Tuesday, 25 July 2017

Hizi ndizo busara za Mfalme Suleiman

Na. Steven Mwakyusa (Mtu makini)

Mara nyingi huwa nikitaka kupata burudani ya Rhymes katika muziki wa bongo fleva, wazo la kwanza huwa linanijia kumsikiliza Afande Sele! Huyu jamaa alikuwa na namna yake ya uandishi yenye kufurahisha sana, alikuwa anaonya, anakemea, anajisifu, anajitukuza na akiamua kusifia anasifia japo ni mara chache sana!
Mayowe ndiyo track iliyomuweka kwenye ramani kama Solo artist japo alishaimba nyimbo nyingi tu akiwa na Sugu, huku kibao chake cha Afande Anasema kikiishia kwenye album ya Sugu(Milenia) kwani hakikupelekwa redioni!

Hili likawa moja ya chachu kwa Afande kuja kivyake na Mayowe, Mayowe ni wimbo ambao alimshirikisha Jay moe huku ukijaa majisifu maonyo na vijembe vya kila aina! Kama kuna mahali anasema
"Kelele za mashabiki, zisikuvimbishe kichwa ukajiona mwanamuziki, wakati madukani tape haziuziki" Afande anaenda mbele zaidi na kudai "nipo ndani ya meli ya fani , pamoja na dhoruba naamini meli itafika pwani" na mwishk akamaliza kwa kusema "kazi bila malipo, ni bora ushinde ndani na demu wako mcheze kidali poo"
Baada ya Mayowe Og pamoja na remix yake Afande Alisikika na Darubini kali akiwa na Dogo Ditto...Darubini kali ulikuwa mwanzo wa unabii mwingi katika game Afande anaanza kusema "Afande anasema, wote kimya na maneno yangu yatamgusa mwenye hekima"...hii ni kweli tupu, mara nyingi ukiwa na mtazamo tofauti, mwisho wa siku watakaokuelewa ni wenye hekima tu..
Afande aliongea mengi katika darubini kali, ambayo mengine yanaendelea kutokea mpaka sasa!
Baada ya hapo alikuja kusikika tena katika Mtazamo, ambayo aliwashirikisha wakali wengine wa kitambo Hicho Solo thang Ulamaa...pamoja na Prof J wa Mitulinga mti makavu....Mtazamo ulikuwa mtazamo kweli ukijaribu kuangazia mwenendo mzima wa game!! Afande alimaliza verse yake kwa kuwashukuru Solo na Jay akisema.."Asante Prof J, Majani na Ulamaa..mmegusa ninapopataka..nami kwenye mtazamo nina jambo nataka kuweka.."
Ni Afande Sele aliyesikika na Sana Tu, Nafsi ya Mtu, Usinichukie akiwa na Watu Pori...ila baadaye akaja kuwageuzia kibao na kuwaimbia kibao cha Heshima akiwa na Chelea Man, Heshima imejaa kila aina ya mafundisho na haikuwa tena kwa ajiri ya Koba na Ditto, Kuna wasanii wengi mpaka sasa wana kila sababu ya kusikiliza heshima ya Afande..."Kuna mahali anasisitiza "Bila Heshima unadhani utafika wapi mshikaji, hata usome kama mimi alafu uwe na kipaji"..akaendelea tena "wanaokusifu leo kesho watakuona kimeo, ukipoteza mwelekeo...."
Afande alisikika tena katika Karata Dume, humu alikuwa anazidi kudhihirisha maana ya ufalme, huki malalamiko makubwa yakiwa namna muziki unavyodhulumiwa, kuna mahali anasema "mambo hayajawa danga chee, msanii sitendewi haki deile, bei ya kuuza napangiwa, nikibisha narudishiwa mziki wangu unaibiwa, mwizi wangu namjua..."....
Haikutosha kwa afande sele kulalamika mwisho alichomeka kijembe kwa waliojaribu kuuza wenyewe "wangapi waliuza wenyewe mwishowe wakakwaa kisiki"
Afande akiwa na muendelezo wa majungu kama kawaida yake akaja akatangaza Kingdom, hii ilikuwa mahususi kumjibu Madee ambaye alionekana kumdiss Afande katika nyimbo zake zake, Jamaa alisikia akidai" unasema hiphop hailipi, Itakulipa vipi vip wakati unatukana waasisi, unatukana marasi alafu ujajiita rais..rais gani ana matusi, huna hata ofisi labda kwenu uwanja wa fisi..sio kwetu maras wazee wa peace"
Afande pia Katika Simba Dume anajaribu kujilinganisha na Simba za Simba huku wasanii wengine akiwalinganisha na Swala...huku akisisitiza yeye aonekani hovyo..Simba anaonekana anapoendakuimba na yeye anaonekana kwenda kwenye show...Afande kuna mahali anadai "Msanii hatulii nyumbani, ataandika nini zaidi ya story za chumbani?"
Pia Afande alisikika katika "Miaka 10 ya Ufalme" huku kikubwa akiwa anahoji wapi alipokosea..mbona yeye hana hela nyingi?? Akaenda mbali na kudai mwaka unaofuata na yeye atamuimbia sherri...
Huyu ndiye Afande Sele, kiukweli kaimva mengi sana! Ila mbali ya yote ngoma za mapenzi ni kama mbili tu, nawe wewe basi aliyoimba na Mr Nice na ile Mpenzi nipe ninachotaka...
Je kwako ni mistari gani unaielewa toka kwa Baba Tunda??

0 comments:

Post a Comment