Na.Steven Mwakyusa (Mtu Makini)
Baada ya Feruz kufanya poa na kufanikiwa kuachia album yake aliyoiita Safari, Ilifata zamu ya mkali mwingine katika DNF akiitwa Daz Mwalimu ambaye baadaye alikuja kujiita Daz Baba!!
Kibao cha mwanzoni kabisa kumtambulisha kama solo artist kiliitwa Wife akiwa na Ngwea, Baadaye Daz Baba alisikika katika Namba 8 akiwa na Fid Q na Baadaye katika Nipe 5 akiwa na wasanii wenzake wa Daz Nundaz...
Kama ilivyokuwa Wife na Namba 8, Nipe 5 iliweza kushika chart za juu kabisa katika muziki na hii ikamwezesha kuingiza sokoni album yake aliyoiita Elimu Dunia, Elimu dunia ilikuwa jina la album pia jina la wimbo ambao aliwashirikisha Afande Sele pamoja na Feruz!
Albamu hii pia ilisheheni vibao kama Usiku huu ft Mr Blue, Rastaman, Mwalimu, Unavyofanya, Raia na usinihukumu!
Pia Daz Baba alipata kushirikishwa katika vibao vingi maarufu kwa wakati huo vikiwamo Niko Busy ya Jaffarai na Huyu Jamaa ya Boni Crew pia Kulwa na Dotto ya Soggy Dogy Hunter!
Itoshe tu kusema hii ni moja kati ya album bora kupata kutokea kwenye muziki wetu huku ikisheheni nyimbo zenye mafunzo makubwa katika jamii, kuanzia elimu dunia, usihukumu, mwalimu, rastaman, usihukumu, unavyofanya hata na ile wife bado ni applicable kwa sisi tunaoandamwa kila siku kuhusu kuoa.
Huyu Daz Baba 2004 alituambia ashakuwa mtu mzima..na anahitaji wife, sijui alishapata?
NB; My favourite tracks toka kwenye elimu dunia ni Wife, Nipe 5, Unavyofanya na Elimu dunia!!
Elimu dunia Album ( Tracklist)
1. Elimu dunia(ft Afande Sele & Feruzi)
2. Namba 8 (Feat Fid Q)
3. Usihukumu
4. Raia
5. Unavyofanya
6. Rastaman
7. Usiku huu(ft Mr Blue & Critic)
8. Wife(ft Ngwea)
9. Nipe 5 (ft Daz Nundaz)
10. Mwalimu
0 comments:
Post a Comment