ads

Sunday, 23 July 2017

BILLBOARD CHART NA UBORA WA MUZIKI

 Na. Steven Mwakyusa (Mtu Makini)
"Billboard chart" mpaka sasa ndiyo chati ya muziki inayoheshimika zaidi duniani! Historia yake inaanzia January 4 ya mwaka 1936, ambapo jarida la Billboard lilichapisha kwa mara ya kwanza chati ya muziki wakiita "hit parade"...

Chati rasmi ya muziki kwa maana ya "Billboard Top 100" ilianza mwaka 1958. Kwa miaka mingi wasanii wamekuwa wakipigania kushika chati katika chati hizi! Hivyo basi inapaswa kusema Billboard imekuwa kielelezo cha mafanikio ya msanii husika!
Pamoja na kuibuka kwa chati nyinginezo kama Uk top 40 na American Top 40 bado BB imeendelea kuwa kioo cha rank za muziki duniani!
Rekodi mbali mbali zimewahi vunjwa za kukaa namba moja kwa muda mrefu, hii ni toka kipindi cha akina Pink Froyd, Adam Brayans, Boys II Men, Whitney Houston, Mariah Carey, Toni Braxton, R Kelly, Nelly, 50 cent mpaka akina Ed Sheraan wa sasa!
Mabadiliko makubwa yametokea kwa miaka ya karibuni, huku muziki wa RnB na Hip hop ukipigwa mweleka mkubwa na muziki wa Pop, hata ukiangalia chart za karibun ni 60-80 zinajaa nyimbo za aina hii, hii inesababisha wasanii wengi kubadilisha gia angani wakiwemo akina Rihanna, Jason Derulo, Drake, Justin Timberlake nikitaja kwa uchache!!
Wimbo wa Despacito wa Luis Fonsi ambao mpaka sasa unashika namba 1 katika Billboard top 100 umeshaangaliwa mara 2.75billion huko Youtube!! Despacito mpaka sasa imeonekana kuipiku Shape of You ya Edd Sheeran ambayo imesumbua kwa miezi kadhaa!
Kilichotokea kwa Despacito ndicho mwaka jana(2016) kilikuwa kwa One Dance ya Drake akiwa na Kyla pamoja na Wizkid, pia Closer ya Chainskokers wakiwa na Halsey walimfuatia Drake kwa karibu!
Mwaka 2015 ulikuwa mwaka wa Wiz Khalifa na See you Again ambayo alimshirikisha Charlie Puth, pia Hellow ya Adele na Uptown Funk ni nyimbo zilizosikika duniani kote na kushika chart za juu katika BB!
Mwaka 2014 ulikuwa mwaka wa Pharell William na kibao chake cha Happy
Mwaka 2013 ulienda kwa Macklemore na Ryan Lewis wakimshirikisha Wanz na kibao chao cha Thrift Shop
2012 ulienda kwa Gotye akimshiriki Kimbra na kibao kikienda kwa jina Somebody That I Used To Know
2011 Adele alisumbua vilivyo na Rolling in the Deep
NB: Je ni lini nasi tutapeleka na sisi muziki wetu huko duniani? Maana mpaka sasa ndicho kielelezo pekee cha ubora na kupata kujulikana katika ulimwengu wa muziki!
Je ni lini nasi tutafikisha angalau viewers 100m youtube? Kipi kiongezwe katika muziki wetu na kipi kiondolewe?

0 comments:

Post a Comment