ads

Friday 31 March 2017

J MOE ANAPORUDISHA FIKRA ZETU NYUMA

Na:Steven Mwakyusa(Mtu Makini)

"SamahaƱi kama nimekukwaza baba lake
Ila ukweli ukubalike..
Mi analogy siyo social network
Nyie instagram ndo imefanya muwike.."


Hii ni moja ya mistari ya J moe katika ngoma yake ya "nisaidie kushare"...
Hii mistari imenirudisha nyuma kipindi cha analogy, ambapo sisi wapenzi wa muziki ilikuwa shughuli pevu kuzipata nyimbo za wasanii!!
Bila kutega masikio redioni ilikuwa ngumu sana kupata chochote, radio kama RFA, Kiss FM na Radio one zilipata umaarufu karibia nchi nzima. Vipindi kama Showtime, DJ show, African Beats, Weekend show na Weekend fever ilikuwa ni dhambi kubwa sana kuvikosa!!
Madj na watangazaji maarufu kwa kipindi hicho walitoa burudani ya uhakika wakiwemo akina Kid Bway, Fred Waa, Lazaro Matarange,  Glory Robinson, Abubakari Sadick kwa fujo, Soggy Dogy, Dj Venture, Dj Ommy na wengine walifanya muziki kuwa na ladha ya kipekee...
Kwa mwanzoni kupata nyimbo mpya ilikuwa mpaka unyonye redioni, hapa ilikuwa mpaka utegee usiku ndipo unapata quality ya kueleweka ambayo haina matangazo. Kwahiyo kukaa na radio mpaka saa 7 usiku show zinapoisha ilikuwa kawaida sana ili angalau usumbue watu mchana!
Mbali na kunyonya redioni option iliyokuwepo ni ya kusubiri albums, hapa ndipo ushabiki wa kweli ulipokuwa unaonekana na si hizi kelele za social networks, albums kama Funga Kazi, Ulimwengu ndo mama, historia ya kweli, Nini chanzo, Kima cha chini, Machozi jasho na damu na Jasho la Mnyonge ziliuza copy kila kona ya nchi!!
Kwa wale wasanii waliokuwa wakitoa wimbo mmoja mmoja, nao tuliwapata kwenye compilation albums, albums kama "Kali za bongo" zikiwa na vol 1, vol 2 na kuendelea zilifanya ladha ya muziki kuwa ya kipekee kabisa!! Hizi compilation nazo zilikuwa zikisubiriwa kwa hamu na walio wengi!!
Baadaye zikaanza kuja cd, na habari za kuburn nyimbo ikashika chatt, hivyo basi kuwa na cd yenye nyimbo mpaka 15 ndiyo ulikuwa ujanja! Baadaye zikaja flash na na baadaye zaidi zikaibuka hizi social networks, taratibu umaarufu wa radio na watangazaji ukaanza kushuka chini, kinachoitwa albums kikapotea kabisa, kuapatikana nyimbo ikawa rahisi zaidi huku ikiacha pigo kwa wasambazaji wa albums kama akina MAMU na wengine!
Hivyo J moe anaposema yeye ni analogy yupo sahihi, analogy ilikuwa analogy kweli..ushindani ulikuwa katika mashairi, uwezo wa kuflow na beats kali, lakini sasa watu wanakaa kusifia videos, ule ubunifu kama wa Ndiyo Mzee, Kibanda cha Simu, Mvua na Jua, Vina Utata na Mayowe haupo tena!!
Ushindani umehamia kwenye viewers youtube na followers Insta, ubunifu uko kwenye photoshoot na si vinginevyo! Hakuna namna ni nyakati tu ndizo zinazoamua, ila I wish ule ushindani urudi tena, hakika ulifanya muziki kuwa wa namna yake!!

0 comments:

Post a Comment