ads

Thursday, 6 April 2017

TANZANIA VS KENYA, MUZIKI ULITUUNGANISHA ZAIDI!!

Na.Steven Mwakyusa (Mtu Makini)

Kwenye miaka ya 2000 baada ya muziki wa bongo flava kushika chatt hapa nyumbani, baada ya muziki wa dansi kula mweleka kulitokea muingiliano mkubwa kati ya muziki wa Tz(Bongo Flava) na muziki wa Kenya(genge). 

Muingiliano ulikuwa mkubwa na ilikuwa kawaida kwa wasanii wa kenya kuja kufanya ngoma tz, au kushirikishwa na wasanii wa hapa nyumbani! Pia wasanii wa hapa nyumbani waliweza kuvuka mpaka na kufanya kazi kenya na kutengeneza ladha ya kipekee kabisa!!

Mwanzoni walianza Majizee ambao walifanya collabo na Solo thang Ulamaa wimbo ukienda kwa jina la Semeni! Collabo hazikuishia kwenye Semeni ya Majizee peke yake, K South nao walifanikiwa kufanya kazi na Juma Nature, ngoma ikienda kwa jina la 'Tunafanya kazi"...

Ikionekana kabisa kuvuka kwao mpaka kuliumiza vichwa vya wengi, Msanii Bw. Misosi katika Nitoke vipi alihoji kuhusu ujio wa K South hapa nchini, namnukuu "K south toka Kenya hivi ni wasanii, sidhani kama wamekuja kwa sanaa bali utalii!

Bamboo naye hakuwa nyuma, huyu alifanya poa katika "mambo sawa" kazi ambayo alimshirikisha Prof J. Baada ya mambo sawa, bamboo alifanya kazi nyingine ikienda kwa jina la "Kabinti" huku akitumia beat ya "Alifu kwa ujiti" ya Fatma na Jos Mtambo! Na alipoulizwa kuhusu hiyo beat alijibu kwamba kaiokota!!

Naaziz wa Necessary Noise naye alishirikishwa katika wimbo wa TID, watasema sana huku Nyota ndogo yeye akishirikiana na Mr Blue katika kibao cha Mpenzi!

Q chief pia aliweza kufanya vibao kadhaa akiwashirikisha Noonini pia kuna kibao aliimba na Nyota Ndogo

Pia kulitokea collabo moja matata toka Bongo records, wimbo uliitwa Bongo Records...humo ndani kulikuwa na Wyre, Naaziz, Solo thang, TID na J moe to mention few!

Studios/producers wa Kenya kama Ogopa Deejays walipata umaarufu mkubwa hapa nyumbani!

Wasanii kama Aman na Prezoo waliweza kujipenyeza katika soko la hapa nyumbani, huku wasanii kama Noorah, Ay, Mwanafa nao wakiweza kufanya kazi mbali mbali nchini Kenya!

Lakini ni kipi kiliua huu ushirikiano? Je ni muziki upo juu zaidi katika ya muziki wa Tz na wa Kikenya? Je unafikiri zile zama zinaweza tena kujirudia?

1 comments:

  1. Muziki wa Tanzania upo juu kuliko wa Kenya kwa sababu utumiaji wa lugha ya kiswahili kwa Jambo kitu
    Kilichouwa ushirikiano wa Kenya na Tanzania kimuziki Aina tofauti ya muziki bande zote wanaimba

    ReplyDelete