ads

Sunday 5 February 2017

KWA MEDA CLASSIC



Nianze kwa pongezi kwa hatua hii uliyofikia, wimbo mzuri kuanzia, tune , mashairi na video safi kabisa.Najua ni safari ndefu hadi kufika ulipo naiona video ipo #21 trending youtube si kitu kidogo ni hatua kubwa sana.
Najua wengi watahisi ni mwanamuziki mpya kwa ukubwa wa wimbo huu ulivyo kumbe ni safari ngumu yenye vilima tambarare na mashimo lukuki.Nilikusikia kwa mara ya kwanza ulipoimba wimbo wa "Barua kwa Diamond" (huenda haukua wimbo wako wa kwanza) , nilikiona kipaji chako nikatamani kusikia ukitoa wimbo mwingine ukipita njia zako yaani mbali kabisa na uimbaji wa Diamond ambao wengi walihisi huwezi kuimba zaidi ya hapo.
Nikaja kusikia ngoma mbalimbali kama Kongoi,somebody Alele, Salary,hadi Tiffah.Niseme ukweli wimbo wa Tiffah uliniboa, si kwamba ulikuwa mbaya ama nilimchukia Tiffah hapana ni kwa sababu niliona ukirejea kule ambako ulikwisha vuka kule kufanywa kama shabiki tuu wa Diamond wakati nyimbo zako kadhaa zilishaanza kukutambulisha kama Meda Classic mwenye kipaji kikubwa sana.
Nilikuja kukusikia ukihojiws kwenye kipindi kimoja EATV , ulikuwa ukitambulisha wimbo , nikaja kujua kuwa mliwahi " kuhustle" na Harmonize hivyo ulifurahia mafanikio yake. Hapo nafsi ilifarijika na kukuona una malengo ya kufika kule walikofika wengi kwani kwako nilikiona kipaji kikubwa zaidi ya wengi waliofika mbali. 
Nikasubiri ngoma kali , ukashirikishwa na Nas nikajua waja .
Ukaja nivunja moyo ulipotoa Kokoro remix nikadhani unataka tena kurudi nyuma , niseme ukweli nilivunjwa moyo kuona kipaji chako ukikificha licha ya kuwa uliiimba vyema hiyo kokoro remix lakini nilijua utaja puuzwa tuu huku unacho kipaji cha kuimba na kutunga.
Lakini sikuchoka nikaandika hadi makala kwenye blog ya Kalamu Yangu yenye kichwa hiki kikeracho "Meda Classic achana na Diamond fanya yako" sikuwa na hakika kama utapata ujumbe ila kwa kuwa wote tuna marafiki Iringa basi ungekufikia hata kwa kuchelewa.
Nikiwa nimekata tamaa juu ya kipaji chako kupotea nikakutana na taarifa ya wimbo wako kwa Millard kilichonikera hata mwandishi alikutambulisha kama ' Aliyeimba barua kwa Diamond' ila nikajua huo ulikuwa mwisho wa kuitwa hivyo utaitwa Meda Classic ,Meda wa Sidhani na ngoma nyingine kali kabla ya kuwa Meda ambaye kila mtu atamfahamu kama mwanamuziki mwenye hitsongs za kumwaga.

Hongera Meda classic usirudi nyuma , najua nitatoa hiyo link ya sidhani kwenye bio yangu na kuuweka wimbo wako mwingine mpya mzuri kuliko sidhani.

0 comments:

Post a Comment