ads

Tuesday 30 May 2017

PNC: MSANII ALIYESHINDWA KUFURUKUTA MBELE YA COLLABO

Na. Mtu Makini
Mara nyingi collabo baina ya wasanii huwa inanuia kutengeneza kitu kilicho bora zaidi, ikiwa ni matokeo ya kuchanganya ladha tofauti za muziki, Hivyo msanii wa RnB anaweza fanya kazi na mtu wa Rap, Mtu wa pop anaweza fanya na mtu wa hiphop au kinyume chake! Mtu wa dansi/zilipendwa anaweza fanya na mtu wa muziki wa kisasa na ukatoka muziki bora kabisa!!

Kuna kundi la pili la wasanii wanaoitwa underground na wengine ni underground wakongwe, ambao wao huwa wanaona hawawezi fanikiwa bila kuimba na wasanii wakubwa! Hawa huwa wanavizia wasanii wanaokuwa kwenye peak kwa kipindi husika huku wakitegemea kusafiria nyota husika! Hili linaweza kuwa msaada kwa nyakati fulani na linaweza kuboost kazi za msanii husika, mathalani msanii anayejiita Nuh Mziwanda aliweza kuitumia vizuri peak aliyekuwepo AK na kufanya kazi yake ya Jike Shupa kutrend kwa kiasi kikubwa kulinganisha na kazi zake za nyuma!!
Tukirudi kwenye mada, PNC ni msanii toka jijini Mwanza ambaye miaka ya 2000 alisikika masikioni mwa wengi na kibao chake cha MAMA, kibao hiki kiliweza kutrend kulingana na maudhui ya kile alichoimba huku ikionekana kugusa watu wengi waliopoteza mama zao!
Baada ya hapo PNC alihamia jijini Dsm na ndipo akaingia kwenye mkumbo wa collabo kila alipoona inafaa! Hizi ni baadhi ya collabo alizofanya na wasanii wakubwa lakini bado zikashindwa kumfikisha kule alikotaka kufika, huyu mimi naweza kumuita underground mkongwe maana amedumu kwenye game kwa zaidi ya muongo mmoja!!
1. Mbona Feat Mr Blue, hii kazi ilifanyika Mj Records kipindi Mr Blue akiwa kwenye chart za juu! Mbona inabaki kuwa moja ya kazi nzuri toka kwa PNC
2. Mammy Feat Alikiba-Ak kipindi anasumbua na vibao vyake kama Cinderella, Nakshi nakshi na nyinginezo, PNC hakumuacha apite hivi hivi. Walifanya kazi na KGT wakaiita Mamy ila mapokeo yakawa ya kawaida tu!
3. Kwanini Feat Bushoke-Peak ya Bushoke pia haikuachwa na PNC yeye kwake ilikuwa ni fursa, kazi ilifanyika na baada ya hapo ikawa kama nyimbo nyingine tu, ya kawaida!
4. Naumia Feat CheleaMan-Hiki kilikuwa kipindi ambacho Chelea Man alisumbua na kibao chake cha Msela/Nipende kama nilivyo, Ni chelea man ambaye alishirikishwa katika vibao kadhaa vya Mb Dog kikiwemo kile maarufu kabisa cha mapenzi kitu gani! PNC hii kwake ilikuwa fursa ambayo bado haikufua dafu
5. Swaga ft Nay Wa mitego- Huu ni wimbo ambao PNC alionesha hasa ufundi wake wa kuimba na kama kukaza alikaza haswa kama ambavyo anasema katika moja ya mistari " Hapa ni swaga tu, nazidi kaza tu"...
Humo ndani ukichanganya na Sauti ya Nay ilitosha kuufanya huo wimbo usumbue lakini haikuwa hivyo!
6. You're the only one Feat Prof J & Chid Benz-Kama haitoshi huku akiwa anatafuta namna ya kutoka, katika kibao hiki alienda kuwakutanisha wakali wawili wa kufoka foka Prof Jize wa mituringa huku pembeni akiwepo King kong mzee wa vina vya kama! Ur the only one ilkuwa the best ila bado haikutosha kuliteka soko la muziki!
Ni PNC aliyekuja kuimba Imebuma akiwa peke yake, ambayo angalau haikubuma! PNC akiwa peke yake aliimba Aiyolela ambayo angalau iliweza kupenya masikioni mwa wengi!
Pia siku za karibuni katoa kibao kakiita Nyota ambacho kinaendelea kufanya vizuri!!
Kimsingi kwa case ya collabo kwa PNC zimefeli, huyu inabidi akomae mwenyewe tu. Mimi nina imani kuna siku umma utamuelewa nini anafanya!!

0 comments:

Post a Comment