna anayepambana wanajeshi wamekuwa mateka , hakuna vita tena.
Sijui hao watangazaji ama wasambazaji wa hizo video wakikutana na picha za mama zao, wake zao ama wadogo na dada zao watafanya nini, bahati mbaya ni wanawake wachache sana ambao wanapambana ingawa ni waathirika wakubwa wa jambo hilo.
Wamekuwa waoga kwani hawaamini kuwa wapenzi wao hawajawahi kuwapga picha hizo na zipo kwenye simu hivyo watakuwa kimya ma kujifanya kupambana kwa kuhofu kutokuwa salama.
Wanaume nao wamekuwa MAPUNGUANI hawaambiliki hadi watapokutana tupu za mama zao (Ashakum si matusi) akili zitawakaa sawa.

Wanajeshi watekwa vita hakuna tena.

0 comments:

Post a Comment