ads

Thursday, 20 April 2017

DAZ NUNDAZ FAMILY; KUNDI LILILOONDOKA NA LADHA YAKE KATIKA BONGO FLAVA!!


Na.Steven Mwakyusa (Mtu Makini)
Daz Nundaz Family ni moja ya kundi ambalo lilipata umaarufu mkubwa sana miaka ya 2000, kundi lilikuwa likiundwa na Feruz, Sajo, La Rhumba, Daz Mwalimu na Critic!!

DNF walifanikiwa kufahamika masikioni mwa wengi na kibao chao cha kamanda ambao kilirekodiwa Fm studio chini  ya producer mahiri wa kipindi hicho akijulikana kama Mika Mwamba!!

Baadaye DNF walitamba na kibao cha Barua na hatimaye wakafanikiwa kuzindua album yao waliyoiita Kamanda ambayo walikuja kuizundua tarehe 25 ya mwezi May mwaka 2002!!

Album ilisheheni vibao vingine kama Nitafanya, Matatizo, Maji ya Shingo (og na rmx)na Shuka Rhymes...

Uzinduzi wa DNF ulipamba na wasanii waliokuwa wanatamba kwa kipindi hicho wakiwemo HBC (Niamini), Waswahili(kila mtu na starehe yake), wagosi(kero), Mwanafa(showtime), Wachuja nafaka (Mzee wa busara), Gk (Sister sister), Afande Sele (Mayowe).

Baada ya Album ya Kamanda Feroz na Daz Baba walifanikiwa kuja na album zao kama Solo Artist na waliweza kuteka mashabiki lukuki, wengine waliobakia walishindwa kifurukuta kabisa huku Critic akiishia kutoa kibao chake cha Mnizoee!

Baadaye DNF kama kundi walifanikiwa kutoa vibao kama Jahazi na Kwenye line, baada ya hapo Feruz na wenzake walitoa kibao kikiitwa Kijana Mteja ikisemekana walimuimba  mwenzao Daz Baba ambaye alitopea kwenye madawa ya kulevya!

Hivyo basi DNF inaendelea kuwa moja ya kundi lililokuja na ladha ya kipekee katika Bongo flava huku nyimbo nyingi zikiwa za majonzi, Mfano Kamanda ilishindwa kurekodiwa mwanzoni katika studio za Bongo Records kwa madai kwamva eti P alisema yeye harekodi Kwaya, hii ndiyo sababu iliyowapeleka fm studio..Bongo Records walirudi baadaye baada ya kusikika na vibao kadhaa!

NB; Kwa upande wangu my favourite tracks toka kwa DNF ni pamoja na Nitafanya, Matatizo, Jahazi na Kwenye line! Je wewe ni vibao gani ambavyo bado unavikumbuka toka kwa wakali hawa wa DNF?

0 comments:

Post a Comment