Na.Steven Mwakyusa (Mtu Makini)
Baada ya kufanya vizuri ndani ya kundi la Daz Nundaz... Ferooz aliibuka na project ya peke yake alouokwenda kuiita Starehe!
Starehe ndiyo wimbo ambao ulimuweka katika chart za juu kwa wakati huo, huu maudhui yakiwa ni mtu ambaye aliendekeza starehe na hatimaye kuishia kuugua maradhi yanauohusiana na AIDs. Katika Starehe alikuwemo nguli mwingine wa wakati huo akijulikana kama Prof J. Uzinduzi wa Starehe ulianzia jijini Dsm na baadaye album ikaenda kutambulishwa katika jiji la Bujumbura, november 4 ya mwaka huo huo 2004 ilikuwa zamu ya Zanzibar katika ukumbi wa Ngome kongwe!
Itoshe tu kusema Starehe ni moja ya nyimbo kubwa kupata kitokea katika muziki ya Bongo Fleva, hii ni kuanzia mashairi/ujumbe, mpangilio wa sauti na uwezo wa kughani achilia mbali production ya P funk Majani!!
Vibao vingine vilivyopata umaarufu ilikuwamo Boss aliyoimba na Solo Thang pia Juma Nature, Jirushe Part 2 aliyofanya na J moe pia ilitosha kumweka katika chart za juu pia!!
Vibao vingine vilikuwa pamoja na Njoo, Jahazi, Jirushe Part 1 ft Scout Jentaz pia Safari!
0 comments:
Post a Comment