ads

Friday, 7 October 2016

SALOME; BADALA YA KUMBEZA DIAMOND ANAHITAJI KUTIWA MOYO


Na.Mwanakalamu
Siku chache zilizopita mwanamuziki mahili nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla alitoa wimbo ambao alimshirikisha mwanamuziki mwenzake aliye chini ya lebo yake ya WCB.Ni wimbo ambao ulitokana na wimbo uliofanywa miakazaidi ya kumi na tano iliyopita na mwanamama Saida Karoli.
Ni wimbo ambaon ulikumbusha hisia na nyakati hizo ambapo muziki wa bingo ffleva ndio kwanza ulikuwa ukifurukuta na kujitutumua ukijaribu kufunika zile nyimbo za nje na zile za asili ambazo hazikuwa zimefanikiwa kuteka hisia za wapenzi wengi wa muziki nchini.
Baada ya kuusikia ule wimbo nilitegemea mambo manne la kwanza ni kupongezwa kwa kufanya kitu ambato wengi waliona ni kigumu kufanyika kwa hofu ya kutafsiriwa kuwa 'wamefulia'.
Jambo la pili ni kebehi na kashfa kutoka kwa wasiomtakia mema mwanamuziki huyo ambaye muziki wa Tanzania una alama yake kubwa hadi sasa.Hawa ni wale ambao walimtabiria mwanamuziki huyo kushindwa hivyo daima hutafuta wapi aliposhindwa hivyo hujaribu kuunga unga unga kasoro ili tabiri zao zionekane kutimia.
Lakini jambo la tatu nililotegemea ni kukutana na wale watetezi na wafuasi wa muziki wa Diamond na wapenzi wengine wa muziki wakifunua nyimbo mbalimbali ambazo zilirudiwa duniani ili 'kuhalalisha'hiki alichokifanya Diamond.Pia nilitegemea kukutana na makala zinazojaribu kuwaelimisha 'hatters'ambao kwa mtazamo wangu hawahitaji elimu bali maombi ya kutolewa roho mbaya juu ya watu wanaofanikiwa.
Jambo la mwisho ambalo nililitegemea ni kuhusu kuibuka kwa watu ambao watajidai wanamtetea mwanamama Saida Karoli wakidai kuwa Diamond kamdhurumu na Diamond angeibuka na kutoa ushahidi wa taratibu kufuatwa katika kuurudia wimbo huo.
Hayo yote yalitokea na lakini hadi leo bado wadau wa muziki wanapata wasiwasi na shaka juu ya hiki alichokifanya Diamond wakisahau kabisa Mpango wa kurudia nyimbo za zamani uliffanyika hapa nchini japo haukuwa na mafanikio makubwa kama ilivyo kwa wimbo huu wa Salome ambao nina hakika utaleta tunzo nyingi huko mbele na heshima ya muziki wetu ambao daima tumeonekana tukichukia kusikia ladha za Naija.
Ilishafanyika kwenye Kimasomaso na Alikiba ambapo wimbo haikupewa heshima walau ya kufanyiwa video tena ukitolewa na wimbo mwingine ambao mwanamuziki huyo aliufanya kama ''comeback'' yake.Pia huenda aliyetoa wazo hilo ndugu Joseph Kusaga aliwaachia jukumu lote wanamuziki ambao walikuwa kwenye mpango wa kuzirudia nyimbo za kale.
Mwanafa pia aliirudia Yalaiti ya Bi kidude chini ya project ya KUsaga hii walau wimbo huu ulipata na video na kusumbua kwenye chati mbalimbali za muziki.
Lakini Diamond ameamua kuwekeza kwenye wimbo huu kama ilivyo kawaida yake ya kuipa thamani bidhaa yake yoyote, wimbo ambao kiukweli umetupa kile ambacho alikuwa akituhumiwa kukiua kwa muda sasa; Ubongofleva halisi ambao ulionekana kumezwa sana naUnigeria ambao haina ubishi ulimfungulia njia za kimataifa.Ametupa kile ambacho akina Navy kenzo na Banana Zorro wamekuwa wakitupa kila watoapo nyimbo.

Navy Kenzo wamekuwa wakitupa Mellody za Kiafrika zenye asili ya Tanzania kama ambazo leo hii Diamond ametupatia kwenye Salome ana Rayvany amemwonesha bosi wake kuwa hakukosea kumsainisha kwenye lebo yake.
Mwisho nawaomba watanzania kumpongeza Diamond kwa uamuzi huu ambao si tuu umemwamsha Saida Karoli kutoka kwenye usingizi mzito aliolala ama aliolazwa baada ya kukata tamaa baada ya kufanya kazi nzuri kwa muda mrefu na kuambulia mapato kidogo bali umeipa thamani muziki wa bongo kwa 'levo' aliyofikia Diamond ni ukweli usiopingika sauti ya simba imevuma nyika zote.
Diamond anatakiwa kupewa moyo aendelee na ujasiri huu ili hata keshokutwa Ben Paul akiurudia wimbo wa Mb Dog ama Maua Sama akiimba wimbo wa Stara Thomas asitarajie kukejeliwa.
Viva Diamond Viva Tanzania.
Nawasilisha.

0 comments:

Post a Comment