ads
Showing posts with label Mazingira. Show all posts
Showing posts with label Mazingira. Show all posts

Sunday, 10 April 2016

YAJUE HAYA KUHUSU MILIMA

Na.Steven Mwakyusa

Ukiitazama sura ya dunia hasa nchi kavu utakutana na milima na mabonde, ipo milima ya aina mbalimbali kutokana na namna ilivyofanyika mpaka kufikia hapo ilipo!! Milima ni miinuko ambayo ina urefu kuanzia mita 600 toka usawa wa bahari!
#1 Milima iliyopo pwani ya Norway, Brazili, Australia, magharibi mwa India na kwingineko inakadiriwa kuwa na umri wa miaka 1000 mpaka 1200 million!
#2 Kuna aina kuu tatu za milima, milima ya volcano(volcanic mountains), milima mikunjo(fold mountains) na milima tofali(block mountains).
#3 Mlima Everest ndiyo mlima mrefu zaidi katika uso wa dunia kwa maana ya nchi kavu ukiwa na futi 29,028.Mlima Everest unapatikana katika mpaka wa Nepal na Tibet barani Asia!
#4 Mlima Kilimanjaro ni wa 10 kwa urefu duniani ukiwa na futi 19,317.
#5 Milima imekuwa chanzo cha kufanyika mvua kwa kulazimisha upepo wenye mvuke kupanda juu na baadaye kusababisha mvua nyingi katika upande unaopakana na bahari (Windward side), huku upande wa pili ( Leeward side ukipata mvua chache au kukosa kabisa.
#6 Safu ndefu zaidi za milima katika nchi kavu ni milima ya Andes yenye urefu unaofikia 7200 km, katika safu ndefu zaidi ni zile za Mid-Antlantic ridge zenye urefu wa 11,300 km.
#7 Mpaka mwaka 2011 iliaminika kuwa mlima mrefu katika mfumo wa jua ni mlima Olympus mons katika sayari ya Mars wenye urefu wa 21.9 km.
#8 Mlima Rheasilvia unaopatikana katika Vesta Astroid una urefu wa 23km ndiyo mlima mrefu zaidi mpaka sasa katika mfumo wa jua (solar system)
#9 Pamoja na kutokea kwa mmomonyoko wa udongo (soil erosion) unaosababisha na mvua na upepo milima imekuwa ikipungua kwa kiasi kidogo sana, kuna wanasayansi wanaoamini katika kinachoitwa "Isostacy theory"

Saturday, 9 April 2016

YAJUE HAYA KUHUSU UCHAFUZI WA MAZINGIRA

Na.Steven Mwakyusa
Uchafuzi wa mazingira umekuwa ukikua siku hadi siku kutokana na ongezeko la watu duniani likienda sambamba na kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu! Kuongezeka kwa uhitaji wa makazi, kukua kwa technolojia hasa uzalishaji katika viwanda, usafirishaji na kilimo vinatajwa kuwa sababu za kuongezeka kwa huu uchafuzi!
Uchafuzi wa mazingira umegawanywa kulingana na kitu kinachoathiriwa moja kwa moja, hapa tuna ardhi(land pollution), hewa(air pollution), maji (water pollution ) na kwengineko zinatajwa kelele(noise pollution)
Athari za uchafuzi wa mazingira zimekuwa kubwa, hasa kwa kusababisha magonjwa na kuua mimea pamoja na viumbe wa majini samaki wakiwemo. Joto limekuwa likiongezeka duniani (global warming ) na kusababisha mabadiliko makubwa ya hali ya hewa!!
‪#‎1 Mto‬ Ganges uliopo India unatajwa kuwa ndiyo mto uliothiriwa kwa kiasi kikubwa na "water pollution"
#2 Inakadiriwa kuwa watoto 1000 wanakufa kila siku nchini India kutokana na magonjwa yanatokana na uchafuzi wa maji.
#3 Kutokana na takwimu la Shirika la Afya Duniani (WHO), katika mji wa Mexico City watu 6400 wanakufa kila mwaka huku wengine zaidi ya 100,000 wakipata matatizo katika mfumo wa upumuaji kutokana na uchafuzi wa hewa(Air pollution)
#4 Kati ya mwaka 1956 na 1968 viwanda nchini Japani vilitupa madini ya Mercury moja kwa baharini, Mercury iliathiri samaki na baadaye mpaka walaji wa samaki na kupelekea watu wengi kuugua na wengine kufa!
#5 BMWs yanatajwa kuwa magari rafiki kwa mazingira huku Mitsubishi na Chyrister yakitajwa kuwa na uchafuzi zaidi wa mazingira. Ila kadri siku zinavyoenda ndivyo magari yanavyozidi kuboreshwa na kutoa moshi kidogo!!
#6 Inakadiriwa zaidi ya computer 130,000 zinatupwa kila siku wakati simu 100 million zinatupwa kila mwaka na kusababisha uchafuzi mkubwa.
#7 Viwanda nchini Marekani vinazalisha kemikali za sumu zinazofikia tani million 3 kila mwaka!

NB; Ukiliangalia suala la uchafuzi wa mazingira "locally" unaweza usione athari zake kwa haraka, ila kama utalitazama "globally", hatari iliyo mbeleni ni kubwa kuliko wengi tunavyifikiri. Japo kufuta kabisa huu uchafuzi ni jambo lisilowezekana, ni wajibu wa kila mmoja kujitahidi kulipunguza hili tatizo. Matumizi ya nishati mbadala kama gesi na solar badala ya mkaa na kuni yanasaidia kupunguza kiwango cha CO2 hewani, pia matumizi ya mboji badala ya mbolea za viwandani inasaidia hata pia kufanya "recycling" ya taka ngumu hasa za plastic!!

Wednesday, 10 February 2016

MIEZI SITA BILA YA JUA

Na.Steven Mwakyusa(Mtu makini)
Wakati ambao jua halizami kwa miezi 6, pia halichomozi kwa miezi 6 pia!!

Hili linaweza kuwa jambo geni na la kushangaza kwa walio wengi, ila ni jambo ambalo limekuweko toka kuwapo kwa hii dunia!!