ads

Thursday, 1 June 2017

NDIYO ALIKUWA MWIZI NA MSHENZI SANA


‘’Alikuwa mwizi sana shuleni na mtaani’’
‘’Yule alikuwa mzinzi sana’’
Ndiyo tusemavyo na kuwadharau watu wenye historia hizo zisizovutia, huku tukijisifia kuwa tulikuwa watu waliokuwa na mienendo sahihi.

Je, hao wezi, washenzi na wazinzi wapo wapo sasa, wanafanya nini,?
Je, hao wenzetu bado wana tabia hizo?
Sisi Je? Tupo wapi tulikuwa wema kweli ama tulifanya kwa siri na hakuna ‘msala’ uliotuumbua na kuonesha mapungufu yetu?
Naomba nikuambie rafiki na ndugu yangu, haijalishi historia yako ni aibu kwa kiwango gani , cha msingi na cha maana leo hii upo wapi unafanya nini.Kama bado unapata uoga kwa historia yako mbya ya wizi, uzinzi ama utoaji mimba (uliojulikana kwa wengi na uliokuwa siri) anza maisha mapya ambayo yatakuwa na historia njema baadaye.
Kwa utafiti usio rasmi nilioufanya wengi wa wale ambao walikuwa na historia isiyovutia ni miongoni mwa watu waliopiga hatua katika maisha yao.Hii inanifanya nikuambie ndugu yangu , usiionee aibu historia yako isiyokuvutia bali tengeneza historia ambayo itakumbukwa na kufutwa na kwa historia yako isiyovutia ambayo inakuumiza leo.
Usiogope wakisema ulitoa mimba, uliacha shule, sijui ulipata sifuri, sijui ulikuwa mlevi kupindukia, ulipigana na mzazi wako, uliua , ukabaka.Hayo maneno hayatoibuka hadharani kama umefanikiwa kubalika na kujijenga kimaadili na kiuchumi zaidi itakuwa ikiwauma wasengenyaji na wasemaji kwani licha ya kuwa mashuuhuda wa matendo yako ya nyuma hawana cha kujivunia.
Sina la zaidi leo, nakuambia ndugu yangu, Uliteleza ukaanguka kwa bila kukusudia au kwa kukusudia. Simama yajenge maisha yako ili historia ya maisha yako iwe msingi wa vizazi vijavyo kutokata tama.
Mwanakalamu nawasilisha.
1 June 2017

0 comments:

Post a Comment