ads
Showing posts with label Diamondplutnumz. Show all posts
Showing posts with label Diamondplutnumz. Show all posts

Monday, 5 June 2017

DIAMOND PLATNUMZ HAPITI NJIA ZA FEROUZ


Na. Mwanakalamu
Kwa kifupi katika harakati za kufikia na mafanikio hasa kwa kutumia sanaa washauri ni msaada mkubwa ni wale jamaa "Masela" ambao ukaribu wako na wao unawafanya wajitoe kwa hiari ama kwa kusukumwa na mazingira.
Unapofanikiwa wale jamaa wanakuwa na mategemeo makubwa ya kusaidiwa na wewe wengine wanataka pesa wengine watajidai wana vipaji vyenye uhusiano na sanaa yako ili tuu wapate mchongo...mfano kama wewe mwanamuziki atajidai ni Dj ili mwende sambamba kwa kuwa hana utaalamu na weledi wa kazi hiyo mambo mengi yataenda kisela na kukosa ubunifu mwishowe mwanamuziki huanguka.
Pia kundi hilo la masela usipolipa nafasi na kuangalia vigezo vya kitaa yaani achana na akina 'nanii' pale Tandale eti uwe na Sallam hawataki na hapo vita huanza kwa kuwa wanajua maisha yako ya nyuma na udhaifu wako basi watatumia kama fimbo kukunyong'onyesha na usipokuwa makini unaporomoka kabisa.
Diamond ni mfano mzuri wa watu walioamua kuacha taaluma na vipaji vifanye kazi na si usela na kujuana...
Ndiyo maana tulisikia hili na lile kumuhusu mengine ni kweli lakini waliokuwa wakimfahamu ndiyo waliopeleka kwa wale waliokuwa wakihisi ni maadui wa Diamond na kutumia kama fimbo.
Hii ilipelekea Diamond kurushiwa mayai viza kwenye show na mengineyo yote ni Diamond aliyakabili na sahizi anatumia mafanikio yake kuwajibu.
Ndiyo maana nacheka sana watu wanaposema ana 'show off za kipuuzi' kumbe hawajui nani anamkomoa kupooza yale machungu.Wengi hudhani Diamond kila akitupa dongo lamuhusu Kiba ,Diamond ana anaowalenga na ukiona kamlenga Kiba basi ni kwa ajili ya kukukuza bifu kwa ajili ya biashara yake.
Hivyo kuhit na kupotea huweza kuwa kwa sababu hizo.Lakini kuna wale wanaoridhika na kubweteka kama Sam wa Ukweli ambao walipopata yale mahitaji Muhimu waliyokuwa wakiyaota hawana ule uhitaji wa kutamani zaidi..mfano unatamani kuwa na pikipiki ukiipata hutamani tena gari ama gari zuri unarudi ulikotoka ukifurahia 'Kifekon' Chako.
Uvivu na ujinga ni sababu, yaani mtu anakuwa tuu mvivu matokeo yake lazima uishiwe.Pia kuna athari za kutumia madawa ya kulevya kwa 'kiwango kilichopitiliza' nimesema kwa kiwango kilichopitiliza kwani wanamuziki wengi pengine huwa na tabia ya kuyatumia madawa hayo wakiwa na pesa hupata uhakika wa kuyapata hivyo hupitiliza kile kiwango chao cha awali wakija kufilisika hawawezi kumudu tena kiwango hicho.
Pia wapo wanaohit tuu kama bahati... Mfano Chellea man na Baba levo

Friday, 7 October 2016

SALOME; BADALA YA KUMBEZA DIAMOND ANAHITAJI KUTIWA MOYO


Na.Mwanakalamu
Siku chache zilizopita mwanamuziki mahili nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla alitoa wimbo ambao alimshirikisha mwanamuziki mwenzake aliye chini ya lebo yake ya WCB.Ni wimbo ambao ulitokana na wimbo uliofanywa miakazaidi ya kumi na tano iliyopita na mwanamama Saida Karoli.
Ni wimbo ambaon ulikumbusha hisia na nyakati hizo ambapo muziki wa bingo ffleva ndio kwanza ulikuwa ukifurukuta na kujitutumua ukijaribu kufunika zile nyimbo za nje na zile za asili ambazo hazikuwa zimefanikiwa kuteka hisia za wapenzi wengi wa muziki nchini.
Baada ya kuusikia ule wimbo nilitegemea mambo manne la kwanza ni kupongezwa kwa kufanya kitu ambato wengi waliona ni kigumu kufanyika kwa hofu ya kutafsiriwa kuwa 'wamefulia'.
Jambo la pili ni kebehi na kashfa kutoka kwa wasiomtakia mema mwanamuziki huyo ambaye muziki wa Tanzania una alama yake kubwa hadi sasa.Hawa ni wale ambao walimtabiria mwanamuziki huyo kushindwa hivyo daima hutafuta wapi aliposhindwa hivyo hujaribu kuunga unga unga kasoro ili tabiri zao zionekane kutimia.
Lakini jambo la tatu nililotegemea ni kukutana na wale watetezi na wafuasi wa muziki wa Diamond na wapenzi wengine wa muziki wakifunua nyimbo mbalimbali ambazo zilirudiwa duniani ili 'kuhalalisha'hiki alichokifanya Diamond.Pia nilitegemea kukutana na makala zinazojaribu kuwaelimisha 'hatters'ambao kwa mtazamo wangu hawahitaji elimu bali maombi ya kutolewa roho mbaya juu ya watu wanaofanikiwa.
Jambo la mwisho ambalo nililitegemea ni kuhusu kuibuka kwa watu ambao watajidai wanamtetea mwanamama Saida Karoli wakidai kuwa Diamond kamdhurumu na Diamond angeibuka na kutoa ushahidi wa taratibu kufuatwa katika kuurudia wimbo huo.
Hayo yote yalitokea na lakini hadi leo bado wadau wa muziki wanapata wasiwasi na shaka juu ya hiki alichokifanya Diamond wakisahau kabisa Mpango wa kurudia nyimbo za zamani uliffanyika hapa nchini japo haukuwa na mafanikio makubwa kama ilivyo kwa wimbo huu wa Salome ambao nina hakika utaleta tunzo nyingi huko mbele na heshima ya muziki wetu ambao daima tumeonekana tukichukia kusikia ladha za Naija.
Ilishafanyika kwenye Kimasomaso na Alikiba ambapo wimbo haikupewa heshima walau ya kufanyiwa video tena ukitolewa na wimbo mwingine ambao mwanamuziki huyo aliufanya kama ''comeback'' yake.Pia huenda aliyetoa wazo hilo ndugu Joseph Kusaga aliwaachia jukumu lote wanamuziki ambao walikuwa kwenye mpango wa kuzirudia nyimbo za kale.
Mwanafa pia aliirudia Yalaiti ya Bi kidude chini ya project ya KUsaga hii walau wimbo huu ulipata na video na kusumbua kwenye chati mbalimbali za muziki.
Lakini Diamond ameamua kuwekeza kwenye wimbo huu kama ilivyo kawaida yake ya kuipa thamani bidhaa yake yoyote, wimbo ambao kiukweli umetupa kile ambacho alikuwa akituhumiwa kukiua kwa muda sasa; Ubongofleva halisi ambao ulionekana kumezwa sana naUnigeria ambao haina ubishi ulimfungulia njia za kimataifa.Ametupa kile ambacho akina Navy kenzo na Banana Zorro wamekuwa wakitupa kila watoapo nyimbo.

Navy Kenzo wamekuwa wakitupa Mellody za Kiafrika zenye asili ya Tanzania kama ambazo leo hii Diamond ametupatia kwenye Salome ana Rayvany amemwonesha bosi wake kuwa hakukosea kumsainisha kwenye lebo yake.
Mwisho nawaomba watanzania kumpongeza Diamond kwa uamuzi huu ambao si tuu umemwamsha Saida Karoli kutoka kwenye usingizi mzito aliolala ama aliolazwa baada ya kukata tamaa baada ya kufanya kazi nzuri kwa muda mrefu na kuambulia mapato kidogo bali umeipa thamani muziki wa bongo kwa 'levo' aliyofikia Diamond ni ukweli usiopingika sauti ya simba imevuma nyika zote.
Diamond anatakiwa kupewa moyo aendelee na ujasiri huu ili hata keshokutwa Ben Paul akiurudia wimbo wa Mb Dog ama Maua Sama akiimba wimbo wa Stara Thomas asitarajie kukejeliwa.
Viva Diamond Viva Tanzania.
Nawasilisha.

Sunday, 15 May 2016

KUVUNJIKA KWA NDOA HIZI ZA WASANII MWANZO WA MAFANIKIO YAO


Na.Mwanakalamu
Wiki chache zilizopita taarifa ya Mo Music kuachana na menejimenti yake iliyomtoa baada ya kutomfanyia kile awalichokuwa wamekubaliana zilitoka na kuzua mijadalaa kadhaa miongoni mwa wadau wa muziki.Kuna wale waliokuwa wakikubaliana na uamuzi wake lakini kulikuwa na wale waliokuwa wakipingana na uamuzi wake huku hoja na tabiri mbalimbali juu yake na muziki wake zikitolewa.Mo Music si mtu wa kwanza kuachana na menejimenti iliyomtoa kuna wengi waliwahi kauchana na wale waliokuwa chachu ya kujulikana kwa kwenye muziki japokuwa kila mmoja alitoka kwa njia yake na maneno aliyoyajua.
Zifuatazo ni ndoa za wanamuziki zilizovunjika na kuleta neema kwa wanamuziki;-
Diamond Vs Sharobaro Records
Hii ilikuwa baada ya tukio la kulipuka kwa mabomu ya Gongo la Mboto, ambapo kwa mujibu ya maelezo yao kwenye vyombo vya habari kuwa Diamond alitaka kurekodi wimbo kwa ajili ya kuwapa pole waathirika lakini Bob Junior aligoma kwa sababu ambazo hadi leo zinachanganya kumbukumbu zetu.Kwani Diamond alidai Bob Junior alikataa kumrekoria wimbo huo huo bure akidai hadi alipwe pesa lakini Bob Junior naye akadai kuwa wakati anaombwa kurekodi wimbo huo alikuwa amepata matatizo yamasikio kuuma hivyo alimwomba Diamond awe na subira  akikanusha habari za kudai pesa kabla ya kazi kwani alikuwa ametayarisha albam ya kwanza ya Diamond bila malipo.
Huo ukawa mwanzo wa kutengana kwa Diamond na studio hiyo ambayo alikuwa ameizoa na akaenda kwa Maneck kurekodi wimbo wa Gongo la Mboto alioimba na Mrisho Mpoto.Baadaye akaenda kwa Lamar  akatengeneza moyo wangu ambapo waandishi na wadau wengi walizidi kumkosoa na kudai kuwa alikuwa amepotoka kwa uamzi huo na alikuwa akijizika mwenyewe.
Lakini tofauti na tabiri za wakosoaji wengi Diamond alianza kupanda ngazi hadi leo hii ukiwataja wanamuziki watano wa Afrika huwezi kumwacha Diamond na anastudio yake na Music lebel ya WCB.Lakini kitu cha kushukuru kwa sasa ni kwamba watu hawa wamemaliza tofauti zao na tunategemea kolabo kati ya Bob Junior na Diamond.

Tundaman Vs Spark
Hawa walikuwa maswaiba kweli na uimbaji wao ulikuwa umezoea masikio ya wadau wengi wa muziki.Walifanikiwa kutoa albamu ya pamoja iliyokuwa na ngoma nyingi kali ambapo wlaipata kuwashirikisha wakali kadhaa wa bongo fleva kama Madee na Chid Benz.Mafanikio ndiyo ynasemwa kuwa ilikuwa ni chanzo cha ugomvi wao huku kila mmoja akidai ndiye mtunzi wa wimbo uliobeba ushirikiano wao ‘’Nipe Ripoti’’ walimshirikiasha pia Madee.
Kutengeana kwao kukampoteza Spark ambapo wadau wengi wa muziki hatujui alinachokifanya mara baada ya kutoa wimbo wake wa ‘’Tangu nitoke jela’’ lakini Tundaman ni kama alikuwa amepata  Baraka baada ya kuvunjika kwa ushirikiano wao ambapo ameweza kudumu kwenye ‘game’ akitoa ‘hits’ kadhaa ambapo kwa sasa Mama kijacho bado inasumbua masikio ya wadau wengi wa muziki.

AY&FA Vs East Coast Team
East Coast team ni kati ya makundi makongwe ya muziki ambayo yaliwahi kuuteka muziki wa Tanzania yakiwajumuisha wakali kadhaa kama GK, AY , FA na wengine lakini ghafla AY NA FA wakajitoa kundini huku wadau wengi wa muziki tukiachwa vinywa wazi baada ya kutojua sababu ya watu hao kujitoa.
Wengi hawakuamini kama AY na FA wangeweza kusurvive wakiwa peke yao lakini tofauti na tabiri za wengi wakali hao wakajiundia umoja wao ambapo walifanikiwa kutoa nyimbo kadhaa ambazo zililikamata soko la muziki wa bongo.Walitoa pia Albam ya pamoja iliyokuwa ni moja ya albam bora za muziki wa Hip hop nchini.Miaka kadhaa baadaya ya kundi hilo kuachwa na wawili hao ni kama limekufa kwani  halisikiki tena kwa ngoma kali huku wakionekana kutoendana na mabadiliko katika muziki wa bongo.
Kwa hiyo tunaweza kusema kujitenga kwao na kundi hilo AY na Fa kulikuwa ni njia ya mafanikio yao.
Kasim Mganga Vs Tip Top
Kasim Mganga, tajiri wa Mahaba kutoka Manzabay kule kule kwa Mb Dog alifanikiwa kutoa hits kadhaa  akiwa chini ya Tip top.Alipojitoa Tip top wengi walitabiri kuwa ulikuwa ni mwanzo wa kupotea kwenye muziki ikizingatiwa kuwa Tip Top walikuwa kama wameukamata muziki wa bongo na wengi walikuwa wakitamani kuwa chini ya uongozi huo.
Lakini Kasim akaziba masikio na kuchukua njia yake na baada ya muda mfupi kasim aliendela kupanda ngazi huku ujuzi wake wa kulichezea koo likatoa sauti mwanana na akili yake ikitoa mashairi murua kuhusu mahaba  vikimfanya azidi kuwa kwenye ramani ya muziki Bongo.
Dogo Janja Vs Ustadh Juma
Wengi tulimfahamu Dogo janja baada ya kufika Tip top huku Madee akiwa moja ya sababu ya kufika hapo ambapo kupitia kipaji chake akajikuta akisomeshwa na Madee.Baada ya miezi kadhaa ya umaarufu Dogo Janja akaonesha ujanja wake na kudai alikuwa akinyonywa na Madee na uongozi wa Tip Top ukila zaidi jasho lake zaidi ya alivyokuwa alilila mwenyewe , aaacha shule na kufanya mahojiano na vyombo vingi vya habari akitoa shutuma nyingi kwa Madee na uongozi mzima wa Tip top.Miezi michache baadaye Dogo Janja alizidi kuonesha ujannja wake kwani alipokelewa kwa mbwembwe uwanja wa Ndege akiingia kwenye menejimenti mpya alikwa Ustadh Juma almabye aliamua kumchukua.Chini ya menejimenti hiyo Dogo Janja akatoa jiwe kali la ‘’Ya moyoni’’ ambamo alimshirikisha PNC.KATIKA ‘Ya MOYONI’ Dogo janja aliyatoa kweli ya moyoni huku zile shutuma ambazo wengi tuliamini  penmgine zilitoka kwa bahati mbaya  zikisikika kwenye wimbo na kumfanya wengi kumhurumia  kwa mteso aliyokuwa akiyapata chini ya Tip Top.Akaja na nyimbo nyingine kadhaa ambazo hazikueleweka miongi mwa wadau wa muziki hadi pale tuliposikia karudi tena Tip top akiomba msamaha na kuachia wimbo wa my life ambao bado unafanya vizuri na umemrudisha kwenye chati ya wanamuziki wenye matamasha.
Kurudi Tip Top na kuachana na Ustadh Juma ni kama kumemfungulia njia kwani leo hii unapomzungumzia Dogo Janja unamzungumzia mmoja wa wanamuziki wenye magari yao.

Naomba kuwasilisha; Niambie ni ndoa gani nyingine kwenye muziki ilivunjika na kuleta neema kwa mwanamuziki, niandikie hapa chini.

Thursday, 14 April 2016

NYIMBO KUMI AMBAZO DIAMOND PLUTNUMZ HATOZISAHAU!


Na.Mwanakalamu
Diamond ni habari ya Afrika, ametoka kufanya matamasha ya muziki makubwa barani Ulaya na Marekani na kuteka hisia za wapenzi w muziki wake kila anapotumbuiza.
Ametoka wapi huyu Milionea ambaye kila akanyagapo panageuka dhahabu?
Mwenyewe anasema ''From Tandale to the World''.
Naam katoka Tandale ambako ''alihaso' sana kabla ya kutoboa , alianza kwenye sifuri hadi kwenye tunayoiona mia ila kwake anaweza akasema ndo kwanza yupo arobaini, nani alikuwa anajua kuwa angefika alipofika?
Naamini hayupo na kama wapo basi ni wachache sana na huenda hao wachache walikuwa wakimwombea tuu hayo ama wakiota, lakini ni kweli amefika ambapo kwa jicho na akili ya kawaida hakuna ambaye angewaza.
Alipochukua tunzo nyingi Bongo angebweteka lakini hakufanya hivyo akapiga hatua, alipotajwa kuwania tuzo za BET angejisahau lakini alikaza mwendo na hata alipochukua AFRIMA ahakusimama na hatimanye tunzo hizo zikamzoea akazibeba za kutosha na Mtv nazo zikaweka kambi kwake, lakini hajasiama leo hii kavuka mabara , anafahamika kwote huko na bado anapiga hatua.
Najua ni funzo kwako kijana na hata mzee unayeridhika , kwa kidogo tuu ukipatacho.
Kama nilivyosema awali , kijana huyu alianzia sifuri ambako ni watu wa mtaani kwake na mitaa ya jirani pekee ndip waliojua kipaji chake hadi alipofika leo , leo tutaangalia nyimbo kumi ambazo daima atakuwa akizikumbuka na kuziwekea uzito kila akizisikia.
1.KAMWAMBIE
Huu ni wimbo ambao ulitufanya wapenzi wengi wa muziki tumtazame kijana huyu kwa jicho la ziada.Ulikuwa ni wimbo wa nguvu ambao bila shaka hautosahaulika kichwani mwake kwani ndio ulimtengenezea njia nchini na hata nchi za jirani zinazotumia kiswahili.
2.MBAGALA
Kikawaida mwanamuziki hupimwa na wimbo wa pili kama kweli anakipaji ama alibahatisha wimbo wake wa kwanza.Lakini Diamond alithitisha kipaji chake kwa wapenzi wa muziki kwa kutoa wimbo huu ambao uliikamata Afrika mashariki na kumfanya atazamwe kama moja ya wasanii wakali ambao walikuwa wanakuja kuikamata Tanzania.
Wimbo huu pia ulimfungulia njia ya kimataifa kwani ulifanikiwa kuingia kwenye kuwania tunzo za muziki za Mtv licha ya kutoshinda.
Bila shaka yoyote utakuwa umebaki kwenye kumbukumbu zake daima.
3.NALIA NA MENGI
Wimbo huu ambao aliuimba na Rapa Chid Benz ulionekana kubeba hisia nyingi za maisha yake na ujumbe mzito.Nadhani historia ya maisha yake ilimsukuma kuandika wimbo huu ambao licha ya kutotamba sana redioni ulibaki kwenye 'playlist' za watu wengi wakiusikiliza ujumbe huo.
Kwa kubeba historia yake ya maisha daima wimbo huu hautosahaulika kwake.
4.MOYO WANGU
Yaap! hapa ndipo patamu, ilikuwa ni baada ya kutoka kwa Bob Junior ambako alikuwa ameshatengeneza albam nzima , lakini matatizo katika kutengeneza wimbo wa gongo la mboto yakamfanya kijana huyu kutoka Mbagala ajiongeze na kuanza kurekodi kwingine na akaanza Fishclub kwa Lamar ambaye kwa kipindi hicho alikuwa moto wa kuotea mbali.
Moyo wangu licha ya kuonekana ni wa kawaida mwanzoni ulikuja kuikamata Afrika mashariki na kuwa moja ya nyimbo bora kuwahi kutokea kutokana pia na ubunifu wake kwenye video.
Bila shaka wimbo huu ulikuwa ni mwanzo wa mabadiliko ya kimtazamo wake katika muziki na kuwa moto wa kuotea mbali.
5.NUMBER ONE
Wimbo huu unaweza ukawa ulimlipa na kumpooza mateso aliyokuwa amepitia kwani ulimpa nguvu ya kuvunja rekodi katika tunzo za muziki za Kili na kumfungulia vizuizi vingi vya kimataifa nakisha kumuweka juu.
Number one wimbo ambao huenda kila akiusikia anajikuta akicheka sana kwani ulipelekea kufanyika kitu ambacho nacho huenda hakukifikiria awali.
6.NUMBER ONE REMIX
Huu ni zao la number one ambao aliamua kufanya na Davido ambaye ni kama walicheza bonge la kete kwani Davido akajenga ngome Bongo na Diamond akatoboa.
Wimbo huu ukampa tunzo na njia zaidi za kwenda mbele kimataifa na 'koneksheni' nyingi zilianzia hapa.
Diamond Plutnumz akiusikia huu wimbo huenda akafungua jokofu na kuchukua maji ya baridi na kuyanywa maana anaweza furahi hadi akazidiwa.
7.MDOGO MDOGO
Nilipofanikiwa kuiona 'Behind scene' ya video ya wimbo huu, ilikuwa ni zaidi ya kutafuta, hapo nilimwona Diamond ni mtu wa tofauti na wa ajabu sana , licha ya jina lake na mapesa aliyokuwa nayo alikubali kupigwa na baridi kali la mji mmoja aliopo Afrika kusini ili tuu atengeneze video ya wimbo huu.Hakika yalikuwa mateso angeweza kumfanya mtu mwingine achukue uhusika wa mahali pale ambapo ilimpasa kuteseka ,lakini aliamua kuifanya kazi kwa ukomavu wa hali ya juu na hatimaye wimbo huu uliweza kumuweka kwenye 'levo' za juu barani Afrika.
Akikumbuka lile baridi lazima anyooshe miguu na kucheka kwa furaha.
8.NITAMPATA WAPI
Ni kati ya nyimbo kubwa zilizoweza kumpatia tunzo nyingi za muziki ndani na nje ya Tanzania.Mashairi yake mazuri ,melody kali na video ya kuvutia viliufanya wimbo huu kuwa moja ya nyimbo nzuri barani Afrika ambapo licha ya tunzo ulikuwa ukimpa michongo mingi ya matamasha.
Kweli kwake tatizo halikuwa nyota.
9.NANA
Nana ni wimbo ambao kikawaida tulitegemea ungekuwa ukishindania tunzo mwaka huu lakini mara tuu ulipotoka ulianza kuzoa tunzo nyingi za nje ya nchi.Nana ni moja kati ya nyimbo ambazo huenda alipozitoa hakutegemea makubwa sana lakini wimbo huu umevunja rekodi nyingi ambazo zitamfanya asiusahau.
10.MAKE ME SING
Ulikuwa kama wa kawaida alipoutoa lakini ghafla ukaeleweka na sasa ni moto wa kuotea mbali.Ni wimbo mkubwa si Afrika tuu bali hata alipofanya matamasha nje ya Afrika wimbo huu ulioneke]ana kuwavutia wengi, naamini utakuja kushinda tunzo nyingi za muziki ndani na nje ya Afrika.
Hawezi kuusahau kwani ni motoooo.
Kuna nyimbo nyingi ambazo Diamond Plutnumz hatozisahau lakini hizi ni baadhi ya nyimbo ninazoaminin kutokana na kuwa na historia na mafanikio mbalimbali zitabaki kichwani mwa mtunzi daima.Kumbuka haya ni maoni na mtazamo wangu na si maoni yake na huenda tukatofautiana kabisa nimejaribu tuu kubashiri kwa kusoma matukio na nyakati.
Je, we unaonaje mwanakalamu?
Ungependa nimwandike nani safari ijayo?
Share na wenzako ifike mbali.