Na.Mwanakalamu.
Ni vigumu sana kalamu
yangu kuandika mambo yahusuyo siasa,si kwa kuwa hazina umuhimu bali nimejikuta
napenda sana kutumia kalamu yangu kuandika kuhusu fasihi ambayo
inajitosheleza.Siasa ni maisha , siasa ni haki,siasa ni imani, siasa ni uhai
kwa kifupi siasa ni kila kitu hivyo ina umuhimu mkubwa.
Kwenye dola yoyote kama
siasa hazipo sawa hivyo vitu nilivyovitaja hapo juu huwa mashakani.
Palipo na siasa mbovu,
vita hutokea,njaa huja, dini hazistawi, umoja, mshikamano na udugu havina
nafasi na umasikini hutamalaki.Siasa safi ni moja kati ya nguzo za maendeleo ya
jamii yoyote , hivyo siasa ni muhimu sana kwa maisha ya kila binadamu na kila
mmoja anayo nafasi ya kuhakikisha jamii yake inaogelea kwenye siasa safi kwa
ustawi wa jamii yake.
Baada ya kueleza kwa
kifupi juu ya umuhimu wa siasa safi katika jamii yoyote, nirejee kwenye kile
ambacho kimenifanya nishike kalamu yangu leo.Siku chache zilizopita
nimeshtushwa kumsikia Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Upinzani nchini Ndugu F.A.
Mbowe kuwa anatamuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya katika uchaguzi unaotarajiwa nchini
humo.Alienda mbali na kueleza sababu za kumuunga mkono Rais huyo Kenyatta kuwa
ni moja kati ya mfano wa viongozi wa kidemokrasia aliyeruhusu uhuru wa kisiasa
kupitia bunge na mikutano mingine ya kisiasa.
Lakini kwa taarifa nyingine ambazo nimezisikia kutoka kwenye
vyanzo vyangu vya kuaminika sababu hiyo imekuja baada ya urafiki wa Rais wa
Tanzania na mpinzani mkuu wa Rais Kenyatta katika uchaguzi huo ndugu Raila
Odinga.Urafiki huo umetafsiriwa kama msimamo wa Chama cha Mapinduzi.
Hiii imenitia shaka
kwani siku chache baada ya msimamo huo wa Chama kikuu cha Upinzani nchini
kupitia Mwenyekiti wake, ilitoka ripoti kutoka shirika moja la kimataifa juu ya
ukwiukwaji mkubwa wa haki za waandishi wa habari nchini humo, uliohusisha
kupigwa na kuumizwa kwa waandishi wa habari.Taarifa ilidokeza kuwa ‘mabloga 20’
wamepigwa na kuteswa kutokana na kuandika habari zinazokosoa utawala.
Si hivyo tuu miezi kadhaa
iliyopita , kumekuwa na matukio ya kuuawa na kupotea kwa wanasheria
yaliyofuatiwa na mgomo mkuwa wa madaktari nchini humo , matukio ambayo Serikali
ya Rais Kenyatta imekuwa ikinyoshewa vidole.
Na baadaye serikali
imekuwa ikipinga vyama kuwa na vituo vya kujumlisha matokeo kitu ambacho chama
chetu cha upinzani nchini kinaamini na kutuaminisha watanzania ni moja ya
sababu ya kukosa ushindi kwenye uchaguzi mkuu uliopita.
Je, CHADEMA haioni kama
inamuunga mkono mtu ambaye anafanya kitu ambacho hata nchini inapigania
kisiwepo?
Au ni lazima kupingana
na kile ambacho Rais Magufuli anaoneka akukipenda?
Haioni kama kumuunga
mkono mmoja wa wagombea Urais tena kwa tamko Rasmi la Chama kutaleta mngongano
wa kidiplomasia kama upande iliouchagua ukashinda?
Na Je, haioni umuhimu
wa kuaachia Wakenya wamchague Rais wao , na kusubiri kumpongeza mshindi
aliyeshinda kwa haki?
Kwa upande wa Chama Cha
Mapinduzi, licha ya kutokuwa na tamko Rasmi laChama imekuwa ikisemwa huku na kule mitandaoni kuwa
wanamuunga mkono Mgombea wa Upinzani Ndugu Raila Odinga kwa kuwa tu ana urafiki wa muda mrefu na
Mweyekiti wa chama chao ambaye ni Rais wa Jamuhuri.
Nao hawaoni si sahihi
kuwaachia Wakenya waamue na kumpongeza Mshindi?
Hawaoni kama wanaharibu
diplomasia ya nchi zetu kama wampingae
akashinda Urais?
Kupitia Kalamu Yangu
nashauri CHADEMA na CCM kusubiri kuwapongeza washindi.
Alamsik.
0 comments:
Post a Comment